Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mbona uzi mzima hakuna video wala audio za hayo matangazo au ni kwamba hayaruhusiwi humu?
 
Kuna tangazo la bia ya tusker aliimba T.I.D sijui yule, nalitafuta sana. Nikilipata ntaliweka hata ringtone. Achana na lile la wakenya
[emoji445]Nikufananishe kama jabaliiii..... Majirani zetu wanashangiliaa....... Oh oooh mimi na wewe milele ...... Wingi na umoja wetuuu...... Tu marafiki halisi..... Bia boraaaaa Tusker, Tumarafiiiiiki halisi [emoji445]... Sauti ya TID ile alitisha sana.

Mwenye haka kanyimbo atuwekee humu ndani
 
Screenshot_20220520-074658.jpg
 
Twende pamojaaaa...... bega kwa begaaa.....
Marafiki wa kweliii.........
Nadhani ni tangazo la TTCL kama sijakosea.
 
Tangazo moja Ka soda ya fanta,liliimba
Oooooh kaluvale,na Luna jingine LA bamboocha jamaa anakunywa coca alafu anasisimuka ghriiiiiiuu.
 
Bila kuwasahau maharamia Zumo na Mzee Ole...! Sijui ana Mzee Ole ana undugu na 7ya [emoji5]
Nilikuwa namkubali sana Zumo... Mzee wa kupiga miwani tinted... Na tisheti kali, anachomekea kwenye jinzi... Lile gazeti nimelimisi sana.
 
Wanafunzi walioomba kujiunga na Elimu ya Juu wengi wamekosa nafasi.. Halafu unatuletea habari za Chai Jaba

Yeye anahusikaje kwenye wao kukosa nafasi?
Pili ni nini unaweza fanya ama ulichofanya kuhakikisha wanapata nafasi?
Punguza jazba
 
Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
Jambo ndogo,jambo kubwa na jambo katikati

Sent from my SAMSUNG-SM-J327A using JamiiForums mobile app
 
Nitaweka ninayo yakumbuka.

1. Bingwa ameingia bingwa nani bingwaa.. Tangazo la bia.

2. Chibuku hoyee hongera hongeraa chibuku hoyee hongeeera.

3. TTCL simu kwa maendeleo, huduma bora na nzuri kwa wateja wetu kwa matokeo mzuri...

4. Safari asili yake nchini Tanzania safari moja huanzisha nyingine, safari ni safari iwe kwa miguu ama kwa basi safari ni safari

5. Usione soo sema naye kuhusu kusubiri kuwa mwaminifu au kitumia Condom. ISHI.

Mhenga mwenzenu.
 
1. Chai bora kilele cha ubora, ni chaguo la watanzania….
2. Mzee nimepaka rangi nyumba, naomba univumilie mpaka hii rangi itakapochujuka,
3. Amani ni sabuni safi amani ni sabuni bora!
4. Coral paints ya kisasa. Rangi ya kujivunia….(kwanza tupambe na kisha tusherekee….)
5. Kah we ni mdhembe….
6.tunasonga mbele kwa umoja, mafanikio yetu ya pamoja miaka kumi ya kuhudumia wateja wetu wa Tanzania….
7. Dum dum du dud du dum du
8. Sweetheart ni lotion yako mwanadada…
9. Una mpango wa kuondoka leo? Hapana shaka baba…..
10. Ni fresh ni poa ni yako…….
11. Liki hill hotel ……
12. Tangazo la scandnavia nasahau maneno
13. Mimi ni daktari wenu wa meno hapa nyumbani na nimevaa koti jipya…. Hiyo ngumu tudokeze basi
 
Back
Top Bottom