Mnaotaka kuingia USA pitieni BAHAMAS πŸ‡§πŸ‡Έ

Hajui kuwa hizo Kaz za hovyo kwa USA malipo yake ni kama ya mbunge kwa mwezi
Dogo pesa anayolipwa mbunge huku kwa mwezi kule marekani inaishia kwenye kodi ya nyumba na serikali tu, sasa we jifariji udhani kwamba pesa ya mbunge hapa kule ni kubwa sana, kiasi kwamba unaweza uka spend na bado eti ukafanya savings nyingi
 
Kila kitu mnajigharamia wenyewe mkuu
 
duh mbona mtiti sasa 😁😁😁 hapo ndo unaonaga wa tz anakwenda ambaye hakuchaguliwa. Binafsi wakinichagua ukiachana na gharama ya passport tu vingine siwezi muduπŸ™†πŸ»β€β™‚οΈ
Yeah siyo mchezo naona pia ndio namna ya kupunguza kiaina idadi ya wanaoenda, maana jumla ya Gharama za visa, medical, pamoja na interview pale ubalozini tu siyo chini ya $1000, hapo bado safari na pesa ya kuanzia maisha ukiwa kule kwa kipindi ambacho utakuwa unatafuta kazi
 
Sasa hela yote hiyo si bora ufungue duka genge nje ya mji akauza na mivinyo tofauti tofauti....ukapiga hela then usa unaenda kama mfanyabiashara baada ya kuzuru china.
 
Wakinichagua ntaleta mrejesho hapa mtanichangia NITANGULIE NIKAWAANDALIE MAKAO KWA BABA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ili ntakapokuwepo na ninyi muwepo
 
Kama unataka kwenda Bahamas - utafikia Nassau Paradise Island. Hapo ndipo unapoweza kuanza mipango ya kutoka Free Port (Bahamas) kuelekea Fort Lauderdale ( Pwani ya Miami - Florida)

Sasa kabla hujatamani safari zingatia mambo yafuatayo:-

Ni kweli kuingia unahitaji Passport lakini pia vigezo vya wewe kutoishia Uwanja wa Ndege na kurudishwa ulipotoka ni pamoja na
1. Passport ambayo haijaisha muda wake (Hii umeshaeleza); hapa walau iwe na miezi sita ya kabla ya kuisha muda wake ( Hili sio tatizo maana Vijana wengi wa Kitanzania wana passport).

2. Uwe na tickect ya kurudi ulipotoka ama uwe na ticket inayoonyesha kituo kingine baada ya Bahamas ( Hapa sasa vijana ndio huwa wanajilipua kwa kuwa na ticket ya ndege ya kurudi Bongo huku kichwani akiwa hana huo mpango wa kurudi.
Hii ni muhimu ili upate muda wa kupanga mipango yako ya kuzamia Florida na usipate usumbufu kutoka kwa maafisa wa Uhamiaji wa Bahamas; ni wasumbufu na wapo kila mahali.

3. Ushahidi wa kuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yako ukiwa Bahamas; hapa sasa ni muhimu sana maana ukishuka hapo Nassau na una Dola 200 jua kuwa watakushikilia hapo uwanja wa ndege na watakurudisha uwanja wa ndege wa Dar es Salaam pale Kipawa karibu na Majumba sita. Hapa sasa ndipo matumizi ya kadi za Benki za Visa Card huwa yanaonekana. Wakitaka ushahidi unaonyesha salio lako la kwenye kadi ya benki.

Hitimisho; licha ya kuwa gharama za safari kwenda Nassau - Bahamas ni ndogo walau USD 2500/- zingatia kuwa na hela nyingine ya ziada ili walau uguse ardhi ya Marekani. Ukitoka hapa na ticket ya kwenda tu kuwa na uhakika, utaishia kuangalia majengo ya Uwanja wa ndege wa Nassau na tutakuja kukupokea pale Dar tena ukiwa na kesi ya kujibu kwa serikali ya Dokta Samia.
 
