Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

Wap
Unatetea ujinga, kwa nini Mwanamke alificha kua ana Mtoto!!? Kesho akipata Mwanaume mwenye pesa na akampenda,atamficha hadi Mume wake na Watoto! Wanawake mnafanyaga ujinga wenu alafu bado mnataka kuonewa huruma!!!
Wapuuzi
 
Kama hakukuta Bikra hapo, sioni tatizo la Mwanamke.
Kama hakuulizwa pia sioni tatizo la Mwanamke.
Kama Mwanaume hakuamua kufuata utaratibu akaamua aishi na mtoto wa mtu kiholela, sio tatizo Kwa mwanamke.

Mwanaume mzima unashindwaje kujua mwanamke aliyejifungua? Kama umeshindwa Kwa kumuangalia tuu haya hata wakati unafanya naye sex ukashindwa kujua?

Mwanaume ndio mwenye shida.
Asimuache!
Japo bado jukumu lakusema ukweli lilikuwa la mwanamke
 
Duh,si ajabu alivyokuwa anakwendaga kivyake likizo kwao babati huyo mwanamke alikuwa anakwenda kumpelekea mbunye mzazi mwenzake wa mwanzo,ndio maana jamaa anapagawa sana
Inawezekana kbs
 
Sitetei naongea ukweli.Sio kila singles mother ni mbaya,na kuwa single mother sio dhambi.Na Kwa Hilo tukio sioni ubaya aloufanya huyo dada.Mtoa mada alipaswa kusema wanaume ulizeni historical background ya wenzi wenu.Labda bibie hakuulizwa chochote angewezaje kukurupuka eti nna mtoto ili iweje?
Daaaaaah! hivi Kuna mahusiano ya miaka9 yatakosa taarifa muhimu Kama hii kweli? Yaani hata Ingetokea hilo swali halikuulizwa(japo ningumu),huyo dada angeshindwa kueleza kitu muhimu Kama hicho?
Na inamaana wakiwa wote yule mwanamke alikuwa anajihesabu anawatoto wawili wale alozaa na jamaa. Mahusiano yangekuwa ya wiki au mwezi tungemtetea huyo mwanamke Ila sio miaka yote hiyo.
 
Inauma sana mda wote unajiapiza hutokaa kuoa au kuzaa na single mom

Unakuja Kutana na binti mzuri anakwambia hana mtoto unasema yes hapa nimepata halafu kumbe baadaye unagundua ni single Maza
Kwa sisi wanaume uongo kama huo sidhani kama jamaa atakuja kuwa naye sawa ile 100%
Hili nalo muende mkalitizame.... 😂😂😂
 
Mbona huyo jamaa ni mpumbavu aisee,,hilo jambo ndo la kukasirisha?
 
Nawasalimu nyote

Rafiki yangu yupo kikazi Dodoma tangu mwaka2013.

Mwaka huo aliripoti kazi na dada mmoja mwenyeji wa Babati.Jamaa kwao ni Tanga. Hapa na pale baada ya miezi kadhaa wawili hawa wakajikuta niwapenzi.

Mapenzi yalivyokolea wakaamua waoane kimjini mjini.Yaani waliishi pamoja bila kwenda kujitambulisha kwa wazazi japo kwa njia ya simu waliwapa taarifa.

Likizo zote walikuwa wanabaki huko Dodoma na pale ilipobidi kwenda nyumbani kila mmoja alienda kwao.
Mwaka2015 wakafanikiwa kupata mtoto wao wakwanza.Hapo Sasa wazazi wa upande wakiume wakalazimisha jamaa ampeleke mtoto nyumban.Kwa kuwa mtoto hawezi kwenda mwenyewe ikawa ndo nafasi Sasa ya jamaa kwenda namkewe.Wazazi wakafurahi kuona mjukuu na mkwe wao.

Miaka mingine ilofuata kila mmoja alikuwa anaenda kwao wakati wa likizo na wasipoenda walikuwa wanabaki wote Dodoma. Mwaka huu jamaa wamebahatika kupata mtoto wao wapili.Upande wa mwanamke nao wakakomaa kuwa wanataka kuona wajukuu pamoja na baba yao.Jamaa akaamua atumie likizo yake hii kwenda ukweni Babati.

Wamefika ukweni wamepokelewa vizuri bila shida yoyote.Baada ya muda anakuja binti wa Kama miaka13 hivi.Amefurahi kweli kuwaona pale lakini zaidi anamchangamkia mke wa jamaa. Baada ya shamrashamra mama mkwe anatoka huko jikoni na kumwambia Yule binti"umefurahi kuwaona wadogo zakoee, nahuyo ndo baba yenu msalimie vizuri".

Nifupishe tu hii stori kwa kusema yule mke wajamaa alikuwa na mtoto aliyemzalia nyumbani kabla hajaenda kikazi Dodoma.Kuzalia nyumbani sio shida,tatizo nikwamba kwa miaka yote aliyokaa na jamaa hakuwahi kumwambia kuhusu yeye kuwa na mtoto nyumbani.Mtoto(binti)yupo darasa la saba mwaka huu.

Usiku badala yakuwa muda wa kubwaga moyo jamaa wakaamua wautumie kwa mazungumzo ya kilichotokea.
Mke wajamaa alikiri kuwa kweli binti ni wakwake Ila alishindwa kumweka wazi jamaa kwa sababu ambazo kimsingi hazikuwa na mashiko.

Jamaa alipanga akae siku mbili tatu ukweni ila amekatisha ziara na karudi Dodoma.Amechanganyikiwa,ameshindwa kukisanua pale ukweni hvyo ametulia akifikiri nini Cha kufanya.

