Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

Kuna Dada mmoja naye alikutana na Mwanaume wakapendana, wakatambulishana pande zote mbili na wakafunga Ndoa Kanisani kumbe Mwanaume alikuwa tayari ana Mtoto wa Kike mkubwa hakumjulisha hilo, miaka imekwenda yule Dada akagundua hilo alilia sana Mwanaume aliomba msamaha akidai alimficha maana alimpenda sana akaogopa kuachwa,walisameheana maisha yakaendelea ni vizuri kuwekana wazi mapema kwani kweli humuweka mtu huru.
 
Kuna Dada mmoja naye alikutana na Mwanaume wakapendana, wakatambulishana pande zote mbili na wakafunga Ndoa Kanisani kumbe Mwanaume alikuwa tayari ana Mtoto wa Kike mkubwa hakumjulisha hilo, miaka imekwenda yule Dada akagundua hilo alilia sana Mwanaume aliomba msamaha akidai alimficha maana alimpenda sana akaogopa kuachwa,walisameheana maisha yakaendelea ni vizuri kuwekana wazi mapema kwani kweli humuweka mtu huru.
Hilo nalo nendeni mkalitizame
 
Yeye alikuwambioni kufunga ndoa.Hata hvy anachosikitika nikutoambiwa mapema.Mwenyewe anadai angeambiwa mapema Wala asingekuwa na tatizo
Hakuna tatizo, maana hata yeye hamuuliza kama amezaa. Sasa ulitaka aanze tu kujiongelesha? Wewe unafikiri huyo jamaa alikuwa Bwakira?
Huenda kupatikana kwa huyo mtoto kuliambatana na tatizo kubwa hivyo hapendagi kuliongelea.
 
Sikufichi mwanamke akiwa na mtoto then umuoe inaboa labda jamaa ake awe kafariki yaani kijana utakufa kwa mawazo kwa kweli labda awe mchepuko lakini kuoa!!!

Jiulize jamaa wa kwanza mpaka kampa mimba na demu kaibeba mpaka kajifungua na tambua mwanamke anabeba mimba ya mwanaume anayempenda tu .....swali je huyo jamaa kwa Nina asimuoe ? Na kashamvua chupi mara kibao..
Kama alibakwa? Au jamaa alifariki? Kwa hiyo ulitaka aitoe mimba?
 
....Hakuna sababu ya kukasirika

Walikosea kuishi kisela

Mwanamke pia alikosea kuficha mtoto
 
Sitetei naongea ukweli.Sio kila singles mother ni mbaya,na kuwa single mother sio dhambi.Na Kwa Hilo tukio sioni ubaya aloufanya huyo dada.Mtoa mada alipaswa kusema wanaume ulizeni historical background ya wenzi wenu.Labda bibie hakuulizwa chochote angewezaje kukurupuka eti nna mtoto ili iweje?
Nani tena kakwambia kuwa single mother siyo dhambi? Ni dhambi kubwa mno.
 
Imeshatokea hiyo unavaa bomu tu hamna namna, waendelee na maisha.

Bado hata wangefuata taratibu shida iko pale pale, watu waliamua kulificha hili, bado wangelificha tu, na wakati wa yeye kujua ungefika angejulishwa tu kama alivyojulishwa.
 
Hivi mwanamke unaficha mtoto wako ulomzaa Mwenyew sabbu ya msingi ni labda
 
Tatizo liko wapi sasa,kwani wamesema amchukue mtoto akamsomeshe au? Si wamwache hapo waendelee na maisha Yao....Yeye kumzalisha Binti was watu bila ndoa Wala kutambulika hakukosea au? 😠
Huyo jamaa atakuwa bado ni mvulana mwenye akili ya kitoto, sitashangaa akichukua uamuzi wa kujiua.
 
Huyo jamaa atakuwa bado ni mvulana mwenye akili ya kitoto, sitashangaa akichukua uamuzi wa kujiua.
Hadi hapa bado nimvulana au anastahili tuzo.Kumbuka hadi saivi yupo kwenye kuwaza Ila hajafanya maamuz yoyte either mazuri au mabaya.
 
Nawasalimu nyote

Rafiki yangu yupo kikazi Dodoma tangu mwaka2013.

Mwaka huo aliripoti kazi na dada mmoja mwenyeji wa Babati.Jamaa kwao ni Tanga. Hapa na pale baada ya miezi kadhaa wawili hawa wakajikuta niwapenzi.