Sasa hela yote hiyo si bora ufungue duka genge nje ya mji akauza na mivinyo tofauti tofauti....ukapiga hela then usa unaenda kama mfanyabiashara baada ya kuzuru china.

Ndio hivyo mkuu Watu wanataka ile heshima kwa ndugu na marafiki ya kuonekana wanaishi US hata kama wanafanya kazi wasizofurahia kabisa
 
Soma tena vizuri comment yangu, sijakataza watu wazamie ila wasiwadanganye wenzao kwamba ni rahisi kiasi hicho, tena ukizingatia kwa nchi yetu ambayo haina uraia pacha na passport tu kupata ni ishu
kiufupi safari sio kitu cha kila mtu maana wapo wengi walioenda unyamwezini kutembelea ndugu na wakarudi na hawana hata wazo la kuzamia....hivyo hiyo ni hobby ya mtu binafsi
 
Soma tena vizuri comment yangu, sijakataza watu wazamie ila wasiwadanganye wenzao kwamba ni rahisi kiasi hicho, tena ukizingatia kwa nchi yetu ambayo haina uraia pacha na passport tu kupata ni ishu
Uliomba passport ukanyimwa? Ttzo wabongo mnapenda kulalamika fuata utaratibu ukinyimwa uje ulalamike..and hao wenye uraia pacha kwani wao wanaenda kiwanja visa free...?kitu kingine tz unaweza kuwa na uraia hata wa nchi tatu na ukabaki kuwa mtz na mtu asijue as long as passpot ya tz unayo
 
Hehehe,Kwa hiyo na walimu wafanye hivyo?@mpwayunguvilage
 
kiufupi safari sio kitu cha kila mtu maana wapo wengi walioenda unyamwezini kutembelea ndugu na wakarudi na hawana hata wazo la kuzamia....hivyo hiyo ni hobby ya mtu binafsi
Watu wengi wanaenda kiwanja siyo kwa sababu wanapenda kusafiri bali wanaenda kutafuta maisha, sababu ya umasikini na ugumu wa maisha ulioko kwenye nchi zao, na wengine ni kutaka tu ile heshima kwa ndugu na jamaa kuwa wanaishi kwenye hizo nchi
Hapa sijiongelei mimi passport ninayo muda sana ila naongea kwa niaba ya watanzania wengi ambao wakienda pale uhamiaji, wananyimwa passport kwa sababu za kipuuzi kabisa ilihali wana documents zote basi tu ili mradi mtu ajiongeze awape rushwa, wewe usijifanye mgeni kwamba hujui jinsi mamlaka za hii nchi zinavyofanya kazi

Kuhusu watanzania kuwa na uraia wa nchi tatu labda unaongelea wale mafisadi na watoto wao ambao wakivunja sheria wanalindana hilo linajulikana, ila ni mtanzania gani wa kawaida mwenye uraia wa nchi tatu kama ilivyo kwa wanigeria au wakenya, yani unaandika kama vile ni jambo dogo tu wakati ni kinyume na sheria za hii nchi

Ofcourse uraia pacha unachangia kwa kiasi chake nchi nyingi kuwekeana visa free entries, ukibania uraia pacha kwenye nchi yako hata wenzako wengi nao watabania raia wako kuingia kwenye nchi zao, nchi kubwa nyingi ukitaka uzamie kirahisi ni hadi uwe na uraia wa zile nchi za kawaida ambazo zina visa free entries kwenye hizo nchi
 
duh mbona mtiti sasa 😁😁😁 hapo ndo unaonaga wa tz anakwenda ambaye hakuchaguliwa. Binafsi wakinichagua ukiachana na gharama ya passport tu vingine siwezi muduπŸ™†πŸ»β€β™‚οΈ
Orodhesha vitu unavyohitaji wakupe/wakulipie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…