Mliokasirishwa kuhusu Rais Samia kutoa msaada Uturuki hii sio awamu ya Magufuli

Nani kasema Hana huhitaji? Kwani matajiri huwa hawapewi salamu za rambirambi? Au umewahi ona harusi ya tajiri watu hawatoi zawadi kisa ana pesa?

It's economic diplomacy maana Turkey ni business partner. Haya mambo kama ni sukuma gang huwezi elewa.
Point yangu ipo kwenye uhitaji ikiwa tutasema hizo hela tulizotoa ni msaada kwa Turkey, maana wenye kupinga hili suala mnawaona hawana ubinaadamu kwamba wanapinga kuwasaidia waliyopata majanga.

Sasa hayo ya zawadi ni tofauti.
 
are you serious? Tetemeko lote lile unasema hawana uhitaji wa msaada?
Wakati tunafikiria kuwapa hizo hela tuliona kuwa ndio msaada waliyokuwa wakiuhitaji? Au tumetoa tu ili tuonekane nasi tulichangia?
 
Wakati tunafikiria kuwapa hizo hela tuliona kuwa ndio msaada waliyokuwa wakiuhitaji? Au tumetoa tu ili tuonekane nasi tulichangia?

usd 1m ni fedha nyingi ,zitasaidia kwa namna moja au nyingine...Kiubinadamu siyo mpaka waombe ni kutoa mchango kama kushow concern.
 
Unakosoa maiti na kuwaacha waliyohai?
Wakati mnamkosoa JK kuwa nchi ilichezewa, tumecheleweshwa n.k hamkujua ni hakua madarakani kipindi mnamtukana awamu ya 5??

Sisi JPM tumemkosoa alivyokua madarakani kma tulivyomkosoa JK na Mkapa sasa how comes Leo tuonekane ndio tumelipwa sijui tunamchafua??

Sukuma gang mna tatizo
 
Point yangu ipo kwenye uhitaji ikiwa tutasema hizo hela tulizotoa ni msaada kwa Turkey, maana wenye kupinga hili suala mnawaona hawana ubinaadamu kwamba wanapinga kuwasaidia waliyopata majanga.

Sasa hayo ya zawadi ni tofauti.
Ndio zinauhitaji otherwise wasingezipokea.
 
Huyu mama ana mambo ya hovyo sana aisee. Hivi unagawa 2.5 billion pesa za walipa kodi ambao kwa wakati huu vijana tunahangaika mitaji ya biashara inasumbua yeye anagawa, aiseee ama kweli nimeamini mwafrika akili zake ziliumbwa ili atawaliwe.
 
Kwa sababu JPM si mtendaji tena matendo yake yamekoma hana analotenda tena, sasa ukisema unamkosoa haileti maana. Kinachobaki ni lawama ila wa kukosolewa ni Samia maana ndio mwenye kuweza kutekeleza hayo anayokosolewa.
 
Hizo ni zako wewe,nimemkataa shetani jumla.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Inajulikana shetani anashawishi maovu sasa ndio ututajie maovu gani umeacha kwa kumkataa shetani? Au hujui unachokiongea? Kwamba unasema umemkataa shetani halafu bado unaendelea na uzinzi wako uliyokubuhu?
 
Hata Samia akigawa pesa Kwa wananchi. ..bado atatukanwa Tu na wafuasi wa lile kundi ...

Hata akigawa vipande vya Dhahabu Kwa kila Mtanzania bado lile kundi litamtukana tu

Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
 
Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
Hawa watanzania wa humu mitandaoni ndio wako hivyo na hata hivyo serikali yenyewe haijui inachofanya.
 
Udini plus akuna jipya apo majanga km ayo utokea sana dunian na mengne tokea hapa hapa afrika ila sjawai ona tukitoa pesa why leo tunapeleka pesa Turkey

Waislamu na udini ni kawaida yao na wanaupenda sana udini
 
Ukiwa kwenye kundi la Walamba asali au ukiwa Mtoto wa Mama huwezi ona hoja ya wanaolalamika juu ya hili, hoja si kwamba kosa Serikali yetu kuisaidia Uturuki au Malawi katika majanga yaliyowakabili hoja ya msingi hata nchi yetu ina janga la mfumuko wa Bei hasa kwa bidhaa muhimu kama chakula hivyo ilitakiwa ifanyike jitihada kama hizo lakini kinachoonekana jitihada sasa ni kuwauzia Wananchi mahindi kwa bei ya kilogramu moja shilingi 780 hadi 850 kutegemeana na eneo.

Wapo Wananchi wa hali ya chini ambao hawawezi kumudu hiyo Bei kutokana na ugumu wa maisha uliopo, wewe kama bado unaishi kwa Wazazi, upo Chuo unapata mkopo au upo kwenye kundi la Walamba asali huwezi ona hoja kwa wanaohoji suala hilo, kuna Watu wanaishi maisha magumu nchi hii kuliko hata hao Waturuki waliopatwa na tetemeko la ardhi.

Kuna wakati tuwe tunaacha ushabiki na kusimamia ukweli, sidhani kama mtu anaona jitihada za Serikali katika kutatua changamoto zake za ndani atahoji juu ya kuisaidia Nchi nyingine, Nchi hii Ina changamoto lukuki na si kwamba zimeanza awamu hiii lakini Watu lazima wajadili kwani hata awamu nyingine zilizopita changamoto zilijadiliwa, hivyo ondoa mawazo kuwa kujadili changamoto ni kuichukia Serikali iliyopo.
 
Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
Unawajua Watanzania wote wewe? Ulishawahi kufanya utafiti juu ya hili unaloliamini?
 
Atumie mbinu gani kugundua kama thread hizo ni za Wapinzani na si Sukuma gang kama inavyoaminika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…