Mliokuwa mnafikiri miradi ya Hayati Magufuli ni halalisho la kuua demokrasia, hili la Bandari litawasaidia kujua gharama ya demokrasia

Mliokuwa mnafikiri miradi ya Hayati Magufuli ni halalisho la kuua demokrasia, hili la Bandari litawasaidia kujua gharama ya demokrasia

Sikumbuki kama lipo bunge lolote hata kabla ya mwendazake lililowahi kukwamisha muswada wowote ule uliopelekwa na Serikali ili ukajadiliwe Bungeni. !!
Halijawahi kuwepo. Kwahiyo wamwache Mwemdazake apumzike kwa amani
 
Sikumbuki kama lipo bunge lolote hata kabla ya mwendazake lililowahi kukwamisha muswada wowote ule uliopelekwa na Serikali ili ukajadiliwe Bungeni. !!
Unakumbuka sakata la Richmond? Unakumbuka sakata la buzwangi? nk yote yaliibukia bungeni enzi hizo
 
Ishu ni kuwa mwendazake alikuwa mzalendo na mtetez wa wanyonge....angekuwa mwizi na mlafi kama mama asingependwa na mtu yeyote nchini
Sasa effect yake ndio hii hapa ya bunge kuwa butu kabisa. Inabidi kuangalia matokeo ya mbeleni na hiyo ndio shida ya afrika. Kwamba huyu mnayemsema mzalendo kwa haya ya kupoka madaraka na kuongoza bunge, je akija mtu asiye mzalendo itakuwaje? Na matokeo ndio haya sasa.
 
Hii vita itakushinda ukiendelea kumuona mwendazake mbaya! Kwenye hili taka usitake mwendazake anaendelea kuwa shujaa
Mwendazaka was an evil to this country he did more harm than good......huo ndo ukweli mtupu.
 
Hii vita itakushinda ukiendelea kumuona mwendazake mbaya! Kwenye hili taka usitake mwendazake anaendelea kuwa shujaa
Kwangu mimi, shujaa ni yule kiongozi ataehakikisha watanzania wanapata katiba mpya na iliyo bora hata kama hatajenga hata kilomita moja ya lami, kwani kupitia katiba mpya, hata barabara za lami zitajengwa tena nyingi zaidi ya hizi tulizonazo leo hii.
 
Sikumbuki kama lipo bunge lolote hata kabla ya mwendazake lililowahi kukwamisha muswada wowote ule uliopelekwa na Serikali ili ukajadiliwe Bungeni. !!
Lakini hayati JPM alipinga hadharani masuala kama ya mikataba ya kienyeji na kilaghai kama mkataba wa Bagamoyo wa wachina. Alitaka kuwepo upembuzi katika zile "terms" ile aloikuta na ile ilokuwa ikipigiwa chapuo.

Video zipo Youtube akielezea hilo la bandari ya Bagamoyo.

Hivyo ni wazi asingeweza kuridhia hiyo kitu.
 
Kwangu mimi, shujaa ni yule kiongozi ataehakikisha watanzania wanapata katiba mpya na iliyo bora hata kama hatajenga hata kilomita moja ya lami, kwani kupitia katiba mpya, hata barabara za lami zitajengwa tena nyingi zaidi ya hizi tulizonazo leo hii.
Hivi weye kwa akili zako timamu wadhani CCM ikiendelea kukaa madarakani kutakuwepo na katiba mpya?

Mkataba wa Bandari tayari ni kielelezo cha kuonyesha kwamba CCM bado itaendelea kuwepo kwa miaka zaidi na zaidi.

Cha msingi weye endelea na maisha yako wapoteza muda wako bure na hizi siasa ya Tanzania.

Au yafanye lakini iwe ni part-time.

Hivyo ndivyo kila mtu aishi sasa hivi.
 
Hivi weye kwa akili zako timamu wadhani CCM ikiendelea kukaa madarakani kutakuwepo na katiba mpya?

Mkataba wa Bandari tayari ni kielelezo cha kuonyesha kwamba CCM bado itaendelea kuwepo kwa miaka zaidi na zaidi
Kwakweli !! Labda kwa Rehema za Mungu tu !!
 
Mkataba wa bomba la mafuta aliingia mwenda zake kimya kimya hauna masirahi kwa taifa bora mama kawake wazi kwa kila mtanzania kujua.
Mkuu, acha kudanganya wakati jua lachwea.

Kama wazungumzia mradi wa Chongoleani mbona ulitangazwa na video zipo yotube?

Na leo hii wametoa fursa kwa vijana wa Tanzania na Uganda wajiorodheshe ili wapewe mafunzo ya kufanya kazi kwenye mradi, mwisho wa kujiandikisha ni tarehe 28/6/23

Sasa utasemaje mkataba uliifanyika kimyakimya?
 
Kwaio uchaguzi huru na wa haki ni kwa JPM tu?sio kwa Mwinyi, Mkapa or JK, au hawa wengine hawakufanya uchaguzi?ht uchaguzi ungekua huru na wa haki upinzani wasingekua na wabunge zaidi ya Nusu bungeni kuweza kuzuia muswada, hizi ni hesabu za kawaida tu huitaji kua mtaalam wa statistics kulijua hili.
Mpina angeungana na wapinzani wangekuwa wengi bungeni.
 
Mkuu, acha kudanganya wakati jua lachwea.

Kama wazungumzia mradi wa Chongoleani mbona ulitangazwa na video zipo yotube...
Unajua details za huo mkataba, mda wake? Faida ya taifa? Nk.
 
Mpina angeungana na wapinzani wangekuwa wengi bungeni.
CCM ni "masters in the game" au "legends" waliishagundua kitambo watanzania wengi ndo hivyo tena.

Hata huyo Mpina huenda yupo chini ya uratibu maalum wa kucheza na akili za watanzania.

Tanzania ni nchi ngumu sana ambayo haileweki siasa zake.

Hii yanikumbusha mzungu mmoja huko nje aliposikia JPM kafariki akawa asema "ooh dear the poor man is gone, he was fighting the losing battle".
 
Back
Top Bottom