Mnaomshauri Rais juu ya Ikulu mpya Chamwino muogopeni Mungu

Mnaomshauri Rais juu ya Ikulu mpya Chamwino muogopeni Mungu

Wewe kipaombele umeona ni nini?
Hali duni ya jamii kiujumla, elimu, afya, nishati, barabara, maji, ajira, mishahara na maslahi duni ya watumishi, kilimo, mifugo, ufukara wa kipato kwa wananchi walio wengi..........na hayo ni kwa uchache sana.
 
Habari nzima ya kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma ni white elephant project, si Ikulu tu.

Tumetatua tatizo ambalo hatuna, wakati matatizo ambayo hatuna hatujayatatua.
Watavunga kutolitambua hili, serikali haikuwa na tatizo la ukosefu wa makao makuu achilia mbali jengo la ikulu. Lakini yametumika matrilioni kutatua tatizo lisilokuwepo huku nchi ikikabiliwa na changamoto lukuki hadi kila kukicha tunachukua mikopo. Kama unaweza kutumia matrilioni kufanya anasa ya kutatua shida isiyokuwepo, inakuwaje tena kwenda kuomba mikopo.​
 
Jamani ikulu zote dunia zinahitajika kuwa self sufficient kwa mahitaji yote muhimu. Kumbi za mikutano, migahawa au hoteli kwa ajili ya wafanyakazi, makazi ya rais na wafanyakazi muhimu ambao ni wasaidizi wa rais, kwa kutaja kwa uchache!

Ikulu ni taasisi inayojitosheleza kwa kila kitu katika kuendesha nchi na kufanya maamuzi.
Unataka kumdanganya nani? Kwani tumeanza kuwa na ikulu jana? Mbona ya Dar haina hayo makando kando? Tazama ikulu nyingi hata za majirani zetu utajua namna unavyojua hujui au unataka kudanganya. Ikulu inaendeshwa kwa kodi zetu.
 
Tatizo la Tanzania ni ubinafsi watu wanaonekana wapole ila ni wabinafsi na waliojaa chuki.

Mtu anatakaa yeye tu na familia yake ndio wanufaike na keki ya Taifa.

Hakuna jambo linafanyika kuwaondolea umaskini watu wa chini.

Watawala mara zote wanahakikisha maskini wenye matatizo wanaendelea kuwepo ili wapate wa kuwatawala ni woga tu usiokua na maana yeyote.

Viongozi wetu wapo tayari kushirikiana hata na watu wa nje kukandamiza wenzao ili tu wabakie katika madaraja ya juu kimaisha waendelee kutawala.

Nchi haitapata maendeleo ya kweli kamwe kama viongozi hawataacha ubinafsi na tamaa jambo ambalo ni gumu kutekelezeka.
 
Hali duni ya jamii kiujumla, elimu, afya, nishati, barabara, maji, ajira, mishahara na maslahi duni ya watumishi, kilimo, mifugo, ufukara wa kipato kwa wananchi walio wengi..........na hayo ni kwa uchache sana.
Kwaiyo tusijenge makazi yoyote mpaka tuyatatue hayo?
 
Projects za kifisadi hizo mkuu viongozi wa Afrika wanawaza kuiba tu na sio kutatua changamoto za wananchi

Adui mkubwa wa taifa hili ni viongozi wa chama Cha mboga mboga
Waliona kuwa eneo lililotengewa Ikulu ni kubwa sana hivyo ili kusogeza Usifsadi karibu na Ikulu, wakaamua kuweka vimiradi hivyo kusudi iwe ni rahisi kwa wapiga dili kuingia Ikulu.
 
Kwaiyo tusijenge makazi yoyote mpaka tuyatatue hayo?
Serikali haikuwa na tatizo la makao makuu ya wizara wala ikulu, kwa nini utatue tatizo lsilokuwepo badala ya kukabiliana na changamoto lukuki zilizokuwepo na hata kwenda kukopa pesa!?
 
