Mliokulia kijijini poleni sana, mnakula vyakula duni sana

Ni mazoea ndo tatizo ...sijazoea kabisa vyakula vyao kwa kweli..
 
Kuna uhaba wa msosi na kutojua kupika.
Na kweli mikoa mingine msosi kwao ni janga kinoma, uko hata kama unajua kupika ni sawa na bure maana misosi hamna.
Kwamfano mkoa wa mbeya misosi ipo kibao ila wanyakyusa na mapishi ni mbingu na ardhi, wengi hawajui kupika.
Hata ukifika mbeya town ukila kwenye migahawa yao msosi wao sio mzuri kama migawa ya dsm japo vinavyopatika dsm na mbeya pia vinapatikana kwa wingi tu.

Nazi na vikolokolo vyote vipo ila ndo ivo watu wa mbeya kupika wengi hawajui.
 
Mpaka leo hii mimi sio mtu wa kuumwa umwa na shukrani zote ni kwa MUNGU kwanza kisha ni hivyo vyakula duni vya kijijini unavyosema.
Vile ndio vyakula sasa sio hivi processed foods vinaleta kansa tu kila kitu makemikali ya viwandani.

Japo kijijini nilikuwa naenda likizo tu kwa bibi ila naweza sema faida nyingi mno kiafya na hata vile nachukulia maisha kiujumla.
 
Cha ajabu ukiwapikia misosi ya town wanafurahi kinoma
 
Kuna mkoa siutaji niliendavkikazi huko kwenye kata fulani nikaagiza wali nyama nilishindwa kula,nyama imeungwa kwa mafuta mengi sana,shombo tupu,na ni migahawa yote,niliishia kula wali maharage wiki nzima
Duhhh ...balaaa
 
Chakula ndo tafsiri ya ustaarabu,bara hakuna wanachojua kuhusu chakula zaid ya kuchemsha na maana tunasema hakuna ustaarabu!
 
Watu wengi wenye utapiamlo wanapatikana vijijini zaidi. Vijijini mara nyingi huwa wanakula vile wanavyozalisha zaidi bila kuzingatia mlo bora.
 
Vijijini ndio kuna kiwango kikubwa cha utapiamlo kuliko mjini. Mijini watu wengi wanakula mlo bora zaidi kuliko vijijini.
 
Anahitaji elimu ya mlo bora.
 
Natural food hovyo..!!! Mjini kuna junk food za kutosha na ndo unazotambia
 
Ukame huu tango unalipata wapi, yaani kuna mikoa kama Morogoro, Mbeya na Kagera ina nafuu ila kuna mikoa ukame umewatandika wanakula wasife
Alaa, kumbe ni issue ya ukame na siyo kawaida tu ya kila siku?!!!!!!!
 
Tulienda kwa bibi aunt akapika wali na pilau wandava wakawa wanachukua pilau wanaweka juu ya wali kama mboga kudadeki kucheka nashindwa najikausha tu.
Kama hapakuwa na mboga walikuwa sahihi
 
Vijijini ndio kuna kiwango kikubwa cha utapiamlo kuliko mjini. Mijini watu wengi wanakula mlo bora zaidi kuliko vijijini.
Mijini wanategemea chakula kitoke vijijini wanunue.
Katika vijiji vyenye njaa ni kweli ulichosema. Ila vijiji vyenye neema ya mvua si kweli.
 
Nilishaonaga hiyo hali vijiji vingi nilivyowahi kufika lakini kilichonishangaza zaidi ni kwamba unakuta familia inakula ivo lakini baba ana ng'ombe zaidi ya 30 na mbuzi zaidi ya 50.

Unakuta ana uwezo wa kuuza ng'ombe wawili tu na kufungua biashara ambayo itaingiza kipato cha kuwahakikishia chakula kizuri kwa familia lakini kwao kuwaambia habari za kuuza ng"ombe hawakuelewi kabisa. Wanakwambia hawa ndo wanalinda familia. Umasikini upo akilini!!!!!!

Nilishuhudia mzee mmoja ameumwa mpaka akafariki lakini aligoma kabisa kuuza ngombe ili ipatikane hela akafanyiwe matibabu hospitali.
 
Mijini wanategemea chakula kitoke vijijini wanunue.
Katika vijiji vyenye njaa ni kweli ulichosema. Ila vijiji vyenye neema ya mvua si kweli.
Hata wakiwa navyo kupika ni shida
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…