Mnaopokea salary take home chini ya milioni moja, huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Kuna mwalimu wa sekondari anae pokea hiyo pesa kweli?
Mwalimu wa sekondari au msingi hadi anastaafu hawezi kuwa na TAKE HOME ya 1.29M hapo kafanya kazi 35 years ana degree yake, meanwhile kuna mtu kaanza kazi pake TANAPA ana mwezi mmoja kazini ana certificate tuu anakunja take home ya zaidi ya 1.3M per month.
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakuwa nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Hivi mnaopokea salary baada ya mwezi huwa mnaishi vipi asee?

Mimi nishazoea kuingiza pesa kila siku kisha naitumia nitakavyo sasa sijui wenzetu mnasavaivu vipi kudadadeki

Yaani unafanya kazi siku 30 kisha ndo unashika hela !!!!!!!

Hapana asee nilishashindwa hiyo staili ya maisha
 
Kuna watu wanalipwa laki 80 wanaishia Dar na maisha yanasonga
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakuwa nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Hakuna pesa inayotosha wengine tunawaona wana mishahara ya 4m huko na bado bado hawaishi kwa amani, madeni juu
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakuwa nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Je una familia? Ina ukubwa gani, mpo wangapi kwenye familia hiyo? Kama una familia, watoto wanasoma/unlipa ada? Unaishi kwako au umepanga? Unatumia usafiri binasfi, kukodi au ni wa jumuiya? Una bajeti yako ya mwezi/mwaka?

Hebu jibu hayo maswali kwanza then utaona kwa nini.
 
Mwalimu wa sekondari au msingi hadi anastaafu hawezi kuwa na TAKE HOME ya 1.29M hapo kafanya kazi 35 years ana degree yake, meanwhile kuna mtu kaanza kazi pake TANAPA ana mwezi mmoja kazini ana certificate tuu anakunja take home ya zaidi ya 1.3M per month.
Mwalimu wa sekondari mwenye degree ya sayansi na uzoefu wa miaka kama 30 anaweza kupata zaidi ya hicho kiasi.
 
Sasa hadi afanye kazi miaka 30 tena mwenye degree mkuuuu emu acha utani asee kuna kajamaa kapo pale TRA TANESCO TARURA TANROADS BOT REA RUWASA NSSF PSPF PPF, etc kana certificate ya HUMAN RESOURCE MANAGEMENT kana mwezi mmoja kazini kana take home ya 1.3m
 
Mwalimu wa sekondari au msingi hadi anastaafu hawezi kuwa na TAKE HOME ya 1.29M hapo kafanya kazi 35 years ana degree yake, meanwhile kuna mtu kaanza kazi pake TANAPA ana mwezi mmoja kazini ana certificate tuu anakunja take home ya zaidi ya 1.3M per month.
Huna udhibitisho kiongozi, huo mshahara kwa mwalimu mbona wa kawaida kuna walimu wamekaa tu miaka 10 na kuendelea wanakunja 1,300,000, TGTS F, akianzia degree
Nadhani wewe unachanganya na certificate
 
Watu tunatofautiana kwenye vipato lakini pia kwenye matumizi. Tofauti ya matumizi hujitokeza kwenye:
1. Aina ya usafiri
2. Aina ya chai na sehemu unapoipata
3. Aina ya chakula cha mchana na usiku
4. Matumizi ya simu
5. Kiwango cha kodi ya nyumba
6. Gesi, chakula cha nyumbani, mazagazaga
7. Aina ya mavazi
8. Michango ya kijamii
9. Huduma ulizomzoesha mke/mpenzi
10. Aina ya uwekezaji
11. Kiasi cha akiba unayoweka kwa mwezi
12. Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki
13. Burudani
Hapa ndo utasikia mlinzi anajenga halafu boss anapanga.
 
Mwalimu wa sekondari mwenye degree ya sayansi na uzoefu wa miaka kama 30 anaweza kupata zaidi ya hicho kiasi.
Mshahara hautofautiani kati ya mwalimu wa Sayansi na sanaa kuanzia 2022 kurudi chini, kuwa na uthibitisho
 
400000 ukiwa na akili unafanya mambo yako poa tuu,napokea chini ya hapo nalipa rent 130000,Nina watu 5 nyuma yangu,nanunua gesi ,kulipia umeme ,chakula ,ni kupambane tuu mkuu,
 
Huna udhibitisho kiongozi, huo mshahara kwa mwalimu mbona wa kawaida kuna walimu wamekaa tu miaka 10 na kuendelea wanakunja 1,300,000, TGTS F, akianzia degree
Nadhani wewe unachanganya na certificate
Hicho kitu hakipo kwa sasa labla huko 2014 kushuka chini hata hivyo miaka hiyo mishahara ya Ualimu ilikuwa haijafika huko. TGTS D1 ilikuwa 630K.

Kuanzia 2015 watu wamekaa miaka 8 wengine 7 bado wapo TGTS D1, Samia ndio kawapandisha 2022 kwenda TGTS E1.

Kwa kifupi ...

Kufika TGTS F1 ndani ya miaka kumi itategemea na factor nyingi mno wengi uwachukua hata miaka 15.
 
Mshahara hautofautiani kati ya mwalimu wa Sayansi na sanaa kuanzia 2022 kurudi chini, kuwa na uthibitisho
Ni kuanzia 2020 kurudi chini Ajira za mwisho za Magufuli zile za December 2020 ndio Walimu wa Sayansi na sanaa zilitofautiana.

Sayansi TGTS D3 na

Sanaa TGTS D1
 
Back
Top Bottom