Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
Masahihisho: Siyo 'Levora' ni 'REVOLA' ambayo ilikuwa ni aina ya sabuni kama Lux, Gardenia na Lifebuoy
 
Gazeti la mfanyakazi. Halafu hapo ifike game ya simba na yanga walikuwa wanaremba balaa! Mechi ya bush star na born town gazetin yani nlikuwa napata hisia km mechi ya kweli vile.
Gaseti la sani
 
Gaseti la sani
Dah tangazo la HIV linaannza milango ya kanisa inafunguka huku wimbo wa majonzi unapigwa halafu pale madhabahuni mtoto anabatizwa huku kuna ndg kadhaa na ndg mmoja nadhan ndio alikuwa ameathirika sijui
 
Chai bora. kilele cha ubora, chai bora ni majani ya Tatepa, iwe na maziwa isiwe na maziwa.....
 
Kuna lingine la air Tanzania, Kilimanjaro... Kilimanjaro
 
Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
Baiskeli ni sunshine(lafudhi ya kisukuma).
 
Poa kk ngoja nikukumbushe tangazo ulilopigwa kofi na mzazi wako(pole lkn)[emoji1] [emoji1] lilikuwa linaimba hivi ngoja nikukumbushe.

Nakupenda mpenzi wanguu
Nakupenda kwa vitendoo
Nimekupa moyo wanguu
Nitakulinda na kinga.
Naukumbuka huu wimbo wa tangazo
 
#HakiElimu
1621957319853.png
 
Kuna lile la bia ya kibo gold ....kibo gold yaone maisha ktk mwanga boraa...nilikuwa nawaza Sana naonaje maisha kwenye kunywa pombe
 
Back
Top Bottom