Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

Dogo umekosa chakuandika yaani huyu jamaa alieko ulaya ndo ashinde vichwani mwa watu kama alipigwa risasi na amepona inatosha kumshukuru mungu maswala ya haki yeye anajua sheria zaidi yako mwachie mwenyewe
Unahusika nini mbona povu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Haaaa, mbona Watanzania hampendi Taifa lenye haki? Unadhani ni Lissu pekee aliyeonewa? Wengi tu wanaonewa na vyombo vya dola. Tunataka haki.
 
Mimi sina ujamaa na Lissu. Nasimamia misingi ya kisheria kuwa jinai haina mwisho. Ukifanya kosa leo utakamatwa hata baada ya miaka mia. Je waliompiga Lissu, jinai yao ina mwisho?
 
Instagram media - Bt2Krycj3b7.jpg
 
Watanzania watu wapole Duniani hakuna tena, limeisha hilo
 
  • Thanks
Reactions: T11
Vilevile kwanini jeshi la POLISI halifanyi uchunguzi?

TL alipokuwa nchini alifika mpaka kwa RPC wa Dodoma kudai gari lake.

Kama victim yuko, na anazungumza, sielewi kwanini Polisi wameshindwa kumhoji.
Jamaa (polisi), hata kujaribu kuweka juhudi za kuzuga wameshindwa, wameona waache watu wajiamrie wenyewe waonavyo inafaa.

Wameliacha jambo hili likining'inia. Yeyote atakayetaka kulifuatilia baadae wakati na mazingira yakiruhusu ana uhuru wa kufanya hivyo.
 
Walimtaka dereva mkamkimbiza watie juhudi gani?

Mhanga ni mtu wenu, mnakimbiza ushahidi wenu halafu mnataka watu wajisumbue
 
Tafuta interview ya Mwigulu Nchemba na Hassan Ngoma wa Clouds 360.

Hassan Ngoma alimshtukiza Mwigulu kwa swali kuhusu walinzi wa area D.

Mwigulu alianza kujiumauma na Clouds wamekatisha video clip iliyoko kwenye mtandao.

Kwa maoni yangu, siri ya shambulizi la Tundu Lissu anayo mhusika aliyeondoa walinzi wa area D.

Fikiria mambo ambayo yangesemwa dhidi ya Tundu Lissu na dereva wake kama wasinge-survive shambulizi lile.
 
Walimtaka dereva mkamkimbiza watie juhudi gani?

Mhanga ni mtu wenu, mnakimbiza ushahidi wenu halafu mnataka watu wajisumbue

Hicho ni kisingizio tu.

Lissu ni shahidi muhimu zaidi kuliko dereva.

Na Lissu alipokuwa nchini alikwenda mpaka ofisini kwa RPC wa Dodoma.

Polisi wangekuwa na interest ya kuchunguza wangemhoji Tundu Lissu wakati yuko hapa nchini.

Lakini ukiacha Tundu Lissu na dereva kuna watu wengine wengi wanaotakiwa kuhojiwa.

Mmoja wa mashahidi muhimu sana wa shambulizi dhidi ya Tundu Lissu ni mhusika aliyeondoa walinzi eneo lilipotokea tukio.

Maelezo ya aliyeondoa walinzi eneo lilipotokea tukio yangewezesha Polisi kujua ni nani waliokuwa nyuma ya agizo hilo.
 
Dogo umekosa chakuandika yaani huyu jamaa alieko ulaya ndo ashinde vichwani mwa watu kama alipigwa risasi na amepona inatosha kumshukuru mungu maswala ya haki yeye anajua sheria zaidi yako mwachie mwenyewe
Kwahiyo kupigwa risasi na kupona ndio iwe mwisho kuzungumzia haki? Kujua kwake sheria ndio iwe mwisho kuzungumzia haki?
 
Sio kila jambo linakwenda kama sheria inavyotaka au wewe unavyotaka, wakati mwingine busara inatumika tu, wakati wa uchaguzi haukuwa wakati wa kuhojiana kama ilikuwa lazima kumhoji basi ndo ujue hakuhojiwa na huna namna kulazimisha ahojiwe wakati ule

Wakati ambao ulifaa kuhojiwa akakimbilia ubalozini huku akisingizia kutishiwa na alipofanikiwa kutoroka mkamsifu kwa umwamba na ujanja

Tusisumbuane
 
Back
Top Bottom