Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni mazoea ndo tatizo ...sijazoea kabisa vyakula vyao kwa kweli..Hakuna chakula cha ajabu hata kimoja hapo,tatizo ni kwamba wewe unataka vyakula vizuri kwa muonekano
1.Makande hayo ndio yana virutubisho kwa sababu hayo mahindi unayosema magumu hayajakobolewa yana kile kiini
2.Wali na samaki ambaye hajaungwa ni kwamba hapo hupati cholesterol inayotokana na mafuta ya kuungia
3.Maziwa mgando yana nutrients kibao
Nashagaa unataka makande ya mahindi yaliyokobolewa halafu yawekwe sukari,hivi utaacha kuugua kisukari na presha kweli
Jifunze kuhusu vyakula aisee,hayo maandazi unayoyasifia yamepikiwa ngano iliyokobolewa na yakawekwa sukari yakapitishwa kwenye mafuta ni sumu tu,faida yake mwilini ni ndogo mno
Cha ajabu ukiwapikia misosi ya town wanafurahi kinomaMpaka leo hii mimi sio mtu wa kuumwa umwa na shukrani zote ni kwa MUNGU kwanza kisha ni hivyo vyakula duni vya kijijini unavyosema.
Vile ndio vyakula sasa sio hivi processed foods vinaleta kansa tu kila kitu makemikali ya viwandani.
Japo kijijini nilikuwa naenda likizo tu kwa bibi ila naweza sema faida nyingi mno kiafya na hata vile nachukulia maisha kiujumla.
Duhhh ...balaaaKuna mkoa siutaji niliendavkikazi huko kwenye kata fulani nikaagiza wali nyama nilishindwa kula,nyama imeungwa kwa mafuta mengi sana,shombo tupu,na ni migahawa yote,niliishia kula wali maharage wiki nzima
Chakula ndo tafsiri ya ustaarabu,bara hakuna wanachojua kuhusu chakula zaid ya kuchemsha na maana tunasema hakuna ustaarabu!Nilienda usukumani. Picha linaanza wamechinja mbuzi hawaweki vitunguu swaumu kukata shimbi wala ndimi nkawaambia naombeni nipike mchuzi walibloo wenyewe wakashangaa eti htujui km kitunguu swaumu kinakata shombo, Wana karanga ila kande hawaweki karanga nikawawekea siku hyoo weee walikula balaa, kupika mi ndo nilikabidhiwa jiko,asubuhi chapati za mafutazsiku moja nkapika tambi kulikua na mgonjwa bwana wee waliinjoi mgonjwa alikula mpk akatamani tena.
Inshort mapishi Yako pwani bwanaaa tunajua hasaaa,nilikua napika wali Nazi plus ndondo wanakula hawabakishi hapo mi kwetu ndo sijui kupika sasa, nikawa nasema kimoyo wangekua wanakula vya wadogo zangu Hawa [emoji1][emoji1][emoji1]wangepagawa ila mlenda, mtindi na ugali vilinishinda aseehh.
Kwani ustaarabu n kula tu?Chakula ndo tafsiri ya ustaarabu,bara hakuna wanachojua kuhusu chakula zaid ya kuchemsha na maana tunasema hakuna ustaarabu!
Ni kudra za mwenyezi Mungu tu kuwa bado mnaishi. Niko kijiji fulani sitataja mkoa. Niko na wenyeji wangu.
Asubuhi uji hauna sukari, mchana tumekula michembe. Usiku udaga na dagaa kama saba hivi kwenye bakuli.
Maisha haya magumu sana kijijini. Tuwaombee
Huwa wanaishi maisha marefu yenye nguvu kweli nafikiri sababu ya food style, pia huwezi kuta wananenepeana, unakuta kizee cha kipare kiko 75 ila kina nguvu kweli na shamba kinaenda.
Hivi vyakula vinavyofurahisha kinywa nadhani si rafiki kwa mwili maana vijana wa mjini kuna vitambi fulani huotaga mtu anaonekana mzembe kweli. Waangalie kwenye majukwaa ya mipira utawaona.
Hakuna chakula cha ajabu hata kimoja hapo,tatizo ni kwamba wewe unataka vyakula vizuri kwa muonekano
1.Makande hayo ndio yana virutubisho kwa sababu hayo mahindi unayosema magumu hayajakobolewa yana kile kiini
2.Wali na samaki ambaye hajaungwa ni kwamba hapo hupati cholesterol inayotokana na mafuta ya kuungia
3.Maziwa mgando yana nutrients kibao
Nashagaa unataka makande ya mahindi yaliyokobolewa halafu yawekwe sukari,hivi utaacha kuugua kisukari na presha kweli
Jifunze kuhusu vyakula aisee,hayo maandazi unayoyasifia yamepikiwa ngano iliyokobolewa na yakawekwa sukari yakapitishwa kwenye mafuta ni sumu tu,faida yake mwilini ni ndogo mno
We sema upo usukumani mkuu
Natural food hovyo..!!! Mjini kuna junk food za kutosha na ndo unazotambiaNi kudra za mwenyezi Mungu tu kuwa bado mnaishi. Niko kijiji fulani sitataja mkoa. Niko na wenyeji wangu.
Asubuhi uji hauna sukari, mchana tumekula michembe. Usiku udaga na dagaa kama saba hivi kwenye bakuli.
Maisha haya magumu sana kijijini. Tuwaombee
Hawana option kuna njaa,nao wanatamani kula madikodiko,pili hawajui kupikaNatural food hovyo..!!! Mjini kuna junk food za kutosha na ndo unazotambia
Alaa, kumbe ni issue ya ukame na siyo kawaida tu ya kila siku?!!!!!!!Ukame huu tango unalipata wapi, yaani kuna mikoa kama Morogoro, Mbeya na Kagera ina nafuu ila kuna mikoa ukame umewatandika wanakula wasife
Kama hapakuwa na mboga walikuwa sahihiTulienda kwa bibi aunt akapika wali na pilau wandava wakawa wanachukua pilau wanaweka juu ya wali kama mboga kudadeki kucheka nashindwa najikausha tu.
Mijini wanategemea chakula kitoke vijijini wanunue.Vijijini ndio kuna kiwango kikubwa cha utapiamlo kuliko mjini. Mijini watu wengi wanakula mlo bora zaidi kuliko vijijini.
Hata wakiwa navyo kupika ni shidaMijini wanategemea chakula kitoke vijijini wanunue.
Katika vijiji vyenye njaa ni kweli ulichosema. Ila vijiji vyenye neema ya mvua si kweli.