Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Siioni faida yoyote ile ya Balua kuchezeshwa upande wa kulia.
 
Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?
Huwa wanafanya hivyo mtu anatumia mguu wa kushoto halafu anacheza winga ya kilia ili muda fulani aweze kuingia ndani ya uwanja na kuweza kupita hata mashuti kama alivyokuwa anafanya Ruben.

Kitu nachokiona kwa hawa wachezaji wa sasa mfano Balua, ni uwezo mdogo wa kuinufaisha timu kwa kutokea winga ya kulia kwa mguu wa kushoto. Ruben alikuwa ana uwezo sana na ikitokea amebribo akitandika shuti golini makipa walikuwa hawadaki.
 
Back
Top Bottom