Mliokuwa mnauliza kazi ya Rostam Aziz kwenye ziara ya Rais Samia ya Marekani, hili ndio jibu lenu!

Mliokuwa mnauliza kazi ya Rostam Aziz kwenye ziara ya Rais Samia ya Marekani, hili ndio jibu lenu!

Dua zetu kwa mawakili wasomi hawa walio kiwasha mahakamani mkataba unaenda kutenguliwa huu mbele ya mahakama ya sheria. Wapi kibatala wakili msomi sana wapi TL wakili mbobezi
 
Ukitaka kujua historia ya Rostam tafta wastaafu wa enzi zile jamaa bado kijana anafanya biashara ya Ngozi na Kiwanda cha Ngozi Mwanza(Tanaries). na dili

Jamaa kaanza ufisadi enzi za Mwinyi now anafanya kumalizia tu.

He has been corrupted for a long time.
Nakumbuka akiwa kijana na alipofanikiwa kuwa mbunge kijana zaidi wa Igunga baada ya kifo cha Kabeho(?) alikuwa ni mchuuzi tu wa ngozi lakini akautumia udhaifu wa viongozi wetu na sasa yeye ndie Don, mfalme wa mikataba na dili nyeti, huyu ndie kama akina Vallambia wale wa Rada magumashi.
 
Intelejensia ya Dunia katika karne ya 21 imebadilika sana! Nchi nyingi duniani sasa zinafanya kazi kutengeneza nguvu na ushawishi kwenye uchumi!

Kupata nguvu na ushawishi kwenye Uchumi kunahusisha kutengeneza matajiri wakubwa wenye pesa wanaoweza kuwekeza, kushawishi uwekezaji, kuongeza ajira na mapato ya nchi kupitia ushawishi kwenye uwekezaji

Ukienda Misri kuna Nasser Sawaris anaemiliki viwanda vingi vya cement na shareholder wa kampuni kubwa zaidi ya vifaa vya michezo ulaya Adidas

Ukienda Afrika kusini Kuna Patrice Motsepe
anaemiliki shares nyingi kwenye makampuni mbalimbali ya madini

Ukienda Nigeria kuna Aliko Dangote mwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa cement , Sukari na mafuta na sasa anatengeneza refinery ya kwanza ya mafuta katika Bara la Africa

Tanzania tunae Rostam Aziz mmiliki wa kampuni ya Caspian, Taifa Gas, Tigo na Zantel! Huyu kuaminika kwake kunafanya kuwa mtu ambae Tanzania tunamtegemea sana kwenye kishawishi uwekezaji mkubwa unaotengeneza fursa za ajira na kukuza mapato na Uchumi wa nchi yetu

Urusi wanao wengi akiwemo Roman Abramovich aliyekuwa mmiliki wa club ya Chelsea

Marekani ndo usiseme wanao wengi na wanazidi kuzalisha wengi kila siku kama Jeff bezoz, Bill Gates, Warren Buffet, Elon Musk na wengineo wengi

Mfano wa kazi nzuri za Rostam Aziz kwa Tanzania ni huu! Katika ziara aliyoambatana na Rais Samia Marekani, ameweza kushawishi uwekezaji mkubwa katika kilimo hapa Tanzania kupitia Benki ya maendeleo Afrika.

Hongera Rais Samia, naiona akili kubwa sana kwako inayoenda kuibadili haraka sana Tanzania kiuchumi


View attachment 2207616
 
Back
Top Bottom