Mliokasirishwa kuhusu Rais Samia kutoa msaada Uturuki hii sio awamu ya Magufuli

Mliokasirishwa kuhusu Rais Samia kutoa msaada Uturuki hii sio awamu ya Magufuli

Nani kasema Hana huhitaji? Kwani matajiri huwa hawapewi salamu za rambirambi? Au umewahi ona harusi ya tajiri watu hawatoi zawadi kisa ana pesa?

It's economic diplomacy maana Turkey ni business partner. Haya mambo kama ni sukuma gang huwezi elewa.
Point yangu ipo kwenye uhitaji ikiwa tutasema hizo hela tulizotoa ni msaada kwa Turkey, maana wenye kupinga hili suala mnawaona hawana ubinaadamu kwamba wanapinga kuwasaidia waliyopata majanga.

Sasa hayo ya zawadi ni tofauti.
 
are you serious? Tetemeko lote lile unasema hawana uhitaji wa msaada?
Wakati tunafikiria kuwapa hizo hela tuliona kuwa ndio msaada waliyokuwa wakiuhitaji? Au tumetoa tu ili tuonekane nasi tulichangia?
 
Wakati tunafikiria kuwapa hizo hela tuliona kuwa ndio msaada waliyokuwa wakiuhitaji? Au tumetoa tu ili tuonekane nasi tulichangia?

usd 1m ni fedha nyingi ,zitasaidia kwa namna moja au nyingine...Kiubinadamu siyo mpaka waombe ni kutoa mchango kama kushow concern.
 
Unakosoa maiti na kuwaacha waliyohai?
Wakati mnamkosoa JK kuwa nchi ilichezewa, tumecheleweshwa n.k hamkujua ni hakua madarakani kipindi mnamtukana awamu ya 5??

Sisi JPM tumemkosoa alivyokua madarakani kma tulivyomkosoa JK na Mkapa sasa how comes Leo tuonekane ndio tumelipwa sijui tunamchafua??

Sukuma gang mna tatizo
 
Point yangu ipo kwenye uhitaji ikiwa tutasema hizo hela tulizotoa ni msaada kwa Turkey, maana wenye kupinga hili suala mnawaona hawana ubinaadamu kwamba wanapinga kuwasaidia waliyopata majanga.

Sasa hayo ya zawadi ni tofauti.
Ndio zinauhitaji otherwise wasingezipokea.
 
Huyu mama ana mambo ya hovyo sana aisee. Hivi unagawa 2.5 billion pesa za walipa kodi ambao kwa wakati huu vijana tunahangaika mitaji ya biashara inasumbua yeye anagawa, aiseee ama kweli nimeamini mwafrika akili zake ziliumbwa ili atawaliwe.
 
Wakati mnamkosoa JK kuwa nchi ilichezewa, tumecheleweshwa n.k hamkujua ni hakua madarakani kipindi mnamtukana awamu ya 5??

Sisi JPM tumemkosoa alivyokua madarakani kma tulivyomkosoa JK na Mkapa sasa how comes Leo tuonekane ndio tumelipwa sijui tunamchafua??

Sukuma gang mna tatizo
Kwa sababu JPM si mtendaji tena matendo yake yamekoma hana analotenda tena, sasa ukisema unamkosoa haileti maana. Kinachobaki ni lawama ila wa kukosolewa ni Samia maana ndio mwenye kuweza kutekeleza hayo anayokosolewa.
 
Hata Samia akigawa pesa Kwa wananchi. ..bado atatukanwa Tu na wafuasi wa lile kundi ...

Hata akigawa vipande vya Dhahabu Kwa kila Mtanzania bado lile kundi litamtukana tu

Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
 
Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
Hawa watanzania wa humu mitandaoni ndio wako hivyo na hata hivyo serikali yenyewe haijui inachofanya.
 
Udini plus akuna jipya apo majanga km ayo utokea sana dunian na mengne tokea hapa hapa afrika ila sjawai ona tukitoa pesa why leo tunapeleka pesa Turkey

Waislamu na udini ni kawaida yao na wanaupenda sana udini
 
Kuna watu wana makasiriko hadi mambo kama haya!! Sasa kuna ubaya gani kwa nchi kusaidia wahanga wa tetemeko? Hivi tumekuwa wabinafsi kiasi gani? Tunasahau kuwa majanga ya asili hayana mwenyewe na hayazuiliki kirahisi.

Tunasahau kuwa leo kwao kesho kwetu, tusipojitoa kwa kidogo chetu siku yatatukumba ni nani atatukimbilia? Famasiala nini? Usiombe yakukute.

Mtu analeta hoja za kijinga eti tunatoa msaada wakati vitu vimepanda bei, hizo bilioni 2.3 ndo zinawahenyesha na kuwatoa watu mapovu hivi? Bilioni 2.3 zinaweza vipi kupunguza bei ya unga au vitu kupanda kama sio roho mbaya tu?

