Mliokulia kijijini poleni sana, mnakula vyakula duni sana

Mliokulia kijijini poleni sana, mnakula vyakula duni sana

Pwani ya wapi mbona Zanzibar hawajui kupika mboga.

Kwanza wanawake wa kiislamu asilimia kubwa ni wapishi wazuri hata awe kijijini, lakini pia watu wanaoishi mwambao mwa bahari au ziwa bila kujali itikadi yao hawa wanafahamu mapishi sana, aibu utaipata bara labda kwa watu wachache tu niliwahi kunywa chai kibondo wamechemsha maji tu, wakaweka majani na sukari imeisha hiyo wakati nishazoea chai ina mdalasini, hiriki na tangawizi kwa mbali au wali unakua na harufu safi sana inabidi wanawake wajifunze mapishi ya aina tofautitofauti
 
Huwa wanaishi maisha marefu yenye nguvu kweli nafikiri sababu ya food style, pia huwezi kuta wananenepeana, unakuta kizee cha kipare kiko 75 ila kina nguvu kweli na shamba kinaenda.

Hivi vyakula vinavyofurahisha kinywa nadhani si rafiki kwa mwili maana vijana wa mjini kuna vitambi fulani huotaga mtu anaonekana mzembe kweli. Waangalie kwenye majukwaa ya mipira utawaona.
Vijana wa vijiji hawana vitambi kwasababu ya aina ya vyakula wanavyo kula.
 
Kwanza wanawake wa kiislamu asilimia kubwa ni wapishi wazuri hata awe kijijini, lakini pia watu wanaoishi mwambao mwa bahari au ziwa bila kujali itikadi yao hawa wanafahamu mapishi sana, aibu utaipata bara labda kwa watu wachache tu niliwahi kunywa chai kibondo wamechemsha maji tu, wakaweka majani na sukari imeisha hiyo wakati nishazoea chai ina mdalasini, hiriki na tangawizi kwa mbali au wali unakua na harufu safi sana inabidi wanawake wajifunze mapishi ya aina tofautitofauti
Hiyo huku nilipo,nikienda kwa jirani wananiambia kabisa karibu chai lkn haina viungo kama ulivyozoea,

Chai ya hivyo siiwezi aisee,

Chai
hIliki
Karafuu
Mdalasini
Tangawizi au pilipili manga,
Mchaichai
ChaI inakuwa tamu haiishi hamu[emoji8]
 
Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, Mbeya na Dodoma zina sehemu kubwa ya maeneo ambayo ni mjini.
Boss, Embu niambie, kwenye hii miji uliyotaja mjini ni wapi na km ngapi? Maana hii ni nchi yetu sote na tunaijua kutokana na shughuli zetu tunazifanyia humu.

Arusha ina km kama 37 elfu ikiwa na maeneo haya
Arusha district
Arusha city council
Karatu
Ngorongoro
Longindo
Monduli

Mwanza kama km elf 25 ikiwa na maeneo haya
Ilemela
Magu
Kwimba
Misungwi
Nyamagana
Sengerema
Ukerewe

Dodoma km elf 41 kama sio 42
Maeneo
Dodoma
Bahi
Chamwino
Kongwa
Mpwapa
Chemba
Kondoa
 
Hawana option kuna njaa,nao wanatamani kula madikodiko,pili hawajui kupika
Huyo aliyeenda huko na kuibuka na uzi huu unadhani anajua kupika? Kama anajua kwanini asiwapikie? Diko diko hata la dagaa lipo.
 
Nilienda usukumani. Picha linaanza wamechinja mbuzi hawaweki vitunguu swaumu kukata shimbi wala ndimi nkawaambia naombeni nipike mchuzi walibloo wenyewe wakashangaa eti htujui km kitunguu swaumu kinakata shombo, Wana karanga ila kande hawaweki karanga nikawawekea siku hyoo weee walikula balaa, kupika mi ndo nilikabidhiwa jiko,asubuhi chapati za mafutazsiku moja nkapika tambi kulikua na mgonjwa bwana wee waliinjoi mgonjwa alikula mpk akatamani tena.

