Mliofanikiwa kutoa Zaka asilimia 10% ya vipato vyenu mmewezaje? Binafsi naishia kusaidia 2% hadi 4%

Zaka ni ishara ya utii kwa Mungu, na Sadaka ni ishara ya upendo kwake.

“Mpende Bwana Mungu wako...”

Kutoa zaka na sadaka ni kutekeleza amri za Mungu.

Kama unaye Mungu.
Mkuu naomba mafundisho ya Yesu yanayotufundisha kuwa zaka ni lazima
 
Hadi hapo nakutangazia amani malangoni pako na wanao watajaa amani .Milango unayoitikisa kwa hicho unachoita kidogo ikumbuke comment hii ndani ya 2 to 5 yrs utakuwa mwingine kabisaaa.
Mimi waga inarudi maradufu ndani miezi kadhaa tu..halafu sio kwa hela tu bali na baraka nyingine ..haya mambo zamani nilikuwa siamini ila aisee ni kweli
 
Zak ni 10% na Sadaka ni 10% = 20%

20/100 × 50000 = 10,000 Zaka na Sadaka Jumla.

Zaka na Sadaka ni Kwa ajili ya kueneza Injili na Kwa ajili ya Watoainjili. Inatolewa kanisani au Kwa utaratibu mwingine uliotolewa na kanisa.
Asilimia 10 ya faida au mapato?
Nipe huo mfano kwa mfanyabiashara mwenye mtaji wa 500,000 yeye zaka yake unacalculate vipi
 
Mkuu kwa maelezo yako hapo hakuna uthibitisho kuwa Yesu alifundisha kuwa kutoa fungu la kumi ni lazima. Unaungaunga mambo hili kuhalalisha hisia zako
 
Wapi atakutana na Mungu ampe hiyo 200k?
Mkuu yamkini hulijui neno la MUNGU kabisa... Pumzi unayopumua hua anakutania naww anaiweka puani mwako? Baraka anazowapa watu hua anakutania nao anawapa mikononi?
 
Mkuu yamkini hulijui neno la MUNGU kabisa... Pumzi unayopumua hua anakutania naww anaiweka puani mwako? Baraka anazowapa watu hua anakutania nao anawapa mikononi?
Mkuu jibu swali acha longolongo. Usilete vitisho jibu swali.
 
Hilo fungu la 10 labda liwe elf 10 tu. Hela ilivyo ngumu nikatoe laki 2 kizembe
 
Mkuu jibu swali acha longolongo. Usilete vitisho jibu swali.
Mbna mekujibu mkuu au unataka nijibu vpi? Ukiwapa watumishi wa MUNGU eg Mapadrii,wachungaji,manabii etc unakua umempa Bwana MUNGU...
 
Mnaosema fungu la kumi sio lazima upeleke kanisani mnampotosha mwenzenu, maelekezo ya bibilia kuhusu fungu la kumi ni kwa kuhani tu na sio vinginevyo, kulikuwa na maana Mungu kuamuru makuhani kupewa Hilo fungu la kumi, walitakiwa wagawe kwa walawi(watumishi wa madhabahuni) wagawe Kwa yatima na wageni wanaofika kanisani wanahudumiwa Kwa hilo fungu la kumi, fungu la kumi linatakiwa kuwa kamili sio kwa mafungu alivyosema mtoa mada. Kwa kuhutimitisha ndugu mtoa mada mpaka sasa haujatoa fungus la kumi kwa ukamilifu, na ili uweze kutoa kwa ukamilifu usitangulize mahitaji yako ambayo hayawezi kutoshelezwa Kwa huo mshahara, waza kwanza aliyekupa nguvu za kupata Hela.

Kingine usipende kuacha Hela zako kwa mtu usiyemjua Hela zako zaweza kukufunga
 
Asante Sana mkuu
 
Makuhani wengine Wana tofauti gani nahao watu wengine????... Makuhani wengine ni hatari kuliko walozi wakiikaribia Hela yako !!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado kuna watu wajinga kiasi cha kutoa zaka kwa dini kuendelea kuwaibia? Ndiyo maana matapeli wa kidini wamechipuka wengi ili wapate ulaji huu rahisi. Mungu ahitaji madafu yako maskini wewe unaibiwa
 
Hakuna MTU nilempangi matumizi, hapo Ni kuamua mwenyew utoe uwe na mahusiano mazuri na MUNGU wako au usitoe kwa hasara nafsi yako mwenyewe
Hakunaga Mungu anayetaka utoe zaka ndo akupende..hao ni wachungaji na mapadre ndo wanahizo pigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…