Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Haraka ya nini wakati bado hajaanza muhula wa pili? Haya ya kubadili katiba anaweza akitaka akae na wapinzani waone watabadilije
Ni kuweka maandalizi ya mapema tu kwa sababu muhula wa pili anaanza mwishoni mwa mwaka huu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katiba siyo msaafu wala siyo Biblia. Katiba yetu ilitungwa na wanadamu ambao ni watanzania kwa lengo la kuwa kama muongozo wa masuala mbalimbali ya kuongoza Nchi yetu. Katiba Ni karatasi tu zilizojaa maneno ya namna gani ya jambo fulani lifanyike na hatua zipi zifanyike na kufuatwa katika kufikia hitimisho la jambo fulani.

Katiba yetu ipo kwa ajili yetu watanzania na ni kwa ajili ya ustawi wetu pamoja na Taifa letu kwa ujumla wake. Ni muongozo wa mambo yetu wenyewe.

Nilikuwa napenda kuwaambieni watanzania Wenzangu ya kuwa tufike wakati tutambue ya kuwa viongozi aina ya Rais Samia hawazaliwi kila siku na wala hawapatikani kila Nchi na wala siyo Rahisi kuwatengeneza .

Huyu Rais ni Mchapa kazi kwelikweli,ni mzalendo aliyetukuka na ambaye huwezi kumtilia shaka juu ya uzalendo wake,ni kiongozi mwenye maono,akili kubwa,upeo mkubwa na Karama ya uongozi. Ni kiongozi ambaye amejitoa na kujitolea Maisha yake Kama Sadaka kuwatumikia watanzania.

Ameyatoa Maisha yake kama Zawadi kwa Watanzania. Sasa kwanini tusithamini na kutambua Moyo huo wa upendo wa kipekee wa Rais wetu? Kwanini tusibadilishe katiba yetu ili Mama aendelee kuongoza Taifa letu.

Uzuri wa Mama yetu ni kuwa bado yupo imara kimwili na kiakili. Akili yake inachemka Muda wote na hapa unaweza kuona kupitia mipango yake na mambo makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya hapa Nchini.

Jiulizeni Angela Merkel aliiongoza Ujerumani kwa miaka mingapi.Kumbukeni ya kuwa Ujerumani ndio Taifa lenye uchumi mkubwa sana barani Ulaya. Na ni yeye aliyefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Ujerumani inaendelea kuwa imara kiuchumi.

Sasa kwanini tusimpatie Mama yetu Muda zaidi wa kuongoza Taifa letu ili tufaidi vyema kazi ya mikono yake ? Mnafikiri ni Nchi gani hapa Afrika mashariki na ukanda huu wa kusini Mwa jangwa la Sahara itakayotufikia kiuchumi?

Huyu Hapa Mama wa Shoka Jasiri Muongoza Njia👎View attachment 3225535View attachment 3225537View attachment 3225539View attachment 3225540

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe mchurie tu huyo mkojani wako,watu walitaka kufanya huu ubatili kwa Magufuli na wote tunajua kilichofuata.
 
Ni wazo jema ila kwa Ustawi wa Demokrasia haitavutia sana, maana kuna siku madaraka yataangukia kwa Mwingine alafu akitaka kuvunja katiba kufuata Utaratibu huu italeta shida..

Alafu Mkuu, mheshimiwa anafanya Mengi makubwa ambayo watu wanapaswa kuyajua mfano Kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Hayati Mwl, Ujenzi wa Mashule Mapya nk ndo vitu unapaswa kuwajuza wadau, hizi thread za hivi zinafanya upunguze credibility yako hapa jukwaani na ukizingatia mada zako hua zina mhusu one wa Inji hii, au hukufundishwa law of relativity??
Its simple, rafiki zako wakiwa wanaongea visivyoeleweka wanasababisha na wew rafiki yao uonekane wa hivyo hivyo. Unavyofanya sio vizuri kwa kweli
Mafanikio ya Raisi Samia na yale yote makubwa aliyoyafanya nimeshaandika sana humu jukwaani kwa kina na kirefu sana na kwa ushahidi murua
 
Hivi unawazaga kwa kutumia makalio?

Vipi kama Mwinyi angeamua kubadili katiba aendelee kuongoza, Mkapa angepata wapi nafasi ya kuwa Raisi?

Vipi kama Mkapa angeamua kubadili katiba aendelee kuongoza, Kikwete angepata wapi nafasi ya kuwa Raisi?

Vipi kama na Rais Kikwete angeamua kubadili katiba aendelee kuongoza baada ya miaka yake kuisha,
Unadhani Mama angepata wapi nafasi ya kuwa Raisi leo hii?

Acha kuwaza kwa kutumia makalio you phoooool...
Hatuangalii habari za nafasi bali utumishi wake. Uongozi siyo zawadi bali ni utumishi kwa watu na kugusa Maisha yao
 
Kwa sasa watanzania wanataka Mama aendelee kuongoza Taifa letu. Maana chini ya uongozi wake wameona mafanikio makubwa yaliyopatikana na namna Maisha ya watanzania yalivyo badilika na kuwa yenye Matumaini makubwa sana .
Watanzania wenyewe...ni TUMBO LAKO NA TAMAA ZAKO ZA MADARAKA CHINI YA UONGOZI WAKE, Watanzania wenyewe ni MAFANIKIO YAKO UNAYOYAPATA CHINI YA MAPUNGUFU YA UONGOZI WAKE.

NA SIO WATANZANIA WENGINE...
 
Back
Top Bottom