Mnaotaka kuingia USA pitieni BAHAMAS πŸ‡§πŸ‡Έ

So unahitaji wakuandalie kama budget ya Tshs ngapi?
Sijajua kwani sina uzoefu na masuala ya safari za nje ila kwa wajuzi walisema kupitia threads moja hivi kuwa maximum ya bajeti inaenda mpaka 10 milion kulingana na jimbo unalotaka kwenda kuishi
 
Siwezi tena kwenda marekani.
Mimi na baadhi ya watanzania wenzangu tumekuwa tukiehindia kula ukoko wa wali wakati huku nyumbani vyakula bwerere.
USA hapana aise.
Bongo patamu sana siondoki tena.
 
Mkuu tupe uzoefu wako. Mimi nina mpango wa kuingia USA nipo kwenye mchakato wa kujikusanya financialy
 
Ukishindwa kutafuta maisha hapa tz!!! Usijidanganye popote wewe Blai!!! Watu wapi USA mwaka wa 20 wanaona aibu kurudi!!!asikudanganye mtu!??
Unataka kuniambia Elon Musk angekuja kufanya mishe zake Tz angetoboa kwa level aliyopo sasa hivi? Kiteknolojia, kiuchumi uwezekano wa kutoboa Marekani ni mkubwa ukilinganisha na Tz. USA nchi ya fursa ile we ubunifu wako tu unatoboa labda kipingamizi kiwe makaratasi. Mange kimambi mbona anakula maisha fresh tu, unafikiri angebaki Tz leo hii angeweza kuingia barabarani na G-wagon?
 
Mkuu punguza negativity. Mambo mengine acha watu wafike wakayakute uko uko tu sio kuanza kutishana. Wewe kama unaona kuna posibility yoyote ya kuingia uko States mwaga nondo masuala ya makaratasi sijui deportation acha wapambanaji tukakutane nayo uko uko.
 
Mkuu naomba kujua gharama za maisha hapo Bahamas zipo vipi ni kiasi gani kinaweza kukutosha kukaa kwa kipindi ambacho unapanga mipango wa kuzamia states na pia kutoka hapo bahamas mpaka states ina-cost kiasi gani bila kusahau ukikanyaga states suala la makazi na hustles unaanzia wapi na ni kiasi gani kinaweza kutosha kwa kipindi kifupi ambacho utakua unatafuta kibarua cha kujishkiza.
 
Mkuu tupe uzoefu wako. Mimi nina mpango wa kuingia USA nipo kwenye mchakato wa kujikusanya financialy

Huwa nakeleka sana na watu wanaishia kupinga tu bila kutoa suluhisho. Jamaa kaeleza njia za kufika USA anakuja mtu anasema haiwezekani halafu hatoi alternative yoyote

Tatizo mkipewa hizo alternatives mnadai mnatishwa sijui mnakatishwa tamaa, njia za uhakika ni kupata kazi au scholarships, kushinda dv lottery, kupata tourist visa au kufunga ndoa na raia wa huko (hata ya mchongo), na hizi njia zote hazihitaji unga unga mwana lazima uwe na pesa kidogo

Hapo ukifanikiwa kupata visa kupitia njia yoyote kati ya hizo ukishafika kule sasa ndio unazamia moja kwa moja, unafanya kazi za chini ya meza huku ukitafuta green card, tatizo watu hizo njia hawazitaki sababu hizo zote ni lazima upitie ubalozini in short watu wanataka kuzamia bila visa

Yani wao wanataka kusikia zile njia za alizamia kwenye meli ya mizigo sijui alijificha kwenye matairi ya ndege, au sijui aliomba visa ya nchi fulani kisha alivyofika akaungaunga hadi akazamia marekani, sasa hizo njia siyo za uhakika kuna asilimia kubwa za kufeli na kuwa deported
 
mgogo in USA
 
Izo izo njia ambazo unaziita sio za uhakika kama kuna uwezekano wa kupenya hata kidogo tu we shuka madini.
 
Izo izo njia ambazo unaziita sio za uhakika kama kuna uwezekano wa kupenya hata kidogo tu we shuka madini.
Hizo njia ambazo siyo za uhakika ndio hizo ambazo nilisema ni za uongo na wengi huishia kuangukia pua, hoja hapa ni kwamba huwezi kuzamia nchi za watu kirahisi kama unavyotaka ingekuwa inawezekana kirahisi hivyo si kila mtu angetumia njia hizo, mimi nimepinga njia zisizo za uhakika ili nitaje njia za uhakika halafu wewe unaniambia tena nitaje zisizo za uhakika sasa kama unataka zisizo za uhakika si ndio utumie hiyo njia ya mleta mada
 
Kila mtu anajua alichosema mleta mada sio njia ya uhakika lakini kuna walioitumia wakafanikiwa kwaiyo uwezekano upo. Maisha yana risk nyingi sana ni suala la ujasiri wako tu, anyway kama hauna maujanja tulia fuata utaratibu kwenye kila jambo ili utoboe kwa izo njia zako halali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…