Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

Wazee wa hiyo sehemu walikukaribisha? Unatishiwa tu, ongea na wazee. Mimi walitaka kunipiga kipapai, ila nilipambana na sasa tunaheshimiana. Wewe jua tu maisha ni mchezo, basi cheza kwa step.
 
Nawe inabidi uwatishe kwa mkwara mzito; chukua chungu kikubwa kimwagie damu ya ng'ombe au ya kiumbe chochote, alafu ibuka saa sita mchana jua kali, vaa kaptula huku kichwani umefunga kilemba cheupe; chimba shimo mbele ya kiwanja, na anza kuongea kwa sauti; ''yeyote atakayeleta kijicho au mambo yoyote ya kishirikina katika kiwanja hiki, afe hapo hapo kwa kupigwa na radi ya mizimu'' baada ya kumaliza kusema hivyo anza kuunguruma kama simba.

Ondoka halafu usisemeshane na mtu.

Kwa huo mkwara, hutoona mauza uza tena, watakuogopa.​
 
Fanya maombi
Iombee na kuikomboa ardhi hiyo
Omba kibali cha umiliki
Mfutilie mbali Shetani karibisha ulinzi wa Mungu
Mix chumvi ya mawe na olive oil kiasi tu upate labda litre moja iombee afu mwanga/nyunyiza kwenye pembe za kiwanja na nyumba yenyewe huku ukinuia ulinzi kwa damu ya Yesu
 
Kheeee[emoji16]
 
Unajenga wapi mkuu? Yaani uliponunua kiwanja
 
Mtu akitaka kukusumbua au kukudhuru haijarishi umemfanyia mabaya au mema la! Unaweza fanya mema yote na kipapai ukapewa bila hata huruma.
 
Sawa ila ukiwa unaenda weka unafki kwa majirani kidogo, unajua sisi weusi nuksi sana, yaani unapiga hatua kimaendeleo majirani wanavimba hasira so kuepusha wape hi kidogo, jifanye unawasikiliza ushauri wao nk yaani fast mauza uza yanaisha
Huwa haijarishi mtu mbaya ni mbaya tu.
 
Watu wabaya ni wabaya tu.Hata ukiamua kujipendekeza kwake atataka kukuumiza tu.Ukiumia kwake ni kicheko.Kujinyenyekeza au kuwa karibu nao sidhani kama ni jibu la haraka.
Huo ndiyo ukweli mtu mbaya ni mbaya tu hata ujipendekeze vipi, tena ukiwa na mazoea yakujipendekeza ndiyo anakukula bila kelele huku anakuchekea Meno yote 32½
 
Jenga mji wako, maliza, hamia halafu ukishahamia fuga mbwa. Narudia tena, FUGA MBWA sio kambwa koko...ukiendelea kuona vitimbwi njoo niite **** utanikuta nimekaa pale. Hawa wanahizaya walinisumbua sana hata mimi kipindi niko kwenye ujenzi na punde baada ya kuhamia mara usikie vishindo nje, mara kama watu wanamwaga mchanga juu ya bati, ila nlivyoleta masela hyo habari ilikuwa ni historia.
 
Vip hao mbwa usiku uliwaachia nje
 
Wazee wa hiyo sehemu walikukaribisha? Unatishiwa tu, ongea na wazee. Mimi walitaka kunipiga kipapai, ila nilipambana na sasa tunaheshimiana. Wewe jua tu maisha ni mchezo, basi cheza kwa step.
Eneo lenyewe ninalojenga ni la mjini waliojenga eneo hilo waliowengi sio wenyeji harakaharaka wenyeji eneo hilo waliokaribu nami ni kama watatu.
 
Usijiroge na wewe sijui ukaanza kuizindikia nyumba yako au kumwaga maji ya Mwamposa au kufanya chochote cha kishirikina.

Ukianza hizo mambo za kishirikiana ndio kama unaumwagia moto petrol.

Potezea endelea na maisha mtegemee Mungu akupe ulinzi tu

Utanishukuru baadaye

Narudia tena USIFANYE JAMBO LOLOTE LA KISHIRIKINA ETI LIKUPE ULINZI KWENYE NYUMBA YAKO
 
Mwenye hicho kiwanja yaani yule alomuuziq dogo ndo anakufanyia ujinga.

Yeye alimuuzia dogo kiwanja kwa bei rahisi na wewe dogo akakuuzia kwa bei kubwa hapo ndo tatizo lilianzia.

Kujua shida ni nini ni simple sana kama wewe sio bahili, tembelea huo mtaa anģalia mtu mzima ambae kaishi hapo muda mrefu hasa mwanaume. Fanya research huyo mtu asiwe wale wazee wasiojielewa wanashida kwenye pombe.

Basi nenda kwake mwambie ukweli wote na muombe akupelelezee chanzo cha hayo mauzauza. Wakati unaondoka mwachie hata efu 30 au 50 mwambie hiyo ni ya vocha tuwasiliane. Usubiri majibu kwa muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…