Tumezoea kupewapewa tu, na sisi siku moja tukijitoa sio mbaya!! Tatizo bongo wengi hawajui diplomasia ya kiuchumi, Samia sio hayati mwendazake yule ambaye hela za tetemeko rambirambi alikula yeye na genge lake bila aibu. Alikuwa rais wa hovyo sana na hakuwa na hata na chembe ya aibu usoni na moyoni mwake.
Tujikumbushe [emoji1313][emoji1313][emoji1313]: "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kufanya jitihada za kujijengea nyumba zao wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali. Mkuu wa Mkoa amedai kuwa jumla ya fedha zilizochangwa ni zaidi ya Bilioni 5.4 na kusema kuwa zimeelekezwa katika kukarabati miundombinu ya taasisi za Serikali na kuwataka wananchi wanaosubiri msaada wa serikali kusubiri mchango itakayotolewa na wadau walioahidi kuwasaidia waathirika moja kwa moja."

Uturuki wametusaidia mangapi nchi yetu tokea uhuru? Yaani tatizo ni hiko kibilioni 2.5 ndo tunang'aka kiasi hiki angetoa bilioni 100 jee??

Kuna watu hawafurahii utawala na mageuzi aliyoyafanya Rais Samia hususan maridhiano na kurudisha maridhiano na demokrasia iliyokuwa imeporwa na dikteta katili wa awamu ya tano. Hawa Sukumagang ndio wanaopinga kila kitu. Mimi naona kama wamenunishwa na maridhiano kati ya Chadema na Mama, basi wahame nchi.
Ukiwa kwenye kundi la Walamba asali au ukiwa Mtoto wa Mama huwezi ona hoja ya wanaolalamika juu ya hili, hoja si kwamba kosa Serikali yetu kuisaidia Uturuki au Malawi katika majanga yaliyowakabili hoja ya msingi hata nchi yetu ina janga la mfumuko wa Bei hasa kwa bidhaa muhimu kama chakula hivyo ilitakiwa ifanyike jitihada kama hizo lakini kinachoonekana jitihada sasa ni kuwauzia Wananchi mahindi kwa bei ya kilogramu moja shilingi 780 hadi 850 kutegemeana na eneo.

Wapo Wananchi wa hali ya chini ambao hawawezi kumudu hiyo Bei kutokana na ugumu wa maisha uliopo, wewe kama bado unaishi kwa Wazazi, upo Chuo unapata mkopo au upo kwenye kundi la Walamba asali huwezi ona hoja kwa wanaohoji suala hilo, kuna Watu wanaishi maisha magumu nchi hii kuliko hata hao Waturuki waliopatwa na tetemeko la ardhi.

Kuna wakati tuwe tunaacha ushabiki na kusimamia ukweli, sidhani kama mtu anaona jitihada za Serikali katika kutatua changamoto zake za ndani atahoji juu ya kuisaidia Nchi nyingine, Nchi hii Ina changamoto lukuki na si kwamba zimeanza awamu hiii lakini Watu lazima wajadili kwani hata awamu nyingine zilizopita changamoto zilijadiliwa, hivyo ondoa mawazo kuwa kujadili changamoto ni kuichukia Serikali iliyopo.
 
Sometimes naona viongozi wapo right. Ukifanya kazi huku unasikiliza kelele za watanzania unapoteza nguvu zako bure. Watanzania ni lile kundi ambalo hawajui wanataka nini
Unawajua Watanzania wote wewe? Ulishawahi kufanya utafiti juu ya hili unaloliamini?
 
Basi itakua ulikua sukuma gang maana majority ya waTanzania wanajua Chadema ni chama Cha upinzani and obviously watapinga sera mbovu za CCM.

Wanaitwa hivyo sababu ukisoma post zao humu walikua wanamsifia sana JPM akiwa Rais mfano takwimu za TRA, ujenzi wa miradi n.k ila mambo hayo hayo yakifanywa na Samia utasikia takwimu za uongo, mara sijui miradi unapigwa Hela hata kama umemalizika!! Hiyo double standard Yao ndio imetufanya tuseme wanapinga Kila kitu.

Sio kweli, tatizo wapinzani wakikosoa utawala wa JPM haraka haraka mnasema wamelamba asali as if mmeambiwa yeyote anayemchukia JPM basi anampenda Samia!! What the hell?? Msifungamanishe haya mambo otherwise tafuta thread zote zinazoongelea mikopo, bando, gharama za maisha, na teuzi uniambie wapi Kuna mpinzani kamsifia Mama Samia ukipata hata moja najiondoa JF.
Atumie mbinu gani kugundua kama thread hizo ni za Wapinzani na si Sukuma gang kama inavyoaminika?
 
Back
Top Bottom