Mnaopokea salary take home chini ya milioni moja, huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Mnaopokea salary take home chini ya milioni moja, huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Mshahara haijawahi kutosha.

Juzi tumemsikia. Sa100 akilalamika kuwa ongezeko la 23% haikumfikia.
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakua nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Duuu mbona unajibana sana mkuu unawezaje 1.29m unawezaje kutoboa wiki mbili?
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakua nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Wewe huna akili utawezaje kupanga bajeti?Haujajiuliza kwa wale ambao hawana mshahara wanawezaje kuishi?
 
Kwa kutegemea na standard ya maisha unayoishi na ukubwa wa majukumu nakubaliana na wewe kwamba hizi salary za kibongo ni mtihani.

Imagine unatumia gari binafsi kwenda na kurudi kazini na labda umepanga nyumba maeneo yanayoendana na hadhi yako inakuwa ni majanga.

Ndo maana serikali ingerudisha japo allowance za nyumba, usafiri, maji, umeme kuwapunguzia watumishi wakiwemo walimu ugumu wa maisha unaotokana na mishahara midogo.
 
Huo mshahara mbuzi sana nikajua labda milioni 4.5 kumbe unalipwa utopolo mtupu wa kifeitoto, 🤣🤣🤣
 
Nikajua ni mimi tu na huwa najihisi nimerogwa, ndo kwanza leo tar.4 sina kitu, ila ninachojifunza ni kuwa kadri take home salary inavyokuwa kubwa ndivyo dependants wanavyoongezeka.
Mnaosomesha wadogo zenu nadhani mtaniunga mkono
Sure mkuu
 
Back
Top Bottom