Mimi site kwangu Tegeta, walikuwa wanavunja nazi pia wanakunya na kuacha vimimika kwenye chupa zenye maandishi ya kiarabu ya rangi nyekundu.
Nilimtafuta jamaa yangu, tukaenda kununua kondoo tukaja nae site akiwa amefungwa kitambaa cheusi shingoni tukamfunga kwenye mti mbele ya site.
Usiku saa sita tukachimba shimo kondoo tukambana korodani akapiga kelele sana,
Tulipohisi majirani wamesikia zile kelele.
Tukachukua majani tukafukia ktk shimo.
Kondoo tukamtia kwenye buti ya gari tukaondoka, kesho yake tukamchinja tukamchoma, na supu ya kutosha,
Waliogopa hata mafundi wakisahau vifaa asubuhi wanavikuta,
Toka siku hiyo sijaona upuuzi tena,