Mnaomsikiliza Lissu kwenye wimbi la 255 CHADEMA je, anahimiza jamii na vijana kufanya kazi?

Umeelewa nilichoandika lakini au umekimbilia kuangalia nilipoandika jina Lisu na wewe uka quote na ku comment?

Nimekwambia mikataba ipo.., nikakupa mfano wa Msumbiji kuhusu gesi, au Congo kuwa wana utajiri wa madini na tayari wana mikataba na wazungu, lkn mikataba hiyo haizuii wazungu kutafuta watu aina ya Lisu ambao wanapigania matumbo yao kuwa set kuanzisha chokochoko ili waweze kuiba kupitia mgongo wa vita au machafuko ya kisiasa.

Leo hii hata akitokea raisi ambae atakuwa na nia ya dhati ya kupambana na mikataba hiyo mibovu nina imani 100% kuwa Lisu hatofurahishwa na hilo, bali atatafuta njia ya kumkwamisha huyo raisi kupitia hao hao wazungu walioingia mikataba na nchi yetu.

Najua kila mwanasiasa Tanzania au Duniani ni muongo, lkn toka mwaka 2015 hadi leo Lisu ameweza kuonekana kuwa ni muongo wa wazi wazi kabisa. I mean yuko tayari kuongea uongo hata mbele ya watu ilimradi awe na uhakika wa chochote mfukoni mwake.

So kwa vile yupo nje ya serikali basi anaweza kutumika kuanzisha kile ambacho wazungu watakitumia kama kichaka kuingia kuiba kama wanavyoiba huko Congo, Msumbiji, Sudan nk.
 

..tunakosea kumtegemea Raisi kwa kila jambo.


..kama makampuni ya nje ya madini yanatunyonya tunaweza kupitia wawakilishi wetu, WABUNGE, kutunga sheria zinazozuia unyonyaji huo, au kupiga marufuku makampuni ya kigeni kujihusisha na sekta ya madini.

..Na kwa bahati nzuri sasa hivi tuna Bunge la chama kimoja, CCM, kwa hiyo hakuna tena kisingizio cha kukwamisha au kupingwa na wapinzani.
 
..Lissu anahimiza wananchi kufanya kazi.

..anahimiza mfumo bora wa kodi, ushuru, na tozo, ambao utachochea kilimo, ufugaji, biashara, na uchumi kwa ujumla wake.

..anakemea wizi, ubadhirifu, na matumizi mabaya ya fedha za umma, mambo yanayorudisha nyuma maendeleo, na kukatisha tamaa wananchi kufanya kazi.
 

Nimekupa mifano halisi kwa Tanzania, acha kunipa mifano ya congo na Msumbiji ambako huna uelewa nako boss. Raslimali zote hapa nchini zinavunwa na hao hao wazungu. Je kuna machafuko gani hapa nchini hadi hao wazungu wavune raslimali zetu? Kama hiyo mikataba ina tija kwa nchi zaidi ya viongozi, kwanini haipelekwi bungeni ikaonekana uhalali wa hiyo mikataba?

Jitahidi kutoa mifano yenye uhalisia, unamlaumu Lisu kuwa anataka kutumika na wazungu, lakini ubovu wa mikataba hutoi ya hapa nchini, unatoa sijui ya Congo, Msumbiji nk. Narudia tena, kama raslimali zetu ambazo wazungu wanataka kuziiba kupitia kwa Lisu ni za maana hivyo, kwanini hazimalizi huu umasikini, badala yake mnatuwekea Matozo yasiyo na maana?

Kwani 2015 hadi sasa kuna mikataba gani ya raslimali iliwahi kuwekwa wazi kwa wananchi, hadi huo uongo wa Lisu uonekane? Zaidi ya propaganda ni wapi uliona mikataba ya hizo raslimali? Au unadhani hatujui Lisu alikuwa anaongea nini kipindi cha yule mlevi wa madaraka? Na propaganda zilikuwa zipi?
 
Angeanza kwanza kutumia nguvu hizi kwa chama chake kwanza ili kuonesha mfano wa kile anachosimamia.

Tukiachana na yale mamilioni ya shilingi waliokuwa wanakatwa wabunge na chama chake toka 2015 hadi, pia tukiachana na mamilioni ya ruzuku ambayo chama chake kilikuwa kinapokea kutoka serikalini, kuna zile M100 zilizotolewa na Sabodo kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya chama ambazo ziliingia katika mifuko ya wajanja wachache hadi kupelekea makao makuu hayo kutojengwa mpaka leo.

Afu bado kuna mtu anaamini kwamba Lisu na hawa wanasiasa wengine wana nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
hizo agenda n za ccm,mpaka muhimizwe ndo mufanye kazi ccm ni laana kwa taifa
 

..wanasema mganga hajigangi.

..walioko nje ya chadema wanaweza kufuatilia hayo uliyoyasema.

..Na walioko ndani ya chadema watafuatilia ubadhirifu na ufujaji unaofanywa na serikali na Ccm.
 
..wanasema mganga hajigangi.

..walioko nje ya chadema wanaweza kufuatilia hayo uliyoyasema.

..Na walioko ndani ya chadema watafuatilia ubadhirifu na ufujaji unaofanywa na serikali na Ccm.
Hapa umeongea kweli bila kulalia upande wowote.
 
Sasa katika kushughulikia haya matatizo aliyobainisha CAG, Lissu anashauri nini kifanyike kwa Sasa na Hata hapo Baadaye!!! ?
Yaani hujui hata maana ya katiba? Hivi unaweza kushughulika vipi na wezi waliotajwa na CAG bila sheria? Una tofauti gani na yule mpinga ufisadi aliyesema hataki kusafiri kwasababu atapigwa na akaacha hata ile sheria ya PCCB bila hata kuigisa?
Wewe unaamini huko tuendako hapata tokea wenye vyeti feki kwakuwa waliondolewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…