Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
Kabla ya egoli lilikuwa linapigwa tangazo la huyu mdada[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kikombeee cha urafikiiiiiiii [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
kuna tangazo moja la condom, lilinifanya nipigwe kofi na bimkubwa sitokuja sahau, lilikuwa jamaa anatembea kwenye mvua anafunika mpenzi wake na koti halaf kuna wimbo fulan mzurii mwishoni nikamalizia "kama kweli unampenda utamlinda!" bwana weee lilekofi nalikumbuka hadi kesho
 
[emoji23][emoji23][emoji23] chaiiii jabaaaa embu tuwasikilizeee mama lisheeeee .....yenye harufu nzuri yenye nguvu kuliko zote...chai jabaaa...kikombeee cha marafikiii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kuna tangazo moja la condom, lilinifanya nipigwe kofi na bimkubwa sitokuja sahau, lilikuwa jamaa anatembea kwenye mvua anafunika mpenzi wake na koti halaf kuna wimbo fulan mzurii mwishoni nikamalizia "kama kweli unampenda utamlinda!" bwana weee lilekofi nalikumbuka hadi kesho
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nani bingwa bingwa anaingia bingwa mkaribishe bingwa anaingia bingwa. Lilikuwa tangazo la bia maarufu kwa kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi.
 
Translation " baba yake chale ana viraka viwili vinaulizana umekuja lini, nimekuja Jana nikashinda leoooooooo" kale ka beat ya wimbo kipindi cha michezo RTD sijui kama kale ka beat bado kapo
Kale ka beat huwezi amini ninacho na ndio ringtone ya simu yangu..kila nkipigiwa simu naona wazee wananiangalia[emoji3] [emoji28] [emoji3] na kale ka Majira ninacho pia
 
Maumivu ya kichwa huanza taratiibu, kama mtu anagonga nyundo............
Hili lilikua tangazo la Action dawa ya maumivu enzi za RTD
Action..dawa bora kutoka beta health care..Maumivu yakizidi muone daktari!!
 
Back
Top Bottom