Mnaofikiria kufanya kazi na Manara baada ya haya mjiulize mara mbili. Anachowafanyia Simba nanyi atawafanyia

Matajiri wanyonyaji waache wawekwe hadharani janja zao ili likitokea la kutokea msiseme hamkuambiwa
 
Sio mbaya mtu anapojilipua kwa kusema ukweli...the guy is free now kwa kusema ukweli na ni bora zaidi kuliko kwenda kuongelea vitu hivi pembeni,faida yake mabosi wake wa sasa wata mheshimu
We mwenyewe unajua kwa bakhresa hakunaga malalamiko na kesi za kijinga na wafanyakazi wake,watu wanalipwa on time kuanzi kwenye timu,media na watu wa viwandani lkn hapo nyuma nakumbuka kuna wafanyakazi washawahi kulalamika Mo anawanyonya kwa kulipa kiduchu kuliko kazi wanazofanya.
 
Haji kala mamilioni ya Ghalib sana kuihujumu Simba.
 
Haji anaweza kuwa kakosea kwenye baadhi ya kauli zake ila kilichomuuma zaidi ni kuambiwa kuwa anaihujumu team anayaoipenda.

Root cause ya hasira za Haji zilianza kwa kuambiwa kuwa anaihujumu team, kama ni maslahi mbona kayavumilia kwa miaka 6?
Kwa mwenendo na kauli zake hizi ni dhahiri alikuwa anaihujumu Simba kwani alikuwa anafanya kazi kwa kinyongo muda wote,hivyo njia aliyoona inafaa kulipa kisasi ni kuwa double agent.
 
Kwa mwenendo na kauli zake hizi ni dhahiri alikuwa anaihujumu Simba kwani alikuwa anafanya kazi kwa kinyongo muda wote,hivyo njia aliyoona inafaa kulipa kisasi ni kuwa double agent.
Umehukumu kwa kutumia sababu nyepesi sana,kwani haiwezekani kua Haji alikua anavumilia ili tu kulinda umaarufu wake na kupiga hela kwenye page zake za social media?

Ni dhahiri kabisa kua Haji alikua anapiga pesa zaidi kwa kutumia umaarufu wake alioupata Simba kwenye matangazo ya biashara kuliko pesa aliyokua anaipata kama mshahara.
 
Eti Bakheresa nini na wafanyakazi wake. We kaa kimya kabisa. Nenda kapekuwe mafaili pale CMA karibu na CBE. Usilolijua usilizungumzie kabisa. Kwa kifupi watu wengi waelewa wakiachishwa kazi huwa wanaenda kuwashtaki waajiri wao pale mahakama ya kazi na wanamalizana hukohuko na sio kuitisha waandishi wa habari kama huyo bumunda wenu mnayemtetea kwa nguvu zote. Hebu fikiria kila anayeachishwa kazi kwa utata aitishe "press" hivi hii nchi ingekuwaje.

Kimsingi jamaa ni "zero" kichwani tena ile ya darasa la kwanza ambayo walimu huwa wanaingozea masikio. Hajui kipi cha kuwasilisha kwa waandishi wa habari, hajui kipi cha kupeleka TCRA na polisi tena kimya kimya na pia hajui kipi cha kuacha kuzungumzia hadharani ili kisimuharibie kwenye kazi zake huko mbele ya safari. Jamaa yenu huyo hata siri za medani hajui ni zipi ambazo hufichwa mpaka kifo yeye yote anabeba kwenye kapu anaweka hadaharani dunia ijionee na kusikia.
 
Binaadamu tunajisahau sana.

Haji kanufaika sana kufanya kazi Simba hata kama asingekuwa analipwa ingawa yeye anaangalia upande mmoja tu wa yeye kuitumikia timu.

Ila kwa sasa hayo yote hayapo kichwani kwake...labda tu hao wanaomrubuni sasa watamfadhili lakini akiachwa kidogo apigwe na njaa akili itamkaa sawa.
 
Manara amepata umaarufu kupitia uwekezaji na jitihada za Mo. Halafu anautumia umaarufu huo kutangaza bidhaa za wafadhili wa Yanga. So unfair
 
MANARA alikuwa MWAJIRIWA wa SIMBA SC na sio MeTL
Manara amepata umaarufu kupitia uwekezaji na jitihada za Mo. Halafu anautumia umaarufu huo kutangaza bidhaa za wafadhili wa Yanga. So unfair
 
Haji anaweza kuwa kakosea kwenye baadhi ya kauli zake ila kilichomuuma zaidi ni kuambiwa kuwa anaihujumu team anayaoipenda.

Root cause ya hasira za Haji zilianza kwa kuambiwa kuwa anaihujumu team, kama ni maslahi mbona kayavumilia kwa miaka 6?
Sasa kwa kwenye akili wanaweza wakakubali kua alikua anaihujumu timu kwa alichofanya
Kwa sababu unapotaka timu unayosema unanipenda ichafuke kwa sababu zako binafsi au umetumwa huko ndio kuihujumu. Hakuna asiyejua mchango wake kwa simba, sasa unataka kuharibu mema yote
 
Partner ajirekebishe kwasababu ameweka fedha wakati mwengine tukubali kwamba C.E.O ni mwajiriwa kama alivyokua Manara wakati wake ukifika nae ataachia ngazi tu!!..Mo akiondoka Simba Leo hata akiwaachia kila kitu bado Simba itadondoka!!..Manara kapotea njia kwasababu alidhani Mo hatoweka fedha kabla ya press yake ndio maana kabla ya game ya kigoma alisema mchakato wa Simba hautofika mwisho!!...Manara analia hajui anaelekea wapi?!!..kaacha team wakati wa mafanikio ni mjinga pekee ataendelea kumsikiliza Manara
 
Historia yake inajulikana wazi
 
ona mwingine huyu. huwa mnawezaje kujiunga JF kwa akili hizi? kwa hiyo Kaduguda anatoa uhalali wa kila mtu kutofanya busara? Wengi mnatetea huu ujinga kishabiki sana badala ya kuiona future ya mtu. Hivi ni mwajiri gani aliye malaika atamwajiri Haji,au mfanyabiashara gani timamu atafanya biashara na huyu. ambaye hatokuwa na uhakika wa siri za biashara zao kuvuja
 
Mbumbumbu fc mshasahau kuwa mlipomtimua Kaduguda aliongea mbovu na kudai hela zake za maandazi na mihogo aliyokuwa anawanunulia wachezaji pia akidai cone zake za mazoezi,lakini leo hii yupo Simba kama kiongozi. Na Manara atarudi tuu.
Angerudi kwenye Simba ile ya kina Mzee Mpili na Simba hii ya Kidigitali.
 
Swadakta wa swadakta.
 
Simple tu, wasimwonee. Hilo ndilo la kilichukua. Watanzania tumejaa unafiki halafu tunasema ni ethics.
Manara ameweka nyeusi na nyeupe, hajamwonea mtu.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kama wana makandokando ya ajabu ,tutamshukuru Manara akiwaanika peupe. Tunaowatahadharisha hawa watu tunapata nini?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…