Mapenzi yalivyokolea wakaamua waoane kimjini mjini.Yaani waliishi pamoja bila kwenda kujitambulisha kwa wazazi japo kwa njia ya simu waliwapa taarifa.

Likizo zote walikuwa wanabaki huko Dodoma na pale ilipobidi kwenda nyumbani kila mmoja alienda kwao.
Mwaka2015 wakafanikiwa kupata mtoto wao wakwanza.Hapo Sasa wazazi wa upande wakiume wakalazimisha jamaa ampeleke mtoto nyumban.Kwa kuwa mtoto hawezi kwenda mwenyewe ikawa ndo nafasi Sasa ya jamaa kwenda namkewe.Wazazi wakafurahi kuona mjukuu na mkwe wao.

Miaka mingine ilofuata kila mmoja alikuwa anaenda kwao wakati wa likizo na wasipoenda walikuwa wanabaki wote Dodoma. Mwaka huu jamaa wamebahatika kupata mtoto wao wapili.Upande wa mwanamke nao wakakomaa kuwa wanataka kuona wajukuu pamoja na baba yao.Jamaa akaamua atumie likizo yake hii kwenda ukweni Babati.

Wamefika ukweni wamepokelewa vizuri bila shida yoyote.Baada ya muda anakuja binti wa Kama miaka13 hivi.Amefurahi kweli kuwaona pale lakini zaidi anamchangamkia mke wa jamaa. Baada ya shamrashamra mama mkwe anatoka huko jikoni na kumwambia Yule binti"umefurahi kuwaona wadogo zakoee, nahuyo ndo baba yenu msalimie vizuri".

Nifupishe tu hii stori kwa kusema yule mke wajamaa alikuwa na mtoto aliyemzalia nyumbani kabla hajaenda kikazi Dodoma.Kuzalia nyumbani sio shida,tatizo nikwamba kwa miaka yote aliyokaa na jamaa hakuwahi kumwambia kuhusu yeye kuwa na mtoto nyumbani.Mtoto(binti)yupo darasa la saba mwaka huu.

Usiku badala yakuwa muda wa kubwaga moyo jamaa wakaamua wautumie kwa mazungumzo ya kilichotokea.
Mke wajamaa alikiri kuwa kweli binti ni wakwake Ila alishindwa kumweka wazi jamaa kwa sababu ambazo kimsingi hazikuwa na mashiko.

Jamaa alipanga akae siku mbili tatu ukweni ila amekatisha ziara na karudi Dodoma.Amechanganyikiwa,ameshindwa kukisanua pale ukweni hvyo ametulia akifikiri nini Cha kufanya.

Nimemtuliza jamaa kwani hasira alizokuwanazo siwezi shangaa nikiambiwa kaua na kujiua.Ubaya tu nikwamba pamoja na mkasa huo mzito akifanya mauji polisi watasema chanzo Cha mauaji ni WIVU WA MAPENZI.
Mke bado yupo Babati kwani walikubaliana tangu mwanzo kuwa jamaa angewaacha huko walau wiki mbili.

Wakuu,hili nalo linapitaje kwa huyu rafiki yangu

Ushauri wangu; Kama umekutana naye mjini mkapendana,fanya hima uende kwao...Kuna mengine yamuhimu utayagundua ukifika.

Wasalaam!
Na kinachofuata mke atarudi na huyo binti.
Na jamaa atatakiwa kumtunza.
Maisha ndivyo yalivyo kwa Sasa.
Kumpata binti ambaye Hana mtoto ni nadra Sana.
Zamani wanaume ndio walikuwa wanaoa wakiwa na watoto.
Siku hizi tunaoa upande mwingine ukiwa na goli tayari.
Dunia imegeuka
 
Huyo dada ni gaidi kama magaidi wengine tu.
Mimi huko ukweni hata Kama tutaendelea kuishi siendi Tena.
 
Ndio maana wanasema, kabla hujaoa mke au kuolewa peleleza kwanza familia anayotoka
 
Kuna mzee alinihimiza sana kama nataka kuoa basi nijitahidi kumfahamu vizuri binti na familia yake kwa ujumla.

Ongea na majirani wawili watatu kuijua familia yao na yeye pia.

Hizi mambo za kuchukuana tu, utakosa wa kumlilia..
Utalilia jamiiforums mkuu
 
Back
Top Bottom