Nimemtuliza jamaa kwani hasira alizokuwanazo siwezi shangaa nikiambiwa kaua na kujiua.Ubaya tu nikwamba pamoja na mkasa huo mzito akifanya mauji polisi watasema chanzo Cha mauaji ni WIVU WA MAPENZI.
Mke bado yupo Babati kwani walikubaliana tangu mwanzo kuwa jamaa angewaacha huko walau wiki mbili.

Wakuu,hili nalo linapitaje kwa huyu rafiki yangu

Ushauri wangu; Kama umekutana naye mjini mkapendana,fanya hima uende kwao...Kuna mengine yamuhimu utayagundua ukifika.

Wasalaam!
Hata Kama ana mtoto mkubwa kwa vile hakumuhusisha tangu mwanzo naye atulie walee watoto wa, hizo hasira ni za hovyo maana tayari wana watoto au baada ya kumuona binti ndio kahisi mzazi mwenzie ni mzee? Waendelee kupendana na kupanga mipango yao ya baadae vizuri tu sioni tatizo hapo ila akae akijua mwenza wake ni msiri sana anaweza kufanya chochote peke yake bila kuhumusisha hasa kwa maendeleo ya binti yake mkubwa

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Mwambie apige chini iyo mama ..chukua watoto is mwingine maisha Ni mafupi maumivu hayana maana.
 
Jamaa yangu mmoja alikutana na binti wakaamua kuishi naye wote wapo Dar bint wa Manzese na wao waliishi Magomeni. Wakienda kusalimia wanaona vitoto vinakuja mama mama mara baba baba jamaa anajua NI watoto wa ndugu na tayari wana mtoto mmoja.

Ikatokea binti kafiwa na mama kakaa msibani baada ya arubani na jamaa alikuwepo kwenye kikao Cha familia kaka mkubwa akasema Sasa mama kafa kila mtu abebe mwanae nyumba tupangishe itusaidie [emoji3][emoji3][emoji3] jamaa anashangaa mwenza anawaambie X na Y kachungukueni nguo zenu tuondoke, jamaa hakuongea kitu wala hakumuiliza hata siku moja ila hawakudumu maana bint ni kama hakujielewa akaanza tabia za ajabu wakatimuana.

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Amekosea kuondoka bila kuonyeshwa kaburi la baba wa huyo mtoto. Huenda hizo likizo anapoendaga kwao jamaa linapasha kiporo kwa mzazi mwenza. Zaidi sina la kushauri. Mambo yao nawaachia wenyewe.

Ewe bachela mwenzangu. KATAA KUOA SINGLE MOTHER, hao ni kwa ajili ya kupiga na kusepa!
 
Kuna mzee alinihimiza sana kama nataka kuoa basi nijitahidi kumfahamu vizuri binti na familia yake kwa ujumla.

Ongea na majirani wawili watatu kuijua familia yao na yeye pia.

Hizi mambo za kuchukuana tu, utakosa wa kumlilia..
 
Kama hakukuta Bikra hapo, sioni tatizo la Mwanamke.
Kama hakuulizwa pia sioni tatizo la Mwanamke.
Kama Mwanaume hakuamua kufuata utaratibu akaamua aishi na mtoto wa mtu kiholela, sio tatizo Kwa mwanamke.

Mwanaume mzima unashindwaje kujua mwanamke aliyejifungua? Kama umeshindwa Kwa kumuangalia tuu haya hata wakati unafanya naye sex ukashindwa kujua?

Mwanaume ndio mwenye shida.
Asimuache!
Alipigwa upofu wa mapenz
Ukizingatia wanawake wa huko manyara ni white basiii jamaa akaona amepatia ngoja amuwahi yeye kumbe wahuni walishapita siku nyingi na kuacha alama

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alipigwa upofu wa mapenz
Ukizingatia wanawake wa huko manyara ni white basiii jamaa akaona amepatia ngoja amuwahi yeye kumbe wahuni walishapita siku nyingi na kuacha alama

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

😀😀😀

Kama wanaelewana na Mke ana adabu Mimi nashauri waendelee tuu.

Uongo unasababu nyingi moja wapo ni hiyo ya huyo demu
 
Ni vizuri kujua taratibu za ukweni zikoje kabla hujaoa! Huko babati mbona bi kawaida Binti kabla hajaolewa huzaa kwanza na huyo mtoto anakuwa Mali ya familia yake!! Jamaa kama anampenda huyo single mom basi aendelee nae maana hakuna namna ! Mwanamke kakosea kutokua wazi ila pia mume nae kayumba kutokufanya utafiti na kumjua vizuri mpenzi wake
 
Daaaaaah! hivi Kuna mahusiano ya miaka9 yatakosa taarifa muhimu Kama hii kweli? Yaani hata Ingetokea hilo swali halikuulizwa(japo ningumu),huyo dada angeshindwa kueleza kitu muhimu Kama hicho?
Na inamaana wakiwa wote yule mwanamke alikuwa anajihesabu anawatoto wawili wale alozaa na jamaa. Mahusiano yangekuwa ya wiki au mwezi tungemtetea huyo mwanamke Ila sio miaka yote hiyo.
Haya mahusiano ya siku hizi ni shida. Mnapoanza mahusiano kabla hata ya kuanza kula mbususu lazima muulizane maswali muhimu kuhusu background zenu. Je mna watoto, ulishwahi kuoa au kuolewa, asili yenu etc. Hii itapunguza mambo mengi huko mbeleni kama mnataka kwenda next stage. Mmeishi 9 yrs halafu usimuambie mwenzako una mtoto? Na huyo bwana naye hakuwahi kuuliza au? Au mwanamke alimdanganya?
 
Back
Top Bottom