TANZIA Mmiliki wa Blog ya Maswa Yetu na MwanaJF, Innocent Lugano Mbwaga afariki dunia

Mwendeshaji na Mmiliki wa Mtandao wa MASWA YETU BLOG, Innocent Lugano Mbwaga maarufu Blogger Boy amefariki dunia.

Innocent mkazi wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu ambaye ni Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara amefariki dunia leo asubuhi Ijumaa Desemba 8,2023 wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitali baada ya kupata ajali ya pikipiki Tandahimba Desemba 5,2023.

"Ni kweli kijana wangu kafariki dunia leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda Mtwara, alipata ajali ya pikipiki siku ya Jumanne akitokea kazini kwake Tandahimba...Taarifa zaidi tutaendelea kupeana", amesema baba mzazi wa Innocent mzee Mbwaga.

JamiiForums alikuwa anajulikana kwa jina la Lugano5

View attachment 2836365
R.I. P Innocent Mbwaga
R.I.P my man😪😪
 
RIP Blogger Mbwaga
 
Ushauri kwa Maxence Melo hizi nyuzi za tanzia zisiwe na sehemu ya comment kwa sababu haina maana. Maelezo/maelekezo yote yawekwe kwenye main post. Pole zetu hazina mchango wowote kwa familia wala marehemu. Asante
Sikubaliani na wewe Mimi naona ni muhimu iwepo na iendelee kuwepo........

Pole Kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na huu msiba......
 
Back
Top Bottom