Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Mimi ninakaa Wilaya ya Ilala. Jana nilikuwa Wilaya ya Temeke nilishuhudia mida ya mchana badala ya mama kuwapikia watoto (watoto walitoka kucheza wakaja kulalamika njaa inawauma) akawapa 500 wote wawili wakanunue bagia na askrimu (ice cream) na ndio imetoka hiyo mpaka Usiku, kulingana na maelezo ya mwenyeji wangu. Sema na mimi nilikuwa majalala, nilibakiwa na nauli tu 2,000, laiti kama ningekuwa na kitu chochote ningeweza kuwaongezea hata 500 nyingine aisee.

Kama hauna pesa ya kumsaidia mtoto masikini, basi mkumbuke hata wakati wa sala au swala.

Daah, uswahilini panatisha wadau, hususan kwa watoto wadogo.
Polee sana mkuu nakuelewa ulivyo jisikia ili urudi tena ukasaidie hao vijana.... mtaani kwenu na washkaji zako azisha kampeni ya michango then mnaenda kusidia hao vijana! Bdo unaweza kuwa msaada kwao
 
Sisi wengine tuliokulia vijijini tulikuwa hatupati hata hizo Aisklim! Unakomaa na njaa tangu asubuhi mpaka usiku.
Lakini tulikua mpaka tukatoka kimaisha.
Hata hivyo nakupongeza kwa moyo huo wa huruma! Barikiwa.
 
No matter unakaa TMK au Ilala ila kitendo cha OP kukosa hata 500 ya ziada mfukoni kulikuwa hamna haja ya kuanzisha huu uzi 😅🚮🚮

Wait, una uhakika hayo machozi yalikutoka kwaajili ya hao watoto kweli?? 😂

Kwamba jamaa anastress so katafuta tukio la kushusha mavitu kichwani mwake? 😭🤣🤣🤣
 
No matter unakaa TMK au Ilala ila kitendo cha OP kukosa hata 500 ya ziada mfukoni kulikuwa hamna haja ya kuanzisha huu uzi 😅🚮🚮

Wait, una uhakika hayo machozi yalikutoka kwaajili ya hao watoto kweli?? 😂
Machozi ya kujihurumia endapo akikuta konda anasema route za usiki 2500
 
Polee sana mkuu nakuelewa ulivyo jisikia ili urudi tena ukasaidie hao vijana.... mtaani kwenu na washkaji zako azisha kampeni ya michango then mnaenda kusidia hao vijana! Bdo unaweza kuwa msaada kwao
Niliogopa kuomba michango humu JF kwa sababu watu wangedhania kwa mimi ni tapeli..
 
Sisi wengine tuliokulia vijijini tulikuwa hatupati hata hizo Aisklim! Unakomaa na njaa tangu asubuhi mpaka usiku.
Lakini tulikua mpaka tukatoka kimaisha.
Hata hivyo nakupongeza kwa moyo huo wa huruma! Barikiwa.
Thanks 👍
 
Kama hakuna wanachokuja kufanya hapa duniani ni heri usiwalete maana faida za kua na watoto ni chache kuliko hasara za kua nao
 
Wewe unayeishi Ilala na hao wanaoishi Temeke tofauti yenu ni nini ikiwa mwanaume mzima ulibakiwa na nauli tu? Kisha unaleta masimango humu ilimladi tu uonekane umeanzisha uzi?
We ndio huyo mama aliyetoa 500 kwa watoto wake nini maana si kwa makasiriko hayo😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom