Mambo vipi wanajamii.
Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.
Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.
Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
mkuu hilo tangazo la revola lilikuwa na version tatu ila version hadi tukawa tunasema ni mtoto wa mengi au wengne tulikuwa tunasema ni kiwete 7bu alikuwa kakaa chini lipo hivi
jamaa:"ngozi yako ni laini na nyololo"
demu:" mmh kama halili"
jamaa: "hakika ww unatumia REVOLA"
demu: "ni kweliii"
halafu kina kuja kimziki
[emoji445] tuliliiiiiii[emoji445]
halafu kuna jingne kacheza MILIAM ODEMBA linasema
"kuwa na ngozi zuri haitokani na VIPODOZI ghalii( hapo tunaoneshwa dresing table imejaa vipodozi vya ukwelu)
jamaa anaendelea
"siri ni moja tu zingatia
kura vizuri(tunaoneshwa matunda ya ukweli)
kulala vizuri
(tunoneshwa ODEMBA kalala katika kitanda cha ukweli)
kushiriki katika mazoezi mara kwa mara(tunaoneshwa ODEMBA anapiga tiz)
kisha hapo safisha ngozi yako na sabuni yenye mafuta ya kurahinisha MWILI sabuni ya REVOLA
ila matangazo ambayo nimeyamis ni mawiri moja la kideo la SAFARI NI SAFARI inaoneshwa Kisoda cha bia ya Safari kinasafili sehemu mbalimbali kea njia tofauti
Scene yake hipo hivi linaanzia bar inafunguliwa BIA halafu kisoda (tulizoea hivyo ila jina halisi ni kizibo) kinanadondojjea katika kreti janaa anabeba abaweka katika gari basi hapo safari ndo inaanza kinadondoka katika maji mmasai anakiokota anaweka katika kiatu chake anavuka barabara kinadondoka kinanasia katika tairi la gari yaan lilijuwa linanipa burudani sana
[emoji445] safari ni safari iwe mchana au usiku kiangazi au masika safari ni safari[emoji445]
jingine ni la radio la fanta hasa radio one
fredy mbahiri anafika anawaambia "AISEE AISEE inakuaje washikaji"
unapigwa mchango wa kununua fanta KUBWA wenzia wanachanga ye anatoa shi 10 sijui vile yaan hana kitu hadi wenzake wanaguna "aaaah frediii "hili nimelisahau kidogo maneno yake anayekumbuka anipe mistari yake
kuna baada ya kazi ni wakati wa TUSKER laga
na moja la SWEETMETHOR (Sigara SM) hilo ni tangazo la kwanza la SIGARA LA VIDEO tz enzi hizo CTN baadae DTV tgen ITV jamaa yupo katika mbuga ya wanyama yaan SCENE yake nimeisahau kidogo
kuna la rangi ya goodstar zebwera na mashaka
mashaka : kijanaa nimepata wapangaji wanaonilipa kodi nyingi zaidii
kwahiyo ni lazima uhameee
zembwera: MZEE nimepaka rangi nyumbaaa
bazi mpaka anazeeka rangi haipauki teh