Mna uhakika Bakhresa na Familia yake wanaangalia haya maujinga

Mna uhakika Bakhresa na Familia yake wanaangalia haya maujinga

Nashukuru hujakanusha madhara ya tamthiria.

Sasa nikuulize?
Nani mwenye Kosa kati ya muuza bangi na mtumiaji?

KUMBUKA: Bangi Ina madhara kwa jamii
Bangi haina madhara kwa jamii, historically bangi iliharamishwa kwa nguvu ya ushawishi wa makampuni ya kutengeneza sigara(back then) na kadri makampuni hayo yanavyopungua nguvu yao ya ushawishi bangi inakuwa legalized slowly but surely. Nchi nyingi zilizo-legalize socially and economically ziko stable zaidi ya nchi yako ambapo bangi imefanya kuwa haramu. Kihistoria TZ ni makabila mengi walikuwa wakitumia bangi ila wakoloni na nguvu ya makampuni yao ya sigara 'wakatutapeli' kwamba bangi haifai nasi tukakubali bila ya kutafakari.
 
Ukimchunga mtoto sana kwenye TV yako sebuleni basi yatakayotokea kwenye smartphone aliyohongwa au kuazima hatakusimulia
 
Me nafikiri Azam media pamoja na kampun nyingne zinazomiliki visimbuzi wanatakiwa watengeneze mfumo wa kila mtu kuchagua channels anazopenda kutazama kwake ili anapolipia zinafunguka alizo chagua tu
Hili wazo jema sana, Binafsi nimeweka News Channel zote
Ningeweka Discovery Channel
Discovery ID
Bloomberg
Za dini ninayoiamini


Ambazo zingetiwa kabatini ni Zote zenye miziki
Katuni zote kabatini
 
Ukimchunga mtoto sana kwenye TV yako sebuleni basi yatakayotokea kwenye smartphone aliyohongwa au kuazima hatakusimulia
Ila unakuwa umefanya sehemu yako, hayo mengine hadi anahongwa maana yake ni mtu mzima.
Kuna umri ukifika tu utajua huyu ana simu
 
View attachment 3283139
Hapa ndipo nasemaga Mzazi unapaswa Kuwa na jicho la tatu hasa linapokuja suala la malezi.
Hizi tamthiria za Azam tv Kuna namna zinatuharibia watoto kwa baadae ,

ROHO YA UZINZI
Mtoto WA darasa la tatu tayari anaanza kujua mpenzi Ni nani,
Mbona kama njia ya kurahisisha maisha ni Kuwa na mpenzi.

ROHO YA ULEVI
-Kuna ulevi humo ndani,, Kuna mtu kanywa pombe kwa sababu ya mawazo,,
Hilo nalo anakaanalo Kichwani.


KUABUDU SANAMU
-Kuna miungu ya sanamu kama ng'ombe wahindi wanaabudu,,,, huyu mtoto badae lazima mtasumbuana kwenye ibada Utakapoanza kumtambilisha kwa Mungu wako wewe.

Wazazi hizo ni baadhi Ya roho Chafu zinamuingia mtoto mapema sana. ...utaona kama hakuna madhara kwa sasa,, ,,,,zinamsubiri mbeleni inakuwa ni rahisi sana kumkumbusha.

Roho gani zilimuingia utotoni ndizo zitaamua tabia zake ukubwani.

Kwa wewe Ndugu yangu usiyepuuzia vitu na unawapenda watoto wako,,
Nakusihi usiruhusu huu ujinga wa matamthiria ya Azam tv.

Mafundisho yapo sehemu ndogo sana na haithiri watoto ukilinganisha na madhara yake kwa baadae.
Hiyo familia nasikia haitumii hata hizo juice wanazozalisha kwenye viwanda vyao
 
Na vile watoto wa siku hizi wamekua na amri kuliko wazazi hata taarifa ya habari haiangaliwi tena ni hayo madudedude
 
Mimi kwangu ni cartoon mwanzo mwisho,ambae hataki ahame.
Ninashukuru Sina tv sebuleni kwangu, Mana media may program my lovely babies mind. Bora wataanza kuangalia wakiwa wakubwa hapo ni sawa , Ila wadogo waendelee kujisomea hadithi kabla ya kulala Kama zamani kupiga stori na babu kabla ya kulala ni Bora , yaani sioni faida ya tv sebuleni, labda niambie Mana nimeshinnda na hayo madude adi kero yaani napenda utulivu Ile human to human interaction
 
Faida za hizi tamthiliya kwa watoto darasa la 2 mpaka kidato cha nne (kwa makisio) ni 0.99,hasara ni nyingi mno.
Content za hizi tamthiliya hazimjengi mtoto,ni vyema wazazi wenzangu mkaliona hili, tamthiliya zimetawaliwa na scene za mapenzi,kiasi cha kuaminisha mabinti kua ukishakua na mpenzi maisha yanakua mepesi sn. Msichana wa shule anaona jinsi msichana kwenye tamthiliya anavyopendwa na kupewa zawadi,kutolewa out na upuuzi mwingine,anashawishika kuanzisha mahusiano ili nayy yamtokee hayo anayoyashuhudia kwenye tamthiliya mwishoe anaangukia kwa wahuni anaachwa solemba,anaharibiwa maisha/masomo chanzo ni ushawishi wa tamthiliya.
Kimaadili na kiimani ndio kabisa,mleta Uzi amesema vyema,Tanzania yetu mostly ni Muslims na Christians,tamthiliya inaonyesha anayeabudiwa si Mungu,ni sanamu na mambo yananyooka tu,hii inamjengea mtoto kua kuna alternative ya kuabudu asiye Mungu na mambo yakaenda.
Mambo ni mengi,tudhibiti kizazi chetu na baadhi ya contents,TV waangalie kwa channels zinazoonyesha contents za kuwajenga,mf. masomo,mafundisho ya dini,michezo,cartoon kuchangamsha ubongo na contents za namna hiyo..
 
Back
Top Bottom