Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Kuna lile la redio tanzania,ilikiwa asubuh utasikia jambo...sijambo jirani,hamjambo africa mashariki hatujambo...saaafi sana unajianda kwenda skuli umejipaka rays huna shida na mtu
Kama hilo tangazo lilikuwa linakukuta nyumban bas ww ulikuwa unachapwa namba maana lilikuwa linawejwa 7:20 weekdays au ulikuwa dalasa la 2
 
Mambo vipi wanajamii.
Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.
Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba" .
Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini

[HASHTAG]#mckonjetv[/HASHTAG]
Kutumia kibuku ni pombe bora. Lilikuwa ni tangazo la biashara katika kipindi cha mchezo wa redio RTD
 
Umenikumbusha tangazo la rosheni ya JAMBO kuna jambo kubwa,jambo ndogo na JAMBO KATIKATI[huyu ndo alikua ananifurahisha]
Haha ata mim nlitaka kusema hvyo nlikua nalipenda sana ili tangazo
 
Hah hah hah hah, pole sana mkuu. Mimi nilikuwa silali mpaka nimsikie mzee Jangala na mwanae Mshamu
Hata mm nlikuwa natama nakaa had saa 3 na nusu alafu 3minutes letter nakuwa nakoloma ila nakuwa walau nmesikia sauti ya mzee mundu
 
Wanafunzi walioomba kujiunga na Elimu ya Juu wengi wamekosa nafasi.. Halafu unatuletea habari za Chai Jaba
Kwani lazima kila mtu asome? Waliosoma wenyewe hawahitajiki, wapo kibao watatosha. Mi nilidhani unasema wote wenye sifa wamenyimwa nafasi.
 
Sanifu.
Kuna akina Tolu Mnyama, Bingwa wa Rivasi.
Sanifu gazeti pendwa sana enzi zile, hasa kwa watu tuliokataa kukua.
Kulikuwa na wachoraji mahiri kama Oscar Makoye (Tolu), Nathan Mpangala (kijast); Fadhil Mohamed (kabwela); Noah Yongoro, Abdul Kingo, king kinya na wenngine kazaa.
 
National bank of commerce, ndio bank yetu sote ana ni bank ya kisasa ndio bank ilio imara.
Kidogo kidogo hujaza kibaba, akiba haiozi.
Weka pesa zako na NBC utafaidikaaaa.
Hili pia lilikuwa kinaletwa katika kipindi cha mchezo wa redio pamoja lile la chibuku.
 
Kuna lile la redio tanzania,ilikiwa asubuh utasikia jambo...sijambo jirani,hamjambo africa mashariki hatujambo...saaafi sana unajianda kwenda skuli umejipaka rays huna shida na mtu
Ha ha haaaaa.
Umenikumbusha na kipinda cha majira. Na lile ziki lake.
Time hizo nakatiza mitaa kuelekea shule.
Nafkiri kilikuwa kinaletwa saa moja na nusu.
Ila sio siri, nime miss zile old days. I wish i cud go back.
 
huu uzi umejaa udhalilishaji wa midomo ya watu...........mkila bun mnalialia
 
Back
Top Bottom