Projects za kifisadi hizo mkuu viongozi wa Afrika wanawaza kuiba tu na sio kutatua changamoto za wananchi

Adui mkubwa wa taifa hili ni viongozi wa chama Cha mboga mboga
Wajeruman waliweka Boma milimani. Mfano Morogoro na Mahenge.. Dar Gavana akaweka ufukweni badala ya UDSM au Makongo wapate uharaka wa kuondokea baharini. Dodoma ilitakiwa iwe kule kwa Waziri Mkuu au Mzakwe, au juu njia ya Mvumi?. Ila msiogope technologia ya sasa ni kubwa, ulinzi ni high tech, electronic etc.
 
Projects za kifisadi hizo mkuu viongozi wa Afrika wanawaza kuiba tu na sio kutatua changamoto za wananchi

Adui mkubwa wa taifa hili ni viongozi wa chama Cha mboga mboga
Muonekano safi. Ila design yenyewe ni kama enzi za Germanyii vile, maboma ya Waisraeli ambopo mizinga ya kivita iliwekwa juu like Fort Jesus ya Mombasa?, I expected contemporary sort of design, non flashy, eco/environmentally friendly. Kwa vumbi la Idodomia vs. rangi nyeupe watapiga rangi kila mwaka.
 
Hivi na yeye akujua alichoongea si kitu kizuri hadi aseme public

Kasuku style....
Hadithi ile ya mfalme mkali aliyeshonewa nguo isiyoonekana(transparent).
Kila chawa na mpambe akawa anamsifia kuwa amependeza sana-kwa kuogopa kukatwa kichwa na mfalme.

Hilo liliendelea hadi akatoka nje ya kasri.
Mtoto mdogo aka piga kelele "Mfalme yuo uchi, mfalme yuko uchi"
Baada ya hapo kila mpambe akatafuta uchochoro wa kutokea!
 
Rais anawasikiliza wahuni. Wao wanachojua ni kuzua kandarasi ili wale cha juu na commission. Hata white house marekani haina uwanja wa ndege. Sasa majengo ya zanzibar jengo la EAC ndani ya ikulu ya nini yote? Kuna mji wa serikali sasa mji wa ikulu wa nini tena🤣😂
Kwanza uwanja wa ndege ikulu unaweza kua sio sawa kwa usalama
 
Hadithi ile ya mfalme mkali aliyeshonewa nguo isiyoonekana(transparent).
Kila chawa na mpambe akawa anamsifia kuwa amependeza sana-kwa kuogopa kukatwa kichwa na mfalme.

Hilo liliendelea hadi akatoka nje ya kasri.
Mtoto mdogo aka piga kelele "Mfalme yuo uchi, mfalme yuko uchi"
Baada ya hapo kila mpambe akatafuta uchochoro wa kutokea!
Mkuu hii story ni kama kitabu Cha Kaptula la Marx ambapo rais kapera na wapambe wake walikuwa wakimsifia lakini Tarishi alimwambia ukweli bila kupepesa macho jambo ambalo lilifanya waziri mmoja kumwambia Tarishi kwamba

"Katika bara hili ni mwiko kusema ukweli"mwisho wa nukuu
 
Nilijua watatenga eneo kubwa liwe kwa umbali kidogo na ikulu waweke mbuga ndogo wafuge pundamilia, twiga, swala, na wanyama wengine wadogowadogo rafiki ili iwe kama kivutio cha utalii na zaidi palepale waweke militarry base sasa niliposikia mambo ya complex, mara Malls nikajua tayari viongozi wetu ile kauli ya ikulu ni mahala patakatifu ya Nyerere hawaikumbuki tena
 
Labda nimeelewa vibaya kuwa eneo la Ikulu ni kubwa mno
Sidhani huo ukumbi utakuwa karibu na Ikulu

Kwanza mjue eneo la Ikulu ni ukubwa gani ndio muanzie hapo
Nasubiri wa karibu hapo
Una hoja ,usikilizwe.

Eneo la ikulu DODOMA ni kubwa sana, hayo Majengo ya ziada yanaweza kuwa hata several kilometers from the residence .

Sasa mjiulize, pale ikulu ya DSM,kumbi za mikutano na Majengo mengine yako umbali gani?
 
Back
Top Bottom