Mliobahatika kuacha unywaji wa pombe mlitumia formular gani?

Mliobahatika kuacha unywaji wa pombe mlitumia formular gani?

Niliona hii video ya mkongo akielezea namna ya kuacha pombe, huenda ikakusaidia.

Mimi bado naendelea kupiga kamnyweso maana hakajanipelekea kujuta.


 
Pole sana mkuu unaweza kuacha ukiamua.

Mimi nilikuwa hivyo ila leo ni siku ya 5 sijanywa pombe na ninapoandika hapa niko bar na mshikaji tumeagiza crate la bia tunakunywa kusheherekea mimi kuacha pombe huu mwaka.

We jamaa hiyo chupa ulioiweka hapo unatuingiza majaribuni😀😀.anyway ukitaka kunywa pombe bila hasara epuka washkaji,halafu uwe unaenda sehemu tulivu sio zile baa kubwa kubwa...
 
Pole sana mkuu unaweza kuacha ukiamua.
Mimi nilikuwa hivyo ila leo ni siku ya 5 dijanywa pombe na ninapoandika hapa niko bar na mshikaji tumeagiza crate la bia tunakunywa kusheherekea mimi kuacha pombe huu mwaka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daah! Noma sana mkuu
 
Kwa MUNGU yote yanawezekana. Jenga Imani kwamba sasa pombe basi. Kisha chukua hatua, Nenda Kawe kwa Mtume Mwamposa Ndugu. Utahudumiwa kiroho na utapona kama kweli Moyoni umejuta.

Usipopona ni PM nitakurudisha nauli Yako!
 
Kwa MUNGU yote yanawezekana. Jenga Imani kwamba sasa pombe basi. Kisha chukua hatua, Nenda Kawe kwa Mtume Mwamposa Ndugu. Utahudumiwa kiroho na utapona kama kweli Moyoni umejuta.

Usipopona ni PM nitakurudisha nauli Yako!
Asante sana kwa Ushauri. Ila huwa naona kama pale kawe watu ni wengi sana. Nitapata nafasi kweli??
 
Wakuu heshima kwenu

Nakuja hapa nikiwa na Tatizo moja kubwa sana la unywaji wa Pombe (Beer). Tatizo hili limekuwa kubwa sana kiasi kwamba ni kama nashindwa kuji Control hasa ninapokuwa na pesa mfukoni, Yaani nikiwa na pesa tu basi nitatafuta kiwanja nitapiga mitungi mpaka mida mibaya na kesho yake kuendelea tena hivyo hvyo angalau mpaka pesa ile iishe

Pombe imeniletea matatizo makubwa hasa kifamilia, Nimegombana na Wife nimegombana na michepuko na nimegombana na ndugu pia. Kwa ufupi ni kama nimetengana na wife kwa namna fulani maana kila mtu anakaa kwake kwa sasa

Pombe imenisababishia kupata ajali na kupoteza gari yangu nzuri kabisa

Pombe inaniingiza kwenye hasara nyingi kwenye biashara na kazini, Kwani kuna wakati nakuwa na hela ya offisi ila mm naamua kuipasua pombe na kunywesha watu mpaka inaisha. Imagine naweza kuteketeza laki 8 ndani ya siku mbili au Tatu, Na nisijue imeenda wapi

Pombe imeniingiza kwenye madeni mengi hasa kwenye Bar mbalimbali wanazoniamini maana wanajua mm ni mnywaji na mlipaji mzuri so huwa wananikopesha mpaka kiwango cha malaki kadhaa na mwisho wa siku najikuta nimeingia kwenye madeni kama hayo.

Pombe pia imeniingiza kwenye madeni na marafiki na ndugu mbalimbali ambao huwa wananikopesha na mimi kushindwa kurejesha maana kuliko nilipe deni ni bora nikakae kwanza ninywe beer mbili tatu nikiwa nafikiria kukulipa hilo deni lako ndugu mdeni.

Pombe inanifanya nashindwa kwenda kanisani Jumapili maana kila jumapili asubuhi nakuwa nipo hoi either kwa pombe za jana yake au kwa pombe nilizoanza kuzipasua jumapili hiyohiyo asubuhi

Jamani ndugu zangu nafanyaje kuachana na huyu adui pombe, Hapa nilipo nasubiri saa 11 ifike nikapate kitimoto then nianze kushushia vitu.

Pombe inanifanya nasahau kununua nguo nzuri na viatu naona ni bora pesa nipeleke Bar , Yaani kuliko nikafanye shopping ya Laki mbili ni bora hiyo hela nikainywe beer za laki mbili.

Pombe inanifanya sasa nasahau au nashindwa kutuma mahitaji ya watoto kwanzia shule na nyumbani.

Mimi sio mtu wa wanawake sana ila kuna wakati pombe inanifanya pia najiingiza kwenye mambo ya Uzinzi japo ni mara mojamoja ila huwa najuta sana.

Jamani ndugu zangu nafanyaje mimi??

Huwa najaribu kuacha mara kadhaa lakini nikija kurudi ndio inakuwa balaa zaidi yaani inakuwa mara tatu ya ule unywaji kabla ya kuacha.

Kuna muda natamani hii inchi yetu ingekuwa kama zile nchi za waislamu ambazo hawaruhusu pombe , maana ingekuwa hivyo kweli ningeacha. Ila sasa ndio kila nikipita barabarani naona matangazo ya beer, Nikisikiliza redio naona beer yaani ni mtihani kwa kweli

Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disaster

Baada ya kusema hayo yote tafadhali naomba ushauri wenu kwa ambao mmefanikiwa kuachana na pombe mlifanyafanyaje , TAFADHAL SANA naomba ushauri wenu

MWISHO WA UZI

View attachment 2495275
Pombe inaniingiza kwenye hasara nyingi kwenye biashara na kazini, Kwani kuna wakati nakuwa na hela ya offisi ila mm naamua kuipasua pombe na kunywesha watu mpaka inaisha. Imagine naweza kuteketeza laki 8 ndani ya siku mbili au Tatu, Na nisijue imeenda wapi

Nipe location tuyajenge
20230125_142221.jpg
Snapchat-324686400.jpg
 
Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disaster
Mkuu kwamba kikao kifanyike bar na mbili tatu pembeni😀😀
 
Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disasterView attachment 2495291
 
Hili limewapata wengi haswa jika la vijana 25+ huwa tunajilipua sana ila kadri unavyoongeza umri unaanza taratibu kupunguza na kuwa na stable budget kwa ajili ya kila siku
 
Back
Top Bottom