Google wanatukia AI nyingi za aina tofauti tofauti (Google lense, multisearch, etc) Na sasa wamekuja na Bard ambayo hawajaiachia kwa watu wengi.
Hii issue ya ChatGPT sio kwamba ndio ushindi wa moja kwa moja kwa Microsoft, nop. Bado wana mziki mzito mana Google ana infrastructure pendwa zaidi.
Tukumbuke kuwa kila simu inakuja na search engine pendwa (Google Search). Siku tu akiiwezesha Google Search kupokea maelezo badala ya keywords amepindua meza.
Kwasasa Google search inapofeli ni kwamba Algorithm yao inajikita kupokea keywords not conversations.