Inshort mapishi Yako pwani bwanaaa tunajua hasaaa,nilikua napika wali Nazi plus ndondo wanakula hawabakishi hapo mi kwetu ndo sijui kupika sasa, nikawa nasema kimoyo wangekua wanakula vya wadogo zangu Hawa [emoji1][emoji1][emoji1]wangepagawa ila mlenda, mtindi na ugali vilinishinda aseehh.
Naam ulimi unafurahia lakini mwili unakulaumu unasema huyu jamaa huku kuunga unga kwa nini...., Wakati michemsho au sometimes kwa mboga partial cooked inatosha kupata nutrients.... Ngoja tumkomoe kwa vijimagonjwa
 
Nimekanyaga mikoa yote ya nchi hii.
Ukiona chakula kitamu Sana huko bara basi fuatilia Routes zote za mpishi WA chakula hicho lazima awe amewahi kufika Pwani au amewahi kuishi na watu walioishi Pwani
Nimekanyaga mikoa yote ya nchi hii.
Ukiona chakula kitamu Sana huko bara basi fuatilia Routes zote za mpishi WA chakula hicho lazima awe amewahi kufika Pwani au amewahi kuishi na watu walioishi Pwani
Uko sahihi,kuna mkoa nilikula ile chapati yenye kurasa nikauliza mpishi nikaonyeshwa kijana toka zanzibar
 
Vijana wa vijiji hawana vitambi kwasababu ya aina ya vyakula wanavyo kula.
Utaotaje kitambi huku umeshinda shambani unalima hekari nzima peke yako,ukirudi unakutana na michembe
 
Ni kudra za mwenyezi Mungu tu kuwa bado mnaishi. Niko kijiji fulani sitataja mkoa. Niko na wenyeji wangu.

Asubuhi uji hauna sukari, mchana tumekula michembe. Usiku udaga na dagaa kama saba hivi kwenye bakuli.

Maisha haya magumu sana kijijini. Tuwaombee
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji119]
 
Mimi nikiwa vijijini kuepuka disappointments za vyakula huwa natafuta tu kitimoto, kumradhi wadau 😀

Vyakula vingi vya vijijini ni vibayaaa labda upate supu ya kuku wa kienyeji basi.
 
Boss, Embu niambie, kwenye hii miji uliyotaja mjini ni wapi na km ngapi? Maana hii ni nchi yetu sote na tunaijua kutokana na shughuli zetu tunazifanyia humu.

Arusha ina km kama 37 elfu ikiwa na maeneo haya
Arusha district
Arusha city council
Karatu
Ngorongoro
Longindo
Monduli

Mwanza kama km elf 25 ikiwa na maeneo haya
Ilemela
Magu
Kwimba
Misungwi
Nyamagana
Sengerema
Ukerewe

Dodoma km elf 41 kama sio 42
Maeneo
Dodoma
Bahi
Chamwino
Kongwa
Mpwapa
Chemba
Kondoa
Ni Dsm pekee ambayo unaweza enda km 30 kila upande na bado pamechangamka

Majiji mengine yote ukivuka km 10 tu kila upande hakuna kitu.

Mwanza ukivuka Igoma tu hakuna kitu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, Mbeya na Dodoma zina sehemu kubwa ya maeneo ambayo ni mjini.
Tembea uone

Mwanza ukivuka Igoma kuna nini?

Arusha km 10 toka mjini kuna nini?

Mbeya ndo usiseme kabisa

Dodoma iondoe kabisa
 
Ni Dsm pekee ambayo unaweza enda km 30 kila upande na bado pamechangamka

Majiji mengine yote ukivuka km 10 tu kila upande hakuna kitu.

Mwanza ukivuka Igoma tu hakuna kitu
Ukivuka igoma tu unautafuta kisesa,hivi kisesa ni mwanza au simiyu
 
Back
Top Bottom