Mnaoshinda mitandaoni mnafanya kazi saa ngapi?

Mnaoshinda mitandaoni mnafanya kazi saa ngapi?

Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha
Wao pamoja na wewe mwenyewe hamna kazi.
 
Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha
Tunafanya digital Marketing so kukaa online ndio kazi yenyewe…
 
Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha
Mkuu; Inafaa uzingatie "Penye wengi pana mengi". Mitandaoni ni kama kijiweni lakini ni zaidi ya kijiwe kwani humu wapo: Wanaofanyabiashara(Halali na Haramu)
Wapo wanaojifunza maarifa (kuelimishana)kutoka kwa wenzao e.g GTs
Wapo wakorofi na matusi yao,vijembe na umbeya etc
Wapo wanaopita humu kama sehemu ya starehe na kuondoa stress
Wapo watoa Taarifa (Wapashaji) zaweza kuwa za uongo au zaUkweli au ni Tetesi n.k.n.k.
Kwa kifupi kila mtu umwonaye humu jamvini anasababu ya kufika hapa. Je, ww ni kitu gani kimekuleta hapa leo na sio jana au ungesubiri ikawa kesho?
 
Nimejiuliza hili pia leo

Ukifuatilia michango yao utajua kama sio mwanafunzi basi amemaliza shule yuko mtaani.

Kuna wale wenye shughuli za kuunga unga 😂
Hawa ndio wanaongoza kwa matusi humu na maneno ya shombo

Nakumbuka old days kuna ID ilikua ikinitukana sana jamvini tena kwa uzushi na uongo
Kuja kumfuatilia kumbe ni kijana tu yupo gereji magomeni na tecno pop yake akiwa free anashinda humu
Mkute sasa anajitanabaisha humu utajua Afisa usalama huyu hapa 🙌🏽😁
Usituchukulie poa mafundi Garage.

Kuna Jamaa yangu nimuhandisi anafanya kazi kiwandani kama Maintenance manager, chini yake ana mtu mmoja mwenye degree ya Mechanical engineer, huyu ndio anachukua order zote kutoka Kwa maintenance manager. Pia chini ya huyu mwenye degree Kuna technician wawili.

Chini ya hawa technician Kuna artisan Zaid ya 35. Sasa kazi ya Maintenance manager nikutuma tu report weekly report Kwa directors, nakazi ya Mechanical engineer nikuchukua taarifa tu Kwa maintenance manager nakuzipeleka Kwa technicians na Artisan. Ukiangalia chain ilivyo wanaofanya kazi muda mwingi ni technicians wakisaidiana na artisan kazi ya engineer ni ku oversee tu. Nakazi labda zikiwashinda hao wadogo Engineer ndio anaingia na ikiwa kubwa zaidi ndio anakuja maintenance manager anatoa maelekezo namna ya kuitatua.

Sasa mtu kama huyo Maintenance manager na Mechanical engineer wake unaweza waona mtandaoni muda mwingi ukafukiri hawana issue. Nakitu kingine wanatumia WiFi ya ofisi. Sasa uliza mshahara wao utakuta Maintenance manager anachukua kuanzia Mil 5 mpaka Mil 7, Engineer wake unakuta anachukua kuanzia mil 2/3 nakwasababu kazi zao ni ku oversee tu unakuta wapo kazini hawana issue nyingi zakufanya wanabidi waingie mtandaoni kupoteza muda.

Kwahio mkuu ukimuona mtu mtandaoni Kila siku sio kwamba Hana kazi yakufanya.
 
Hii mitandao ya kusoma tu na kuandika huwa naona haina shida, kuna wadau kule Club House yaan wanabishana 24/7, unabaki unajiuliza hawa wanafanya kazi saa ngapi, achilia kufanya kazi je wana familia kweli?
Kuna mke au mume atakukuruhusu upayuke tu mtandaoni masaa yote?

Ila mwisho wa siku mambo yao tuwaachie wenyewe [emoji1]
 
Umofya kwenu members! Umofya tena !!!

Niende moja kwa moja kwenye mada, Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua baadhi ya watu kushinda mitandaoni muda mwingi si asubuhi mchana wala jioni.

Swali langu ni mnafanya kazi saa ngapi kama kutwa kukicha mitandaoni? Mnamajukumu kweli ?
Tutafikia maendeleo kweli kama taifa?

Nawasilisha
Pilipili usioila yakuwashia nini? 😀
 
Back
Top Bottom