Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Kuna lile la redio tanzania,ilikiwa asubuh utasikia jambo...sijambo jirani,hamjambo africa mashariki hatujambo...saaafi sana unajianda kwenda skuli umejipaka rays huna shida na mtu
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tangazo la rangi : bwana Moses nimepata mpangaji atakae nilipa kodi ya nyumba yangu hivi lazima uondoke
Aaaaa hapana mzee nimepaka nyumba hivi karibuni naiomba nikae mpaka itakapo haribika Aaaaa haiwezi kuwa taabu hiki ni kipindi cha joto alafu maska baade hii rangi lazima itaharibika atanirudishia nyumba yangu Sawa Sawa mobile lako limekubaliwa
 
Umenikumbusha tangazo la rosheni ya JAMBO kuna jambo kubwa,jambo ndogo na JAMBO KATIKATI[huyu ndo alikua ananifurahisha]
Hahahaaaaa... Yaani umenigusa, Jambo katikati alikuwa ni shida
 
Kulikuwa pia lile tangazo "Posta na simu kweliiiiii agiza barua vitu mbali mbali vifike haraka tena kwa uhakika.........." It was interesting kwa kweli
Iko hivi
Posta na simu kweli
Kweliiii....
Tuma vifurushiii..
Barua na pesa,
Vitu..
Vitu mbalimbali, vifike haraka
Tena, tena kwa uhakika
Litumie sasa shirika la posta na simu Tanzania, ndiyo tegemeo letu
 
Iko hivi
Posta na simu kweli
Kweliiii....
Tuma vifurushiii..
Barua na pesa,
Vitu..
Vitu mbalimbali, vifike haraka
Tena, tena kwa uhakika
Litumie sasa shirika la posta na simu Tanzania, ndiyo tegemeo letu
Long time ago you know mpaka nimecheka
 
Na Tangazo Fulani la babu na mjukuu wake,mjukuu akimuuliza swali babu anajibu kwa methali
 
kuna tangazo moja la condom, lilinifanya nipigwe kofi na bimkubwa sitokuja sahau, lilikuwa jamaa anatembea kwenye mvua anafunika mpenzi wake na koti halaf kuna wimbo fulan mzurii mwishoni nikamalizia "kama kweli unampenda utamlinda!" bwana weee lilekofi nalikumbuka hadi kesho
Hahahahhaaha!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] chaiiii jabaaaa embu tuwasikilizeee mama lisheeeee .....yenye harufu nzuri yenye nguvu kuliko zote...chai jabaaa...kikombeee cha marafikiii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hicho kipande cha tuwasikilize mama lisheeeee kama napaona vileee
 
Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.

Mimi naitwa jambo kubwaa
Na wewe je
Mimi naitwa jambo kati katiii
Na wewe je
Mimi naitwa jambo ndogooo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom