Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Mwisho wa siku mijadala kama hii arguments zake huwa ni philosophical.Suala la kuipa Turkey msaada ni suala la ubinadamu zaidi kuliko kuwanacho au kutokuwa nacho, ni suala la kuwekeza wema na kwenda zako huku pengine ukitaraji matunda yake hapo baadaye bila kutaraji, ni suala la kuonyesha huzuni na kuguswa na shida za watu, huwezi kwenda msibani mikono mitupu ni ama ujitoe kwa hali au mali nasi tumeweza kujitoa kwa mali-pesa hiyo "kidogo" $1M kulinganisha na nchi zingine, kumbuka dunia ni hii moja tunayoishi leo kwake kesho ni kwako basi kuwekeza hisani ni akiba msibani japo sio leo.
Naweza kuona mantiki ya hoja yako but $1 million dollar kwa Turkey aina impact kwenye kutatua changamoto zao na wao wenyewe wanao uwezo.
Si ajabu ata huyo balozi akaambiwa aiache hapo hapo itumike kwa shughuli za kuendeshea ubalozi tu.
Kwa upande wa watanzania huo msaada unazua maswali ya ‘conflicting duties’ (deontological ethics).
Kinachoangaliwa hapo kipi ni hatua sahihi given choices; mfano je ni haki serikali kuipatia $1 million uturuki kwa sasa ambayo tayari imefikisha $50 billion+ kwenye kukabiliana na maafa na serikali yao ina uwezo wa kumudu $82 billion estimated cost to rebuild.
Au? hela hiyo $1 million itumike ata kama kuwatua wamama 100 safari ya kilometer 10 kwenda na kurudi kufuata maji tu; ukizangatia anaetoa hiyo hela ni kiongozi wa hao maskini na yeye maisha yake sio ya shida kama watu anaowaongoza.
Ndio swala lilipo, it’s not rocket science logic kuona busara ni Tanzania kutoa ‘moral support’ ya maneno tu inatosha, kuliko mchango wa hela ambao auna impact wowote kwao na kwa kufanya ivyo ni kama dharau kwa shida za maskini tuliojaa Tanzania.