Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

Kuna Dada mmoja naye alikutana na Mwanaume wakapendana, wakatambulishana pande zote mbili na wakafunga Ndoa Kanisani kumbe Mwanaume alikuwa tayari ana Mtoto wa Kike mkubwa hakumjulisha hilo, miaka imekwenda yule Dada akagundua hilo alilia sana Mwanaume aliomba msamaha akidai alimficha maana alimpenda sana akaogopa kuachwa,walisameheana maisha yakaendelea ni vizuri kuwekana wazi mapema kwani kweli humuweka mtu huru.
 
Hilo nalo nendeni mkalitizame
 
Yeye alikuwambioni kufunga ndoa.Hata hvy anachosikitika nikutoambiwa mapema.Mwenyewe anadai angeambiwa mapema Wala asingekuwa na tatizo
Hakuna tatizo, maana hata yeye hamuuliza kama amezaa. Sasa ulitaka aanze tu kujiongelesha? Wewe unafikiri huyo jamaa alikuwa Bwakira?
Huenda kupatikana kwa huyo mtoto kuliambatana na tatizo kubwa hivyo hapendagi kuliongelea.
 
Kama alibakwa? Au jamaa alifariki? Kwa hiyo ulitaka aitoe mimba?
 
....Hakuna sababu ya kukasirika

Walikosea kuishi kisela

Mwanamke pia alikosea kuficha mtoto
 
Nani tena kakwambia kuwa single mother siyo dhambi? Ni dhambi kubwa mno.
 
Imeshatokea hiyo unavaa bomu tu hamna namna, waendelee na maisha.

Bado hata wangefuata taratibu shida iko pale pale, watu waliamua kulificha hili, bado wangelificha tu, na wakati wa yeye kujua ungefika angejulishwa tu kama alivyojulishwa.
 
Hivi mwanamke unaficha mtoto wako ulomzaa Mwenyew sabbu ya msingi ni labda
 
Tatizo liko wapi sasa,kwani wamesema amchukue mtoto akamsomeshe au? Si wamwache hapo waendelee na maisha Yao....Yeye kumzalisha Binti was watu bila ndoa Wala kutambulika hakukosea au? 😠
Huyo jamaa atakuwa bado ni mvulana mwenye akili ya kitoto, sitashangaa akichukua uamuzi wa kujiua.
 
Huyo jamaa atakuwa bado ni mvulana mwenye akili ya kitoto, sitashangaa akichukua uamuzi wa kujiua.
Hadi hapa bado nimvulana au anastahili tuzo.Kumbuka hadi saivi yupo kwenye kuwaza Ila hajafanya maamuz yoyte either mazuri au mabaya.
 
Hadi hapa bado nimvulana au anastahili tuzo.Kumbuka hadi saivi yupo kwenye kuwaza Ila hajafanya maamuz yoyte either mazuri au mabaya.
Maamuzi atakayochukua yatadhihirisha uvulana wake ama uanaume wake.
 
Na kinachofuata mke atarudi na huyo binti.
Na jamaa atatakiwa kumtunza.
Maisha ndivyo yalivyo kwa Sasa.
Kumpata binti ambaye Hana mtoto ni nadra Sana.
Zamani wanaume ndio walikuwa wanaoa wakiwa na watoto.
Siku hizi tunaoa upande mwingine ukiwa na goli tayari.
Dunia imegeuka
 
Huyo dada ni gaidi kama magaidi wengine tu.
Mimi huko ukweni hata Kama tutaendelea kuishi siendi Tena.
 
Ndio maana wanasema, kabla hujaoa mke au kuolewa peleleza kwanza familia anayotoka
 
Kuna mzee alinihimiza sana kama nataka kuoa basi nijitahidi kumfahamu vizuri binti na familia yake kwa ujumla.

Ongea na majirani wawili watatu kuijua familia yao na yeye pia.

Hizi mambo za kuchukuana tu, utakosa wa kumlilia..
Utalilia jamiiforums mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…