May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Waswahili wana usemi '"Jasiri haachi asili" hivyo wanachopitia Simba kwa sasa kupitia aliyekuwa anafanya kazi hapo ni fundisho tosha kuwa mkae nae kwa tahadhari kwani si Mtu wa staha.
Mtu aliye tayari mpoteze yote mliyofikia kwa kuwa tu maslahi yake yamevurugika ni Mtu Mbaya na Msaliti.
Manara sasa ameonesha rangi zake halisi, kwamba kwake maslahi yake ni muhimu kuliko ya kundi, hata kama aliwahi kuwaaminisha Wanakikundi Wenzake kuwa yeye ni Mwenzao wa kufa na kuzikana.
Kama Manara alituhumiwa na Wenzake kuwa 'anaropoka' siri za kambi kwa Wapinzani...kwa anayofanya sasa bado anataka tuamini kuwa alikuwa anasingiziwa?
Simaanishi kuwa Manara hakukosewa au hakupitia maudhi ya hapa na pale ndani ya Simba, lakini ni vipi Askari akiamua kutoka hadharani kuanza kuropoka kila yanayomkuta kwenye kambi yake?
Au Muajiriwa aanze kuropoka mapungufu ya Kampuni/Taasisi aliyokuwa anafanya nayo kazi kabla?...huenda kwa wakati huo kama Mshindani/Mpinzani utafurahia kusikia...lakini kama una akili lazima utabaki na maswali "je mimi nitakuwa salama kuwa karibu na Mtu kama huyu?"
Anachokifanya Manara ni dhahiri kuwa kwa sasa hajali tena nini kitatokea kwa Simba. Kama ana ugomvi na Moo hivi kuna haja gani kutamani kuwasumbua wote wanaoifuatilia na kupenda mafanikio ya Simba?
Mnapokuwa katikati ya kusheherekea matunda/mafanikio ya kazi Mtu pekee mnayemtarajia aje awavurugie sherehe yenu ni yule ambaye siku zote anapingana nanyi na hapendi mafanikio yenu, na si yule aliye/anayewaaminisha siku zote kuwa ni sehemu yenu .