Mnaopenda kuomba Namba za Simu za Wanawake ndani ya Daladala muwe mnachunguza kama Madume zao tupo nao au hatupo

Kuomba namba sio issue. Hata kama amelewa na ndoa
 
Haya
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Sawa, msani mura amang'ana!
 
Kipigo chake kilikuwa kipigo cha mbwa koko au sio?
Alhamdullilahi namshukuru Mola Muumba wa vyote kwa kunijaalia mafanikio ya kutunukiwa Degree ya Pili (2nd Dan) ya Sanaa ya Kujilinda kwa Mikono Mitupu ama Karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu kutoka kwa Mwalimu wetu Mkuu wa @jundokan_tanzania Sensei @fundi_romi_ siku ya Ijumaa Juni 17, 2022.

ANGALIZO: Jamani ndugu zangu sanaa hii ni ya kujilinda kiafya, kiakili, kinidhamu na ki-utii na sio kupigana na mtu au watu. Ndio maana nina miaka takriban 40 nafanya Karate lakini hadi sasa ni wachache kweli waliojua nacheza sanaa hio.

Ni kweli kabisa sikupenda na sikuwa najionesha hadharani kwamba mimi ni Karateka, na hii kutoka hadharani sasa ni kuwatia moyo na hamasa watu wa umri wowote ama jinsia yoyote kwamba Karate ni sanaa ya kujilinda kiafya, kiakili na kinidhamu. Mie imenisaidia sana kwa kweli!

Ukikuta Karateka mbabe au mpenda shari basi tambua kuwa huyo jamaa ni aidha feki au hajaiva kisawasawa.

Kwa mwenye nia ya kujiunga nasi karibu DM kwa maelezo kamili.
 
Mkuu nimecheka sana kwahiyo unasema Mimi ni mwana Karateka Feki? Uko wapi tumtafute 'Cameraman' wa JamiiForums atufotoe tukiwa tunazichapa 'Kavukavu' mpaka Mshindi apatikane kati Yetu?Ila Sharti Kuu huyo 'Cameraman' akiwa anatupiga asiwe anatuonyesha Sura zetu kwani na nilivyo Handsome Mademu JF watanisumbua.

Ila ukweli ni kwamba GENTAMYCINE sijafanya hilo Tukio na ukweli ni kwamba hata Kupigana kwenyewe tu sijui ila nimeleta tu Kwenu huu Uzi huku nikiu 'dramatize' Kwenu ili tu Watu ( hasa Sisi Wanaume ) tuachane na hii tabia kwani Jana nimeshuhudia Mtu akichezea kichapo ndani ya Dala Dala kwa Kumlazimisha Dada wa Watu ampe namba yake ya Simu kumbe Mwamba alikuwa nyuma yake na anamchora tu huku akiusoma Mchezo wake mzima.

Unachonishangaza Matola tuko hapa JamiiForums muda mrefu ( miaka mingi tu ) ila bado hujaweza Kunisoma Vyema.

Cc: adriz
 
Dojo lako lipo wapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…