MNEKI
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 992
- 1,311
Hapa ndipo nasemaga Mzazi unapaswa Kuwa na jicho la tatu hasa linapokuja suala la malezi.
Hizi tamthiria za Azam tv Kuna namna zinatuharibia watoto kwa baadae ,
ROHO YA UZINZI
Mtoto WA darasa la tatu tayari anaanza kujua mpenzi Ni nani,
Mbona kama njia ya kurahisisha maisha ni Kuwa na mpenzi.
ROHO YA ULEVI
-Kuna ulevi humo ndani,, Kuna mtu kanywa pombe kwa sababu ya mawazo,,
Hilo nalo anakaanalo Kichwani.
KUABUDU SANAMU
-Kuna miungu ya sanamu kama ng'ombe wahindi wanaabudu,,,, huyu mtoto badae lazima mtasumbuana kwenye ibada Utakapoanza kumtambilisha kwa Mungu wako wewe.
Wazazi hizo ni baadhi Ya roho Chafu zinamuingia mtoto mapema sana. ...utaona kama hakuna madhara kwa sasa,, ,,,,zinamsubiri mbeleni inakuwa ni rahisi sana kumkumbusha.
Roho gani zilimuingia utotoni ndizo zitaamua tabia zake ukubwani.
Kwa wewe Ndugu yangu usiyepuuzia vitu na unawapenda watoto wako,,
Nakusihi usiruhusu huu ujinga wa matamthiria ya Azam tv.
Mafundisho yapo sehemu ndogo sana na haithiri watoto ukilinganisha na madhara yake kwa baadae.