Mliowahi kuishi Ulaya: How does it feel kutembea Mjini bila kero za Bajaji, Bodaboda na Machinga?

Asante meku😅
 
Ijapokuwa sijawahi kufika ulaya lakini kwa watu wenye kupenda utulivu wa akili na nafsi hakika ina feel better, lakini kwa kuwa nchi zetu ni maskini na serikali zake dhalimu zenye kujali matumbo yao na maslahi yao, bajaji, boda na machinga zimesaidia pakubwa Watu kutafuta kipato chao halali na kupunguza wimbi la wezi kwa kiasi fulani
 
Ni kama umasikini na uchafu, fujofujo na kutostaarabika vinaendana
 
Jiji kama Dar lazima liwe na shangwe shangwe na hekaheka nyingine.
Kelele ndiyo burudani ya mjini.
Mengine siyo lazima tufanane na miji ya Ulaya.
Mengine tunafurahia kufanana na miji kama ile ya India.
Sasa utakuta mji kama Berlin una wakazi milion 3.8 au Paris na idadi ya wakazi chini ya milion 2.5, miji kama hiyo haiwezi kuwa na vibe kama Dar lenye watu zaid ya milioni 7.
 
Kiatu changu cha ngozi kilikuwa marinading sana...  kiwi iliweza kudumu kwa siku tatu... ni mwendo wa kupangusa vumbi tu..

Kelele za honi nilisahau kabisa....yaani gari linakupiisha pasi honi... ukienda stendi za mabasi hakuna kelele.. za wapiga debe..

Kwenye vituo vya Daladala/ Mwendokasi hakuna kubanana...

Ni mengi tu...

Mwakani tunahost AFCoN... sijui aibu yetu itaificha wapi...
 
Hatuwez wote tukaishi sawa, jamii zinatofautiana kitamaduni na kiuchumi
Katika jiji la Dar kuna maeneo yamepoa, unaweza kuishi huko.
Ohstarbay, Masaki, Kijichi, Kisota nk.
Heka heka zipo Kariakoo na maeneo ya uswahilini, siyo lazima ujumuike maeneo yenye shangwe na heka heka
 
Ukishindwa kuishi miji iliyostaraabika kama hiyo basi ujue ule uswahili wa Mbagala, Buguruni, Tandika umekujaa mno kichwani

Binafsi napenda mno utulivu wa aina hiyo badala ya vurugu zetu za hapa Bongoland
 
Haiwezekani wote tuishi kwa kupoa kama tunaumwa baridi yabisi na kutia huruma ambayo tutajidai tunatafakari mambo.Ni hekaheka tu hadi kieleweke.
DIJAY SINDIKIZA COMMENT

[Link removed]

Kuna watu wamelala hadi saa hii...Dejay amsha majirani! Amkeni Bwana, hamjui ile siku inakuja kama mwizi, wale wa nuruni wataiona hiyo hapo inakuja. Waliolala watakutwa voop wabaki kulia na kusaga meno! ! ! THE KING OF KINGS IS COMING! 🔥🔥🔥🔥🔥🔥

AMKENI BWANA. DEJAY


View: https://www.instagram.com/reel/DXOXwYbCFyf/?igsh=aGk4bXVubDhsN3Y4
 
Na ndo wanaongoza kwa depressions na kujiua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…