Mliofanikiwa kutoa Zaka asilimia 10% ya vipato vyenu mmewezaje? Binafsi naishia kusaidia 2% hadi 4%

Namdanganya kvp.? Kwahy kama hana pesa ya kutoa 10% au majukumu yake yanambana mpaka kushindwa hy 10%. unataka akaibe.?
Kasema anaingiza 2m,,, Ivo 2m ashindwe kumtolea MUNGU 200k kwel?
 
Duuh mafundisho yapi haya mkuu😄 mkuu pole Sana umepotea haswa
 
Paye sio fungu la kumi .Imeandikwa mpeni kaisari vilivyo vyake kaisari (vikamsaidie kutawala ) na mpeni Mungu vilivyo vyake Mungu( vikatumike kujenga ufalme wa mungu) .
Fungu la kumi kwenye biblia halijaelezwa kwa mafumbo ni kwamba asili yake ni israel ilikuwa na makabila 12 .kabila moja liliitwa walawi wao walikuwa kazi yao ni kuwa viongozi wa kidini .kuwasiliana na Mungu kwa niaba ya kabila zingine na kutunza mahekalu.wao walikuwa hawapaswi kuwa serious sana na uzalishaj mali .hivyo kabila zingine zilipaswa kutoa fungu la kumi kwenda hekalun ili kulipa mishahara walawi na ziada kutumika kulea yatima na wajane na shughuli za usambazaji na ufundishaji neno la mungu.
Usitoe fungu la kumi iwapo?
1.Mapato yako si halali ikiwemo pesa ya kubet .kudanga
Rushwa etc
2.usitoe kama huna hakika haiendi moja kwa moja kulea yatima wajane au kulipia shughuli za kujenga ufalme wa mungu
3.Fungu la kumi likitolewa kanisani ni mali ya kanisa sio mchungaji .Viongozi wa kanisa wanapaswa kupima mahitaji yake hususan kulea familia malazi makaz chakula na afya ya familia yake tuu.mambo ya akitaka utajiri atafute mwenyewe aidha naye anapaswa alipe fungu la kumi
4.hivyo ukiona huamini mfumo wa kanisa lako unaweza amua kupeleka kwa yatima vitu sio hela kama mablanket .dawa .kuwatibu .kumbuka kwenye vituo kunaupigaji sana simamia hilo.Fungu la kumi lina jukumu kulea viongozi wa dini .mtembelee kiongozi unaeamini wa kweli mnunulie kitu unaamini kinaboresha huduma yake .mfano wa kijijini mnunulie bodaboda itafanya asimamie vyema kazi za kanisa .au mnunulie kwa walokole suti .mpe offa ya full check up ya afya na matibabu etc mnunulie simu nzuri awasiliane vyema na waumini
Ila kwa makanisa yenye mpangilio kama mfano roman catholic weka tu madhabahuni wao wananamna ilopangiliwa inafikia yatima na wajane straight na mapadre wanaishi kawaida hawastarehe na sadaka .huwezi kuta hata kardinali anagari la kifahali kama mzee wa upako
 
Wapi imeandikwa usitoe pesa ya kubeti au kudanga?
 
Hapo mwisho umeharibu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu hongeea sana kwa kuanzisha huu uzi.Naamini una imani na hofu ya Mungu juu yako.Ni wengi sana tunamwibia sana Mwenyezi Mungu kwa kushinda kumtolea zaka kamili.Na katika sehemu ambayo Mwenyezi Mungu kaahidi kutenda/kujibu kwa wakati maombi yetu mbalimbali basi ni kupitia zaka.Nina ushuhuda juu ya hili.Ukifuatilia Malaki 3:8-11.Utaona.
 
Hakika mkuu,umenena vyema
 
Zak ni 10% na Sadaka ni 10% = 20%

20/100 × 50000 = 10,000 Zaka na Sadaka Jumla.

Zaka na Sadaka ni Kwa ajili ya kueneza Injili na Kwa ajili ya Watoainjili. Inatolewa kanisani au Kwa utaratibu mwingine uliotolewa na kanisa.
 
Hivi kwenye Agano Jipya Nyakati za Yesu Kristo je Kuna mahala alifundisha kuhusu kutoa Zaka ?
 
Kutoa ni moyo, si utajiri. Na unatoa kwa kadiri ya uwezo wako, ukijifilisi itakuwa aje?
 
Mimi ni mzito wa kutoa asilimia 10, hasa kwa kuwa sijui zinaenda wapi kumnufaisha nani? Hivyo sitoi. Ila kwa wenye uhitaji, najaribu ninachoweza.
 
Nani mwaminifu wa kupokea zaka, kwa matumizi gani au inakuwa kama unaitupa tu bora nia yako ni kutoa zaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…