Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

kwa utawala huu katili labda mpaka Mungu aingilie kati, karma itende sawasawa na matendo yao!.
 
Fikra zenu watu wengine mnazijuaga wenyewe! Wewe ulishawahi kuona wapi jambazi anatishika kwa message ya kwenye social media?

Ni juhudi ambazo hazina hata ile harufu tu ya tija!
Umesahau kilichotokea Tunisia na Egypt kupitia social media?
 
Unashawishi sana wewe kufanyiwa utafiti mdogo unapoandika haya humu.

JF haipotezi kitu. kumbukumbu za michango ya kila aliyewahi kuandika chochote humu JF zipo; na zinaweza kufukuliwa na kultwa kuunganishwa na bandiko kama hili uliloweka hapa.

Lakini naomba usinielewe vibaya. Kila mtu anayohaki ya kubadilika au kubadili mawazo kwa sababu mbalimbali.

Kama umeamua baada ya kuona kuwa ulipotea njia, nakupongeza sana.

Daima. Ni Tanzania yetu pekee ndiyo itadumu milele. Tuienzi kwa wakati wetu huu.
 
Hii mikwara ya nyuma ya keyboard noma Sana......
 
Sasa kama waliuwawa siri inatunzwa wapi? Duniani? Mbinguni kibano kiko pale pale
 
Aliyetoa amri walinzi waondolewa area D ili Tundu Lissu auwawe ndiye mhusika mkuu ktk ugaidi ule.

Na maelezo ya Polisi ambayo hayajanyooka, na ya kupiga-piga chenga, yanaelekeza tuhuma hizi mahala fulani.

Familia ya Tundu Lissu ilimuomba Waziri wa Sheria[kabudi] na Mwanasheria Mkuu[kilangi] wawashirikishe wachunguzi toka nje ili HAKI ipatikane.

Bahati mbaya ombi hilo lilikataliwa. Sasa unajiuliza kwanini?
 
Sudani ni Sudani, Tunisia ni Tunisia

Haya mambo yanakwenda na asili ya watu wa eneo husika plus imani na tamaduni na desturi

Sio kwa watanzania

Kama kuna mtu ana ndoto za mchana asahau
 
Hiyo pia inaweza kuwa 'misinformation' ikitumika kuwalinda.

Vilevile kwanini jeshi la POLISI halifanyi uchunguzi?

TL alipokuwa nchini alifika mpaka kwa RPC wa Dodoma kudai gari lake.

Kama victim yuko, na anazungumza, sielewi kwanini Polisi wameshindwa kumhoji.
 
Kuna watu wanataka kuwapandikiza watanzania akili za kiarabu

Sisi ni taifa lenye amani, kama umekata tamaa ni wewe, Magufuli atatumikia muda wake ataondoka hatuna muda na mambo ya kipumbavu
 
Back
Top Bottom