Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Haraka ya nini wakati bado hajaanza muhula wa pili? Haya ya kubadili katiba anaweza akitaka akae na wapinzani waone watabadilije
Ni kuweka maandalizi ya mapema tu kwa sababu muhula wa pili anaanza mwishoni mwa mwaka huu
 
Wewe mchurie tu huyo mkojani wako,watu walitaka kufanya huu ubatili kwa Magufuli na wote tunajua kilichofuata.
 
Mafanikio ya Raisi Samia na yale yote makubwa aliyoyafanya nimeshaandika sana humu jukwaani kwa kina na kirefu sana na kwa ushahidi murua
 
Hatuangalii habari za nafasi bali utumishi wake. Uongozi siyo zawadi bali ni utumishi kwa watu na kugusa Maisha yao
 
Kwa sasa watanzania wanataka Mama aendelee kuongoza Taifa letu. Maana chini ya uongozi wake wameona mafanikio makubwa yaliyopatikana na namna Maisha ya watanzania yalivyo badilika na kuwa yenye Matumaini makubwa sana .
Watanzania wenyewe...ni TUMBO LAKO NA TAMAA ZAKO ZA MADARAKA CHINI YA UONGOZI WAKE, Watanzania wenyewe ni MAFANIKIO YAKO UNAYOYAPATA CHINI YA MAPUNGUFU YA UONGOZI WAKE.

NA SIO WATANZANIA WENGINE...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…