Kuna dogo ana miaka 28 bado hajaoa ila ana girlfriend wake ambae wamejuana takribani miezi minne hivi bila tatizo, kaja kwangu kaka yake aje nimpe ushauri hasa ukizingatia binafsi nimeshaoa na nina familia tayari, pia kwenye mambo ya mapenzi nina uzoefu si haba.
Huyo girlfend wake ni mrembo wa sura na shape kote, kaelimika (sio msomi wa vyeti), kwao pesa zipo maana mzee ni mzito wa kitengo flani, anajitamua, n.k. (Kiufupi hata mimi huwa nampa moyo dogo kwamba hapo alipopata asiachie)
Sasa kuna mnaijeria hapa anataka kuingiza mchanga kwenye kitumbua maana kaanza kuiteka akili ya girlfriend wa huyu dogo,
Dogo kama ni pesa anazo maana alipata bahati adimu mno kuajiriwa shirika ambalo ni ndoto ya wengi kipindi cha magu, ila pia anafanya biashara inayomlipa, ana ndinga kali, kama ni kuhonga tu hata 50 kwa siku huo uwezo anao ila gf wake ni kama huwa anamaindi, huwa anapendaga out hizi za weekend na vizawadi vidogo vidogo.
Kuhusu ishu nyingine kama kuvaa dogo anagonga pamba maana pesa anazo si haba, kama ni gari ya kupigia misele na dem wake anayo ndinga kali tu, kuhusu swaga dogo hajazubaa, kama ni kumjali huyo gf wake anamjali sana tu na gf wake analijua hilo.
Dogo alipiga maswali gf wake kumuuliza ni vipi na huyo mnaijeria, gf wake kakazania ni marafiki tu lakini kwa akili zetu wanaume hii ni hali ya atari (danger zone), muda wowote koloni linaporwa.
Ni mbinu zipi za kivita zitumike kulitetea taji hapa nyumbani?