Magufuli ni Mwalimu wao wa kuendesha nchi ambae awakumuelewa, kwa sababu ya wivu wao wa kazi zake.
Hila sasa wanajutia uongo wao, Magufuli akuwahi zuia habari kama wanavyomsingizia hila alitaka sheria ambayo ipo itumike kwenye kupotosha.
Aliingia madarakani magazeti yakiwa yanaweza andika mama ajifungua chatu huku yanachekewa na huko CDM kulikuwa kuna kiwanda cha kutunga uongo; kama kwenye ili sakata la IGA 99% ya mada za kwenye ili jukwaa ni kuto kuelewa ‘the law of contract’ hiyo ndio shida hasa kuhusiana na maswala ya FDI. Yeye akishaelewesha halafu ukaendelea kutunga uongo uwe ubalozi, chombo cha habari au mwanasiasa mtaelewana.
Kingine ni swala la mikutano ya hadhara it’s political etiquette nchi za wenzetu baada ya uchaguzi; kufunga mikutano ya hadhara mpaka kipindi cha campaign. Donald Trump achezi na rules hizo na vyombo vyao vya usalama vimeshamchoka. East Africa hasa Kenya na Tanzania hatuna ustaarabu huo; sisi tunataka mikutano ya hadhara kila siku ya mwaka for 5 years hilo ni tatizo.
Otherwise Magufuli was the best president ever in Sub-Sahara Africa.
Hawa walilipwa mara tu walipogundua kuwa hakuna kale kamchezo kale ka kudonoa keki hivyo wakaanza zogo.
Hata mimi nikiwa raisi wa Tanzania sitapenda upuuzi wa kudonoa keki kisha kuleta zogo kwani hawa wafanya ile kitu yaitwa distraction yaani kumvuruga mtu ili ama atoe maamuzi ya pupa au apoteze mwelekeo.
Huko kwa wenzetu (nchi ziloendelea) uchaguzi ukiisha (labda kama kuna zogo kama inosemwa ya 2020) vyama vyote huketi kuanza kazi ya kuimarisha uchumi , kushughulikia matatizo mengine ya ndani kama elimu, afya na elimu na hata uhamiaji ni "hot topic" huko nje.
Lakini ikifika muda wa uchaguzi kampeni huanza na vyama hushindana hoja mbalimbali na wapiga kura "electorate" hupima hoja na kuzichambua na baadae huandaa hata midahalo.
Lakini kwa Tanzania wanokifanya wapinzani uchwara na kinowafanya waonekana ni wa hovyo ni kuanza zogo, hakuna sera mbadala bali zogo tu la katiba mpya ambayo wapinzani hawahawa waelewa wazi kuwa hakuna hiyo kitu, katiba mpya na haitokuja kutokea chini ya utawala wa CCM.
Lakini chini ya CCM hiyohiyo hayati JPM alitaka nae apitishe mambo yake kinguvu jambo ambalo kwa upande wake alikuwa amepotoshwa na akakosea maana alizungukwa na watu wanafiki.
Nchi hii hata kama atatokea tena mtu mwenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kifikra ambae ana kundi lake nyuma lenye nguvu ni pale tu atapoamua kufanya maamuzi magumu ya kuleta katiba mpya.
Maamuzi hayo yataigharimu CCM "big time" lakini itakuwa kila mtu asema "to hell" twataka "new direction".
Baada ya hapo ni kuwaita wanojiita wapinzani wote ni kuwapa somo namna ya kukosoa kwa staha na kwa kutumia akili bila kutumia matukio na vibahasha vya akina Amsterdam.
Wapinzani pia watakiwa kutotegemea sana ruzuku ya serikali maana hiyo hutumika kama fimbo au kamba ya kuvuta ukionekana wavuka mstari mwekundu.
N antaweka wazi kabisa kwamba serikali yangu haina vibuyu vya asali.