Mnaoshinda mitandaoni mnafanya kazi saa ngapi?

Mnaoshinda mitandaoni mnafanya kazi saa ngapi?

Tukiachana na maisha yao binafsi.
Hata mimi najiulizaga sana kuna ID masaa 20-24 ziko online zinachangia kila mada na kujua almost everything
Utasema ni robot [emoji1] hivi wenzetu hawanaga ubusy au ndo matajiri!!! Huwa inanishangazaga sana hii kitu
Hiyo tabia ya kushinda mitandaoni ndiyo huwasaidia kujifunza vitu vingi sana, ni vile unaona wanajua almost everything.
 
Wewe ambae unataka kua offline endelea hivo hivo lakini wengine michongo yao inawalazimu awe online na asitoke nje ya mtandao na anakua anapiga pesa kama kawaida, sasa wewe fanya yako na wengine wafanye yao
Mfano wanaobet umempa Man U ushindi lazima ulinde Cashout vinginevyo anatoa draw
 
Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha

Sisi walinzi vipi
 
Sio kila MTU anakazi ya kutoka jasho full hekaheka mkuu,wengine tumejiajir ukifika job unakaa tu kazi yako kuagiza hahahah PC au simu ina bundle hata kulog off huwa hatulog( sio Mimi lakini)
 
Mtandaoni ndio kwenye kazi zetu. Usipotuona mtandaoni jua tumetoroka kazini.
 
Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha
1. Wana access na mitandao masaa 24.
2. Wengi wana uwezo wa kulipia huduma ya internet.
3. Wengi wana nafasi baada ya shughuli zaop zingine.
4. Wapo wenye kufanya kazi mitandaoni kwa malengo mbalimbali.
5. Wengine ndo wanoiendesha nchi hii kwa kuchukua ideas kutoka mitandaoni hivyo mitandao ni sehemu ya kazi zao.
6. Wengine ni kama alivyosema jamaa hapo juu hawana kazi maalum ila wana uwezo mkubwa wa kushinda JF hata masaa 24.
7. Wengine kama mimi tumeopata wito tu wa kuingia JF kutafuta tu kuelimishana kuhusu masuala kadha wa kadha.

Hiyo pesa ndo wawekeza kwenye biashara ndogondogo kama kuchoma chips, car wash, berber shop na zingine. Mimi kibanda changu pale Kwamtogole bado chalipa (nilikifungua 2015) na vijana wangu wapiga kazi kwelikweli. Hivyo nikirudi kule Kibaigwa naingia JF naanza kazi.

Ukiwekeza pesa yako kwenye mifuko kama Vanguard Investment, weye wafuatilia tu mitandaoni ile interest ndo huwa mlo wako. Unakuwa umewekeza kama $50,000 kama kianzio.

Kuna siku waiona kabisa $3000 imeingia waipigia hesabu ndo utaona mtu yupo Dubai na kadhalika.

Hivyo watu hawakai bure hapa JF wengi watumia fursa zilizopo za mitandao.

Halafu usisahau kwamba JF ina majukwaa mengi hivyo kila mwanachama ana uchaguzi aingine jukwaa lipi.

Yaani JF is so Cool.
 
Wengine ndiyo kazi yao hiyo,ameajiriwa kudeal na social media tu,amepewa target kuhakikisha taasisi yake haichafuliwi kuanzia Dini,vyama vya Siasa, Taasisi za Umma, Taasisi za Bank etc.......ndiyo maana mtu kama huyo kila kinachoingia Jeiefu lazima akione
Oooh hao wapo na wanaanzishaga mada za kuponda kuwachota na wanaoranda randa wapo
yote kwa yote si tunadhangaaga tu
 
Tukiachana na maisha yao binafsi.
Hata mimi najiulizaga sana kuna ID masaa 20-24 ziko online zinachangia kila mada na kujua almost everything
Utasema ni robot [emoji1] hivi wenzetu hawanaga ubusy au ndo matajiri!!! Huwa inanishangazaga sana hii kitu
Wakati wewe unafanya kazi.

Wenzako wengine pesa zao zinawafanyia kazi Wala hawahitaji kuvuja jasho.

Siku hizi maisha sio magumu kama unavyodhani ni kujiongeza tu wapi ujiweke maisha Yako yaende vizuri.

Sio lazima kuvuja jasho zama hizi za information age
 
Back
Top Bottom