Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Umeelewa nilichoandika lakini au umekimbilia kuangalia nilipoandika jina Lisu na wewe uka quote na ku comment?Leo hii kwenye nchi yetu tunaona makampuni ya wazungu yakivuna raslimali zetu na Tundu Lisu bado hajachukua madaraka, je hawa wazungu wanamtumia nani hadi sasa? Je ni raslimali gani tunazo, wakati hadi leo bado nchi yetu ni masikini hivi? Kama tuna rasilimali nyingi hivyo hadi wazungu wanataka kumtumia Lisu kuzichukua, kwanini msiuze hizo, badala yake mnatuwekea Matozo ya kipuuzi? Ila nyie wazee propaganda mfu za CCM naona zimewapumbaza vibaya.
Nimekwambia mikataba ipo.., nikakupa mfano wa Msumbiji kuhusu gesi, au Congo kuwa wana utajiri wa madini na tayari wana mikataba na wazungu, lkn mikataba hiyo haizuii wazungu kutafuta watu aina ya Lisu ambao wanapigania matumbo yao kuwa set kuanzisha chokochoko ili waweze kuiba kupitia mgongo wa vita au machafuko ya kisiasa.
Leo hii hata akitokea raisi ambae atakuwa na nia ya dhati ya kupambana na mikataba hiyo mibovu nina imani 100% kuwa Lisu hatofurahishwa na hilo, bali atatafuta njia ya kumkwamisha huyo raisi kupitia hao hao wazungu walioingia mikataba na nchi yetu.
Najua kila mwanasiasa Tanzania au Duniani ni muongo, lkn toka mwaka 2015 hadi leo Lisu ameweza kuonekana kuwa ni muongo wa wazi wazi kabisa. I mean yuko tayari kuongea uongo hata mbele ya watu ilimradi awe na uhakika wa chochote mfukoni mwake.
So kwa vile yupo nje ya serikali basi anaweza kutumika kuanzisha kile ambacho wazungu watakitumia kama kichaka kuingia kuiba kama wanavyoiba huko Congo, Msumbiji, Sudan nk.