Mmoja wa Mawakili wa Erick Kabendera aeleza kinachoendelea

Mmoja wa Mawakili wa Erick Kabendera aeleza kinachoendelea

Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makarazakr lakini bila kujua nani anaandika.Aliandika kwa kujifichaficha, jamboa ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikioa yao namajivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.

Kila mtu atabeba furushi lake. Hivi kama mama mzazi ni chizi, utamtupa nje ya nyumba? Kuna namna ya kufanya kupambana na changamoto. Kuuza utu na heshima yetu nje, ni kujidhalilisha tu. Hakuna mzungu atamkomboa mwafrika
 
Maendeleo yanakuja baada ya watu kubishana kwa hoja,sasa huko kigoma mjini maendeleo yataenda lini kama fedha zote za serikali zinapelekwa cattle???- don't be stupid

Kigoma imeanza kuwepo awamu hii ya tano tu? Mbona Kilimanjaro na Arusha walianza zamani na hatukusema? Kuna ubaya gani Kanda ya Ziwa ikipewa nafasi hiyo? Hata Kigoma itafunguka
 
Kila mtu atabeba furushi lake. Hivi kama mama mzazi ni chizi, utamtupa nje ya nyumba? Kuna namna ya kufanya kupambana na changamoto. Kuuza utu na heshima yetu nje, ni kujidhalilisha tu. Hakuna mzungu atamkomboa mwafrika
Kuna watu hapa TZ na Afrika hushukuru sana wakisikia Mzungu akitukana mataifa yao. Na, Ukiona hivyo, ni ishara na watu ambao evolution haikuwasaidia. Baadhi ni viongozi! Hapa kwetu niliona CHADEMA wakielekea umoja wa EU kushtaki serikali.
Toooo low!
 
Zitto, ni lini utaleta habari za maendeleo ya nchi yako? Waswahili tunakamsemo ketu, "wivu ni kidonda ukishiriki utakonda"

Wewe naye taabu tupu...!!

Maendeleo yanaletwa kwa Zitto kuyaandikia habari/uzi JF au kila mtu atayahisi, kuyashika, kuyanusa na kuyaona kwa macho yake mwenyewe?

Kimya maana yake, no one including yourself is feeling or seeing anything.......!!

Wewe kama unaweza kuyaandikia uzi/thread/mada.....fanya hivyo

Sema tu, Stiglers Gorge, SGR, Bombardier, Chato International Airport, Burigi National Park.....labda tutakuelewa!!
 
Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makarazakr lakini bila kujua nani anaandika.Aliandika kwa kujifichaficha, jamboa ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikioa yao namajivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.
Kwa hiyo hapo tayari wewe ndugu hakimu ,sijui jaji wa mtandaoni tayari umemuona kabendera ana hatia ?Una ushahidi kwamba yeye ndio ameandika hiyo taarifa ?Wakili wake anakwambia anadaiwa kuandika makala hayo ,sasa ni jukumu la waendesha mashtaka kuthibitisha .Hats kama atakuwa kaandika kweli ,aliyoyaandika ni ya kweli kabisa ,shida mini?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Zitto aangalie asije pewa kesi ya kutupa takataka barabarani akakamatwa na Wajeda wa Makondakta
 
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA


Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.

Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.

Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.

Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.

Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.

Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.

Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.

Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.

Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.

Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.

Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.


Imetolewa na

Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.

Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia

Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com
Msaliti msaliti, muache awe ndumila kuwili ili ajue kwa nini watanzania wapo tayari kufa wakimtetea Dkt Magufuli ili atuletee maendeleo, hatutaki wajinga wajinga wanaotaka kushusha ari mioyo ya watanzania wanaosema hapa kazi tu! Akome na akomeshwe huyo msaliti.
 
Mwenye hizo makala zake aweke hapa na tusiojua tumjue.
 
Back
Top Bottom