stonecutter
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 1,724
- 2,584
A. Mazuri ya JPM. 1. Uhodari na uthubutu. 2. Nidhamu serikalini hadi chama (walitiishwa) kwa nguvu ya hatari. 3. Kujipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge (akiliona bango lako au sauti ya kilio chako ikisikiwa, basi utaskia "mwacheni aje" ). 4. Kudhibiti utoroshwaji madini kwa jitihada za kujenga ukuta wa milerani nk. 5. Majangili (wauaji) wa tembo walipoteana. 6. Kujenga hospital za wilaya. Barabara, madaraja, reli, kufufua reli ya kaskazini. Jamani na mengine mengi sana sana. B. MABAYA YALIYOJITOKEZA KTK UTAWALA WA JPM: 1. Wasiojulikana. Hawa jamaa walikuwa hatari. 2. Demokrasia ilifariki na kuzikwa. (hakukuwa na uchaguzi, bali maigizo ya uchaguzi). Wagombea wa upinzani walienguliwa kibabe kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu. Huku lete fyoko uone. 3. Kushtakiwa na kutupwa gerezani kwa kundi flani. Jamani kweli mazuri ya JPM ni mengi kuliko MABAYA. Tuendelee kumkumbuka kwa MEMA kama alivyosema yeye. LAKINI, kama wapo walioumizwa naye na wanamkumbuka kwa mabaya, basi ni haki yao pia.