Mnaonaje Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035?

Mnaonaje Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035?

Sura ya Pili, Sehemu ya Kwanza, Ibara za 38, 39 na 40.

Ibara ya 40 (1) na (2)

Kifungu (1)
"Bila kuathiri masharti ya mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho" Siyo kuteuliwa na Katiba.

Kifungu (2)
"Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais"

Mhe. Rais Samia hajachaguliwa, atachaguliwa kwa mara ya kwanza 2025 na hivyo kwa mara ya pili kama atagombea na kushinda 2030 na hivyo kuhitimisha awamu zake 2035.

Bado tunaye sana tu!
Hii mbona inaeleweka Mkuu ana vipindi vya ke viwili 2025 - 2030 and 2030 - 2035 hii haina ubishi.
 
Sisi wa tz hatujielewi,badala ya kulilia taasisi zenye nguvu bado tunataka mtu pia? Hebu tuweni serious bas hata kwa JPM niliwapinga sana,tuheshim katba kujipendekeza hakufai kabisa.
 
KIUTA haifanyi archiving, inachapa nyaraka za serikali tu. Archiving inafanywa na idara ya kuhifadhi nyaraka za serikali. Kwa magazeti yanachapwa na viwanda binafsi vya uchapaji na archiving zake zinafanywa na Shirika la Maktaba ya Taifa. KIUTA pekee ndiyo inachapa gazeti la serikali (government gazette).

Mimi nimefanya kazi uchapaji Na copies Za magazeti Na documents zote zinazochapishwa zinawekwa kwenye archive ya kiwandani.
 
Hivi Znz na Tangayika ipi inafaidi muungano?
Hili swali la kukamatwa waziri mkuu wa Zanzibar Na baraza la mawaziri wake Na kufungwa Tanganyika kabla Muungano liko wazi kabisa. Halihitaji ushahidi wa documents yoyote. Hawa watu walikuwa Na Familia zao , watoto wao ndugu zao majirani nk
Kesi Yao hamna tofauti Na watu wa uamsho. Walipokamatwa Na kupelekwa Tanganyika kila mtu anajua hata mtoto mdogo..
 
Rais wa Tanganyika
Mark this comment, mama hatapita kura za maoni kwahio atahudumu miaka yake mitano.tu atatupwa baharini kwenye kura za maoni, rais mpya atatoka kanda ya ziwa tena.. Nani?! Stay tuned!

Mark this comment.
 
Nachokoza mada.

Wadau mnaonaje kama Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035? Kwa kuwa Rais Samia alichukuwa nafasi yake kufuatia mauti ya mtangulizi wake mwanzo wa safari na kwamba hakukuwa na utaratibu wa mila na desturi ya uchaguzi bali ilikuwa ni kutimiza matakwa ya katiba.


Kiuhalali na kwa haki kwake, anastahili kuwa wa pili nyuma ya Mwl Nyerere kwa kukaa ofisini kwa miaka 15 kwa maana ya miaka aliyopokea kijiti kwa sharti la katiba na ndipo sasa astahili utaratibu wa mila na desturi yetu ya uchaguzi ambapo anaruhusiwa awamu mbili 2025 – 2035?

Nini maarifa yako, tupe maoni kwa vigezo na ushahidi.
Akae mpaka uhai utakapomuondoa.Tunampenda sana Rais wetu
 
Huu ni ufinyi na ukosefu wa oksijeni kwenye ubongo
“If a door is shut, attempts should be made to open it; if it is ajar, it should be pushed until it is wide open. In neither case should the door be blown up at the expense of those inside.”

Julius Kambarage Nyerere, from his Stability and Change in Africa speech given to the University of Toronto, Canada, 2 October 1969. -


Complex Majority (not Simple Majority) of Tanzanians will push the door until H.E. SSH secures for 15 yrs tenure.
 
Katiba inasema awamu zisizozidi mbili kwa uchaguzi, yeye awamu zake mbili za uchaguzi ni 2025-2035, si ni ukweli huu mkuu imhotep?
Kama angekuwa ametumikia miaka pungufu ya mitatu, then sawa ila kwa bahati mbaya magufuri amefariki na kumuachia zaidi ya miaka minne so kikatiba haruhusiwi kugombea zaidi ya mara mbili. Yaani hapa akiingia uchaguzi wa 2025 ndio mwisho wake kugombea hata kama CCM watapendekeza aendelee katiba inakataa kabisa.
 
Nachokoza mada.

Wadau mnaonaje kama Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035? Kwa kuwa Rais Samia alichukuwa nafasi yake kufuatia mauti ya mtangulizi wake mwanzo wa safari na kwamba hakukuwa na utaratibu wa mila na desturi ya uchaguzi bali ilikuwa ni kutimiza matakwa ya katiba.


Kiuhalali na kwa haki kwake, anastahili kuwa wa pili nyuma ya Mwl Nyerere kwa kukaa ofisini kwa miaka 15 kwa maana ya miaka aliyopokea kijiti kwa sharti la katiba na ndipo sasa astahili utaratibu wa mila na desturi yetu ya uchaguzi ambapo anaruhusiwa awamu mbili 2025 – 2035?

Nini maarifa yako, tupe maoni kwa vigezo na ushahidi.
Dawa yenu ni katiba mpya - maana CCM sasa hivi mnapangiana miaka awamu kwa awamu as if Tanzania mnaimiliki nyie.. usishangae mwingine akasema mama akitoka January anakamata 2035 - 2045.
 
Acha upumbavu

Kama umetumwa useme
No problem whatever the description I deserve. Take this for your help.

“Never argue with stupid me, I will drag you down to my level and then beat you with experience, Mark Twain”
 
Ndio, Mabeyo anajua kinachoendelea kuliko Samia.

Kwenye mazishi ya Magu Mabeyo alimwambia Samia ukitulia njoo nikupe siri za nchi.

Yani Vice President Samia alikuwa kikaragosi tu haambiwi siri za nchi!

Mhimili wa Mabeyo unapingana na mhimili wa Kikwete.
Nadhani hujaelewa swali langu? Nauliza mabeyo ndio ameapa kuwa rais wa nchi au?
Sahiz samia ndio president sio vice tena. Una uhakika gani hajapewa hizo siri?
 
Back
Top Bottom